MAISHA NA UGONJWA WA KISUKARI

Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) ni ugonjwa sugu unaotokea wakati fisiolojia ya mwili inaposhindwa kuratibu kiwango cha sukari katika damu. HIvyo sukari hupanda kwa kiasi kinachozidi kawaida na kusababisha matokeo hasi mbalimbali mwilini.
Baadhi ya matokeo hasi yanayoletwa na kisukari ni Kupatwa na mgandamizo wa damu (presha), Upofu unaosababishwa na kuharibika kwa Retina ya jicho (retinopathy), magonjwa ya figo (nephropathy), magonjwa ya neva za fahamu (neuropathy), Kuharibika kwa mirija ya damu (diabetic angiopathy) nk.
Magonjwa ya neva za fahamu na mirija ya damu huweza kusababisha vidonda sugu visivyopona na kupelekea ulazima wa kukatwa mguu au mkono kutegemea na eneo kilipo kidonda. Kwa hiyo moja kati ya changamoto kubwa kwa mgonjwa wa kisukari ni kuepuka majeraha. Njia mbali mbali zaweza kusaidia kuepuka matokeo hasi ya ugonjwa wa kisukari.
1. Kuacha kabisa kuvuta sigara.
2. Kufanya mazoezi mepesi (aerobic exercise) ili kuchangamsha mzunguko wa damu.
3.Kupunguza kunywa pombe
4.Kuzingatia vyakula vyenye sukari ghafi kwa wingi (kwa maelekezo ya daktari).
5.Kuacha kutumia vyakula vyenye sukari nyepesi kwa wingi mfano soda, juisi za viwandani, biskuti,pip ink.
6.Kupima sukari mara kwa mara ili kujua kiwango cha udhibiti wa sukari katika damu.
7.Kuzingatia vema ratiba ya dawa za kisukari.
8.Kuhudhuria kliniki bila kukosa kwa mujibu wa ratiba.
9.Kuzuia uwezekano wa kupata majeraha miguuni, kuwa mwangalifu na vifaa vyenye ncha kali, kuvaa viatu laini na vyepesi, vinavyoruhuwu hewa kuingia miguuni, vyenye sponji kwa ndani,kuva viatu utembeapo barabarani,kusafisha kinywa na kusafisha miguu.
9.Mjulishe daktari wako unapoona lengelenge, uvimbe, mchubuko au mabadiliko miguuni.
Asante.
Dr. Chris CyriloCyrilo
Kidonda cha mguu wa mgonjwa wa kisukari. (Diabetic foot ulceulce)

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI