MASOKO YA MTWARA MIKINDANI YAKABILIWA NA TATIZO LA VYOO
Baadhi ya wafanyabiashara katika soko la kijiji cha
mkunjanguo katika kata ya Naliendele mkoani Mtwara wamelalamikia ukosefu wa
huduma muhimu ikiwemo choo katika soko hilo.
Wakizungumza sokoni
hapo na mwandishi wa habari hii baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema
kuwa changamoto hiyo imekuwepo sokoni
hapo kwa muda mrefu jambo ambalo limekuwa likiwapa usumbufu mkubwa na kuwaweka
katika hatari ya magonjwa ya milipuko katika eneo hilo.
Uongozi wa eneo hilo akiwemo mwenyekiti wa kijiji
hicho wamekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kudai kuwa eneo hilo halikidhi
vigezo vya kuwa soko na kuwa na kuwa awali mzabuni ambaye alipewa dhamana ya
soko hilo alishindwa kujenga vyoo sokoni hapo.
Aidha masoko mengi katika manispaa ya Mtwara
mikindani yanakabiliwa na uhaba wa vyoo bora
jambo ambalo linatishia afya za wafanyabiashara na wateja wanaofuata huduma
maeneo hayo.
Comments
Post a Comment