UVCCM TEMEKE WAFANYA USAFI MANISPAA YA MTWARA MIKINDANI
Katika kuunga mkono harakati za Rais wa jamhuri ya muungano
wa Tanzania Dk John pombe magufuli kuweka mazingira katika hali iliyo safi na
usalama Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi
{CCM} mtwara mjini wameungana na wenzao kutoka wilaya ya TEMEKE jijini Dar es Salaam kufanya usafi katika maeneo mbalimbali
ya mji wa mtwara.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii kaimu katibu wa umoja
wa vijana wilaya Bi Modesta Mwaya amesema
kuwa usafi ni jambo bora na kuhimiza kuwa wananchi wanatakiwa kufanya usafi
katika mazingira wanayo ishi ili kuweka safi mazingira na kujikinga na milipuko
ya magonjwa isiyo na ulazima.
Bi mwaya amesema kuwa ujio wa umoja wa vijana kutoka temeke
jijini Dar es Salaam ni katika kutengeneza ushirikiano mwema baina yao na
kukikijengea chama kuwa imara katika wilaya ya mtwara kwa kubadilishana na
kuchangiana mawazo katika Nyanja mbalimbali za uimarishwaji chama kwa
kuwashirikisha vijana hasa katika manispaa ya mtwara mikindani kuliko na changamoto kubwa katika uongozi kwa upande wa vijana.
Naye mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm aliyeandamana na umoja huo Bwana SIKUNJEMA
YAHYA SHABAN amesemakuwa umoja huo umekuja mtwara kwa ajiri ya kuumarisha chama
kwa upande wa manispaa ya mtwara mikindani ambako kuliko jionesha kuwepo kwa
changamoto nyingi kwa chama hicho kwa vijana wengi kujiunga na vyama pinzani .
Hata hivyo mwenyekiti huyo alisema kuwa katika ziara hiyo ya ushirika
baina ya umoja wa vijana wa ccm mtwara na Temeke umedhamiria kufanya shughuli
mbalimbali za kijamii zikiwemo kufanya usafi katika makaburi msafa yaliyopo
katika manispaa ya mtwara mikindani na eneo tengefu la Stendi ya kisasa katika
mtaa wa mkanaredi ambayo hadi sasa haijaanza kutengenezwa na kupelekea kuwepo kwa vichaka ambavyo hutishia usala wananchi wa mtaa huo.Ameongeza kuwa baada ya
kufanya usafi katika maeneo hayao jioni wataenda kucheza mpira wa miguu katika
viwanja vya TTC KAWAIDA na mgeni atakuwa
mkuu wa wilaya Mtwara Bi Fatuma Alli.
Utaratibu wa kufanya usafi katika mji wa mtwara umeanza
tangu mwezi Desemaba mwaka jana na hii
ni mara baada ya uzinduzi uliofanywa na Rais wa jamhuri ya muunano wa Tanzania
Dk John Pombe Magufuli kwa kuagiza kila Halmashauri nchini kufanya usafi kwa
kila jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Comments
Post a Comment