Posts

Showing posts from 2016

Lugha za kimakabila zina athari kwenye elimu yetu!

NA RUSTON MSANGI.  Lugha ni mpangilio wa sauti na maneno unaoleta maana ambao hutumiwa na watu wa taifa fulani au kundi fulani kwa ajili ya kuwasiliana. Lugha inayotumiwa rasmi na watu wa taifa fulani huitwa lugha ya taifa na ile inayotumiwa kundi fulani la watu hasa makabila ni lugha za kimakabila.Kuna lugha huitwa lugha mama.Kila mtu mwenye uwezo wa kuzungumza ana lugha  mama. Lugha mama ni ile lugha ambayo mtoto anapozaliwa hukutana nayo na ndiyo lugha ya kwanza kujifunza kuzuizungumza kuitumia kuwasiliana.Pia,inajulikana kama lugha ya kwanza. Kwa mfano, mtoto akizaliwa leo  katika jamii ya watu wanaotumia kiswahili,akajifunza na  kuweza kukitumia kwa mawasiliano,basi hiyo ndiyo lugha yake ya mama. Au mtoto aliyezaliwa leo na kujifunza kuwasiliana kwa lugha ya  kisukuma,  akaweza,hiyo ndiyo lugha mama kwake.Watanzania wengi lugha zao mama ni zile za kimakabila. Katika mfumo wetu wa elimu nchini Tanzania tunazitambua lugha mbili.Kiswahili kinatumika kufundishia elimu

WOGA UNAVYOWATESA WALIMU!

Image
NA RUSTON MSANGI. Kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili sanifu toleo la pili, 2004, Woga ni hali ya kuwa na hofu ya kufikwa na jambo la kutisha au la taabu. Hali ya kutoweza kustahimili vitisho, hofu. Waajiriwa wote ulimwenguni wanapaswa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu. Wakiwa wanatimiza wajibu wao na kupata haki zao bila mateso na manyanyaso yoyote ndani na nje ya eneo la kazi. Nchini Tanzania hali iko tofauti sana kwa wafanyakazi wengi, hususani WALIMU, ambayo ni kada pekee yenye watumishi wengi nchini. Kwa muda mrefu sana walimu wamekuwa ni kundi pekee ambalo kila kiongozi wa nchi hii anaona ni sehemu ya kuchukulia umaarufu. Wakuu wa wilaya, wakurugenzi, viongozi wa kata, viongozi wa CCM nk,  Kwa muda mrefu kwa nyakati tofauti wamekuwa wakimtumia Mwalimu kama sehemu ya kujaribia utendaji wao. Manyanyaso, udhalilishaji na ukandamizwaji kwa Walimu sio kwamba walimu wanaupenda na kukubali, bali ni WOGA tu unawasumbua walimu wengi. Matukio mengi ya kud

Mwanafunzi Alivyochochea Hasira za walimu.

➡Siku ya walimu yaingia dosari. NA RUSTON MSANGI. Kulingana na maelezo ya Kamusi ya kiswahili sanifu, toleo la pili, 2004,dosari ni kasoro,walakini.Dosari ni hali ya kutokuwepi kwa ukamilifu wa kitu. Octoba 5 ya kila mwaka ni siku ya walimu duniani. Katika siku hii maalum, Walimu wote ulimwenguni kwa kushirikiana na mashairika pamoja na Wadau wa elimu huadhimisha na kusherekea siku hii kwa namna mbalimbali. Hufanyika matukio kama mikutano, vikao na shughuli nyingi ambapo walimu na Wadau hushiriki. Mafanikio na changamoto Katika kada ya ualimu na mchango wake katika elimu ya taifa fulani hujadiliwa na kuchambuliwa. Aidha,wakati wa siku hii,walimu na wadau wa elimu, hujikita katika mjadala wa  namna ya kutatua kero mbalimbali ili kuleta ufanisi kwenye elimu na taalauma ya ualimu. Walimu hubadilishana uzoefu. Nchini Tanzania, walimu wamekuwa mjadala.Mjadala juu ya walimu unatokana na tukio la kushambuliwa kikatili kwa mwanafunzi anayedaiwa kugoma na kupiga mwalimu wa m

Mwenge unavyoumiza walimu.

Image
    NA RUSTON MSANGI. Mwenge ni kitu mfano wa kikombe chenye mpini mrefu na utambi ambacho huwashwa na kukimbizwa katika kusherekea au kutukuza jambo fulani. (Kamusi ya kiswahili sanifu, toleo la pili 2004). Mwenge huweza kufananishwa na koroboi/kibatari lakini mwenge ni mkubwa kwa umbo. Nchini Tanzania tuna mwenge wa uhuru ambao azimio la kuuwasha lilitangazwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1959. Kwa mara ya kwanza ulipandishwa katika kilele cha mlima Kilimanjaro usiku wa Desemba 9, 1961. Hii ilikuwa ni siku ambayo Tanganyika ilipata uhuru wake kutoka kwa waingereza. Mwenge huu ukiwa ni ishara ya uhuru, upendo, utu na matumaini. Kila mwaka huwa kuna mbio za Mwenge, ambapo mwenge hutembezwa kila kona ya nchi, ukibeba ujumbe tofautitofauti wa kijamii, kisiasa na kiuchumi. Malengo na ujumbe wa Mwenge huwa mzuri, lakini shida ni katika utekelezaji wake na matumizi ya pesa. Inaelezwa kwamba Mwenge hauna bajeti maalumu inayopangwa bungeni, lakini ni mojawapo

Hitaji la walimu sio bati.

Image
NA RUSTON MSANGI. Kila chama cha wafanyakazi nchini kina jukumu la kusimamia, kulinda, kuboresha maslahi, na kuhakikisha haki za wanachama wake hazivunjwi, wala kukiukwa kwa namna yoyote ile. Majukumu hayo ya chama chochote cha wafanyakazi hayaepukiki kwa kuwa wanachama huwa na utaratibu maalumu wa kuchangia kwa njia ya ada. Michango hii kwa baadhi ya vyama huwa ya lazima hata kama haujajiunga wala kufahamu utaratibu wowote wa namna chama kinavyoendeshwa. Mfano mzuri ni Chama cha Walimu Tanzania CWT, walimu wengi hawajajiunga kwa kuridhia, bali kwa lazima na kuanza kukatwa pesa 2% ya mshahara mara moja. Mojawapo ya dhumuni muhimu la chama cha walimu Tanzania limeelezwa kwenye katiba ya CWT toleo la 2004, katika sehemu ya kwanza, 4 (s)Kuwekeza katika vitega uchumi vitakavyoboresha ustawi wa wanachama ingawa si Chama cha kibiashara. Kwa msingi huu wa kikatiba tungetegemea vitega uchumi vya CWT kunufaisha walimu na si viongozi pekee. Pamoja na makato hayo ya 2% ya mshah

Ufaulu hauji kwa kufanya kazi kama watumwa!

NA RUSTON MSANGI. Shughuli yoyote ile ya kimaendeleo inapofanyika, hutegemewa kuwa na matokeo chanya. Hadi kufikia matokeo yanayohitajika, njia za aina tofauti tofauti hutumiwa kufikia mafanikio. Ubora au ubaya wa njia itakayotumika inategemeana kwa kiasi kikubwa na uongozi wa wa shughuli au eneo husika. Vivyo hivyo katika mfumo mzima wa elimu nchini Tanzania, shuleni tunapopeleka vijana/wanafunzi wetu kupata maarifa tunatarajia wapate matokeo mazuri na kufaulu mitihani yao. Ili ufaulu unaotarajiwa uweze kupatikana kwa wanafunzi wetu, wasimamizi wa elimu na viongozi wa Shule wanategemewa kuwa na mbinu, maarifa, weledi na ushirikiano wa kutosha kutoka kwa walimu ambao ndiyo watekelezaji wakuu wa sera na mipango ya elimu. Hivyo kukiwa na mipango mizuri kwa ushirikiano, hata matokeo yatakuwa mazuri. Kutokana na umuhimu wa elimu nchini, nalazimika kuzungumzia ufaulu, namna ya kufanikisha na vikwazo vilivyopo kwa wasimamizi hasa mashuleni kama ambavyo kila kukicha yanajitokez

Posho hii ifike hadi kwa walimu

Image
NA RUSTON MSANGI. Kila mfanyakazi anapoajiriwa huwa kuna utaratibu maalumu wa malipo, yaani mshahara kwa mwezi au vyovyote vile kutokana na mkataba wa kazi. Mbali na malipo ya mshahara katika ajira, pia huwa kuna namna tofautitofauti ya kuwapatia fedha ya ziada wafanyakazi wa eneo au taasisi fulani ili kuongeza morali ya ufanyaji kazi, kupunguza makali ya maisha,  kufidia muda wa ziada katika kazi nk. Hii fedha hujulikana kama posho. Posho hii inaweza kutolewa kwa mwezi, siku, saa nk.  Posho huweza kuwa kwa ajili ya chakula, usafiri, malazi,   utendaji au namna yoyote ili itakavyokuwa imepangwa na mwajiri kwa makubaliano maalumu. Watumishi nchini Tanzania katika serikali na mashirika binafsi wanapokea posho kutokana na majukumu Yao. Kwa mfano, madaktari na polisi. Kwa upande wa walimu kwa muda mrefu imekuwa ni tofauti sana kuhusiana na suala la posho, japokuwa mwalimu mbali na jukumu kubwa na muhimu la kufundisha,  hufanya kazi nyingi nyingine akiwa kazini. Kilichon

Bodi ya mikopo kwa hili Hapana

NA RUSTON MSANGI. Mataifa mengi ulimwenguni yaliyoendelea na yanayoendelea, serikali zina  utaratibu maalumu wa kusaidia wanafunzi katika nchi zao kwenye masuala ya Elimu. Utaratibu huu hupelekea kuundwa kwa vyombo na taasisi mbalimbali zinazoshughulikia mikopo hasa ya Elimu ya juu. Vivyo hivyo nchini Tanzania tuna utaratibu wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu wenye sifa, sifa kuu ikiwa ufaulu na fani husika. Bodi ya mikopo nchini ilianzishwa kwa sheria ya Bunge namba 9, ya mwaka 2004 na Bodi ilianza rasmi mwezi julai, 2005. Moja ya Majukumu muhimu ya bodi ya mikopo yakiwa yafuatayo,- Mosi, Kusimamia mchakato wa Uombaji mikopo/kuwapata wanufaika stahiki wenye kukidhi vigezo baina ya waombaji. Mbili, utoaji wa mikopo. Tatu, Kukusanya mikopo iliyokopeshwa tangu mwaka 1994. Bodi ya mikopo pamoja na mapungufu makubwa iliyokuwa nayo na ambayo inayo,  imekuwa msaada mkubwa kwa familia masikini nchini. Wanufaika ni mashahidi wa hili. Taarifa ya habari ya Se

HUU NI UHAKIKI AU UDHALILISHAJI?

NA RUSTON MSANGI. Serikali ya awamu ya tano tangu iingie madarakani takribani mwaka mmoja uliopita, imekuwa ikiratibu na kutekeleza mengi nchini. Hivyo kuna mfululizo wa matukio mengi yaliyojitoleza. Matukio hayo yapo mazuri, mabaya na zaidi yapo yakushangaza na kustaajabisha machoni na masikioni mwa watanzania. Zoezi la uhakiki wa vyeti ni mojawapo ya mambo yaliyovaliwa njuga na serikali. Leo Naomba nizungumzie zoezi hili linaloendelea la kuhakiki vyeti vya watumishi walipo kazini. Nieleweke kuwa sipingi uhakiki wa vyeti nchini kwa namna mpya ambayo licha ya kushangaza wengi, lakini pia imewaacha wengi na maswali bila majibu. Nikiri kutoka moyoni zoezi la uhakiki likifuata kanuni, sheria, taratibu, utaalamu na ushirikishwaji wa taasisi tofautitofauti, Ni zoezi zuri kwa maslahi ya taifa, LAKINI kinyume na hapo inakuwa fujo na udhalilishaji. KAMA taifa nilitegemea tuwe na mfumo mmoja wa namna ya uhakiki, na pia sio dhambi kutofautiana kwa baadhi ya Halmashauri katika namna y

KUCHELEWA KWA AJIRA KUNAVYOUMIZA WALIMU

NA RUSTON MSANGI. Kada ya ualimu ndiyo yenye watumishi wengi nchini kuliko kada yoyote ile. Licha ya kada hii kuwa na watumishi wengi,takwimu zinaonesha bado kuna upungufu wa walimu nchini hasa walimu wa sayansi . Waziri mwenye dhamana ya  elimu,Profesa Joyce Ndalichako akijibu swali katika kikao cha bunge kilichopita, alibainisha upungufu wa walimu wa Sayansi 22,460. Miaka kadhaa iliyopita,watu wengi wamepata hamasa ya kusomea fani ya ualimu ili waajiriwe na serikali.Hakika walimu wamekuwa wakiajiriwa moja kwa moja katika shule katika shule za msingi na sekondari na vyuo . Walimu wamekuwa wakiajiriwa kwa vipindi tofauti mara wa wanapohitimu. Kwa mfano, walimu waliohitimu mwaka 2012 walipangiwa vituo vya kazi mwezi Februari 2013. Waliohitimu mwaka 2013 walipangiwa mwezi Machi 2014 na waliomaliza mwaka 2014 walipangiwa mwezi wa tano 2015. Lakini mamia ya walimu waliohitimu mwaka 2015 ,hawajaajiriwa,wanaendelea kusota mitaani.Kuchelewa sana kwa ajira za ualimu kumekithiri  kat

SERIKALI INGEANZA KWANZA NA WALIMU

NA RUSTON MSANGI. Taaluma  ya ualimu ni mama na mhimili wa taaluma zote duniani. Hakuna Taaluma au fani isiyotokana na ualimu. Ualimu ndio unaojenga daraja la uhusiano baina ya taaluma zote duniani.Kwamba watu waliopata taaluma au kusomea fani mbalimbali duniani walipikwa na kuivishwa kwenye chungu cha ualimu.  Ualimu ndio unaotengeneza ,wanasheria, wahandisi, wahasibu na hata mwandishi wa habari, wanasiasa. Dhima ya ualimu ni kutoa au kufundisha   maarifa, ujuzi na hekima. Ualimu ni mchakato wa kufundisha maarifa, ujuzi au hekima kutoka kwa mtu moja kwenda kwa mwingine. Mtoaji maarifa au hekima anaitwa mwalimu na mpokeaji ni mwanafunzi. Wanafalsafa wa kale walifanya kazi ya ualimu kwa vitendo na walifanikiwa kuzalisha kizazi chenye hekima, maarifa na ujuzi tele. Waliacha urithi usiochakaa wala kuharibika vizazi na vizazi. Mwanafalsafa Socrates aliyeishi Ugiriki ya kale kati mwaka 469-399 Kabla ya Kristo(B.K) aliishi kwa kutafakari ,kuhoji na kutafuta na kufundisha hekim

MAWAZIRI WA ELIMU WANAVYOKOROGA KWA ZAMU.

➡sasa ni zamu ya Profesa Ndalichako. Anaandika Ruston Msangi. Kila mwanadamu huzaliwa huru. Anapozaliwa haijulikani mara moja atakuja kuwa nani au mwenye taaluma/ fani gani. Lakini kutokana na malezi ya wazazi, mazingira, na jamii inayomzunguka mtoto huanza kutamani kuwa mtu flani hapo baadae. Kutoka ngazi ya jamii, ndoto za mtoto huamia shuleni ambapo ndipo hasa eneo la muhimu katika kujenga misingi ya daktari, Mwalimu, mwanasheria, Mhasibu, Askari, mwanajeshi, mwanahabari nk. wa kizazi kijacho. Uwezo wa mtoto kimasomo Kulingana na fani itakayo hujulikana akiwa shule. Kila mtoto anakuwa na uwezo kwenye eneo Lake Kulingana na kipaji chake. Hivi vyote vinatokana na misingi ya Taifa, sera, mikakati, mipango ya muda mrefu na mazingira rafiki yenye mahitaji yote muhimu ya kujifunzia ndivyo ambavyo humuwezesha mwanafuzi kutimiza ndoto yake. Ndoto ya mwanafunzi ikitimia basi na ndoto ya Taifa itakuwa imetimia kwa kupata wataalamu viwandani na maeneo yote muhimu. Hivi ndivyo amb

SERIKALI INAVYOZIKA NDOTO ZA KUPATA ELIMU BORA

Na Ruston Msangi. Elimu ni muhimu na nguzo kwa watu na taifa lolote duniani. Siri ya mataifa mengi yaliyoendelea kama Marekani, Uingereza, Urusi, Japan,  China, Ufaransa, Ujerumani na mengineyo,Ni elimu bora. Maendeleo ya mataifa hayo yanatokana na kuwekeza katika elimu bora ambayo baadae imewaletea wataalamu wengi,  teknolojia na maendeleo kwa ujumla. Utambulisho mojawapo wa nchi maskini,zinazoendelea kama vile Tanzania, ni elimu duni. Wakati rekodi zinaonesha elimu ndio mhimili wa Maendeleo duniani, Tanzania na nchi nyingine maskini zinaelezwa kuzika elimu kaburini. Mikakati, mipango na utekelezaji wake, vimekuwa vikisusua sana. Inarudisha nyuma ubora wa elimu. Kwa mfano nchini Tanzania kumekuwa na mipango mingi ya kuboresha elimu, japo mipango mingi imeonekana kushindwa. Leo tuangalie MABADILIKO MAKUBWA YA MFUMO WA MTIHANI WA KIDATO CHA PILI. Hivi karibuni Wakuu wa shule mbalimbali nchini wamepokea waraka kutoka kwa Katibu tawala wa mkoa kupitia kwa wakurugenzi

UZALENDO WA KWELI HAUNA MIPAKA.

Image
. Na, Emmanuel Chengula, Uzalendo ni hali ya kupenda, kuamini, ama pengne kukihusudu kitu fulani kutoka moyoni bila kuwa na mazingira ya kukulazimisha kufanya hivyo. Uzalendo ni zaidi ya love affection, ni zaidi ya mashart ni zaidi ya shinikizo na una kawaida ya kutenda haki na pengine kutoa uhai wa watu au mtu ili kitu hicho kisalimike. Duniani kote kuna mgawanyiko wa watu wenye baadhi ya dondoo za uzalendo lakini sio wazalendo kama lilivo neno lenyewe lakin pia wachache walihesabika ni wazalendo kama mwl nyerere, Nkwame nkrumah, steve bikko, Nelson Mandela, Marcus Gurvey, Martin Luther Jr, Indra Gandhi n.k. Kwa kawaida uzalendo wa kweli ni ule unaoangalia nchi kwa ujumla pamoja na watu wake japo kuwa kuna watu ambao wameugawa uzalendo na kuegemea kwenye chombo ama kitu kimoja; mfano kuna wazalendo wa vyama vya siasa, dini, serikali tu, bunge tu, mahakama tu, haki za wanyonge tu matajiri hana uzalendo nao, matajiri tu maskini hataki hata kuwasikia, wenye ufahamu mzuri tu,

MASOKO YA MTWARA MIKINDANI YAKABILIWA NA TATIZO LA VYOO

Baadhi ya wafanyabiashara katika soko la kijiji cha mkunjanguo katika kata ya Naliendele mkoani Mtwara wamelalamikia ukosefu wa huduma muhimu ikiwemo choo katika soko hilo. Wakizungumza  sokoni hapo na mwandishi wa habari hii baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema kuwa  changamoto hiyo imekuwepo sokoni hapo kwa muda mrefu jambo ambalo limekuwa likiwapa usumbufu mkubwa na kuwaweka katika hatari ya magonjwa ya milipuko katika eneo hilo. Uongozi wa eneo hilo akiwemo mwenyekiti wa kijiji hicho wamekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kudai kuwa eneo hilo halikidhi vigezo vya kuwa soko na kuwa na kuwa awali mzabuni ambaye alipewa dhamana ya soko hilo alishindwa kujenga vyoo sokoni hapo.  Hata hivyo ameongeza kuwa jitihada zinaendelea kuhakikisha soko hilo linapata vyoo na kuwa wataanzisha utaratibu mpya wa kutoza ili kuwezesha kujenga vyoo hivyo. Aidha masoko mengi katika manispaa ya Mtwara mikindani  yanakabiliwa na uhaba wa vyoo bora jambo ambalo linatishia afya za wafanya

CHAMA CHA USHIRIKA MKOANI MTWARA CHAWATAKA WAFANYA BIASHARA WA MAZAO KUFUATA MISINGI NA TARATIBU ZA KIBIASHARA

Chama cha ushirika wa wakulima mkoani Mtwara kimewataka wanunuzi wa mazao mbalimbali kuacha kutumia mizani kwa kuwa ni kosa kisheria na ni unyonyaji kwa wakulima. Wito huo umetolewa na Kamimu Mkurugenzi wa chama hicho mkoani hapa Bw. Laurence Njozi ambapo amesema kuwa chama hicho hakitasita kuwachukulia hatua wale wote watakaobanika kufanya manunuzi kwa njia hiyo isiyo halali. Amesema kuwa ili kuepukana na tatizo hilo pia ni vema kwa wakulima kuwa na subira ya kuuza mazao yao ghalani na kuachana na utaratibu wa kuuza reja reja kwa kuwa unawaumiza. Ameongeza kuwa chama hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya wakulima kukosa uvumilivu kwa kucheleweshewa malipo yao pamoja na wanunuzi hao wadogo ambao hununua kinyume cha sheria. Aidha serikali imepiga marufuku uuzaji wa mazao kwa kutumia mizani kwa wanunuzi wa reja reja na kujaza rumbesa kwa kuwa inawanyonya wakulima.

MAKAMU MWENYEKITI BAVICHA BARA MH PATRICK OLE SOSOPI AKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI IRINGA

Image
Tayari Jeshi la  Polisi limemkamata Makamu M/kiti wa BAVICHA muda huu hapa Iringa Mjini baada tu ya kumaliza Mahafali ya CHASO. Kosa ni la uchochezi wa Kisiasa ambalo alilitenda akiwa DSM katika Mahafali ya CHASO ya tarehe 18/06/2016. Hivyo atasafirishwa kutoka Iringa kwenda DSM kwaajili ya mahojiano na baadae Mahakamani. Imetolewa June 26 Edward Simbeye Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa