WANANCHI WILAYANI MTWARA WATAKIWA KUWA NA USHIRIKIANO MZURI NA WATUMISHI WA UMMA

Wananchi wametakiwa kuwa na mahusiano mazuri na wataalamu mbalimbali wanaoletwa na serikali katika vijiji vyao kwa kuwa pamoja nao na kujenga ushirikiano chanya baina yao ili wapate kile wataalamu hao walichonacho.

Akizungumza katika kikao cha maendeleo ya Tarafa ya Mpapura mkuu wa wilaya mtwara Bi Fatuma Alli amesema kuwa wananchi wanapaswa kuwatumia vizuri watumishi wanaoletwa na serikali  katika vijiji vyao kwa  kushirikiana nao na kuondoa dhana iliyopo yakuwa watumishi hao wanatumia vibaya nyazifa walizopewa na serikali.

Akihusisha tukio lililotokea hivi karibuni katika  zahanati ya Mkunwa iliyopo katika halmashauri ya mtwara vijijini ambapo wananchi wa kijiji cha mkunwa  walimzuia na kushinikiza  mkuu wa wilaya  wakimtaka kumuondoa mara moja Mganga mkuu wa Zahanati hiyo Bi Issabelah.

Mganga Issabelah amekuwa na tuhuma ya  kuwa na lugha chafu ,kejeri na majivuno kwa wananchi na wagonjwa wanaofika katika zahanati hiyo.


Kwa upande wa kaimu mkurugenzi na mganga mkuu wa mtwara Dk Juma Gumbo amesema kuwa baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wa kijiji hicho  Halmashauri ya mtwara wameamua kumtoa mganga katika Zahanati  na kumpeleka katika kituo cha Afya cha Mahurunga kilichopo katika halmashauri ya mtwara akiwa mganga wa kawaida toufati na awali alipokuwa mganga mkuu.

Kwa upande wa  REDIA MNYANI muuguzi mkunga wa zahanati hiyo alipoulizwa na kuhusiana vitendo hivi vya wananchi kutokuwa na ushirikiano mwema  baina yao alisema kuwa tatizo lililopo ni kwamba wananchi kutofahamu changamoto zilizopo za upatikanaji wa dawa katika nchini na upotoshwaji uliopo juu ya kauli za wanasiasa ya kuwa uwepo wa dawa pungufu katika vituombambali hapa  vya afya hapaa nchini huchangia na wahudumu hao.



Hali ya wananchi kutokuwa na imani dhidi ya watumishi wa umma hasa madaktari katika mkoa mtwara ni mara baada ya ujio wa waziri mkuu Kassim Majaliwa Kassim katika hospitali ya rufaa ya mkoa Ligula mwezi February na kumsimamisha kazi mganga na kutoa onyo kwa mganga mfawidhi hospitali hiyo na kukataza uwepo wa maduka ya madawa karibu na kituo cha fya kitendo kilichochukuliwa na kutafsriwa vibaya na wananchi wa mkoa wa Mtwara. 

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI