TAKRIBANI MITI 50 YAPANDWA MKOANI MTWARA
Serikali mkoani Mtwara imepanda jumla ya miti 50 kutoka bodi ya Korosho hadi viwanja vya Mashujaa vilivyopo mtwara manispaa ili kuboresha,kupendezesha na kulinda hifadhi ya barabara .
Akizindua upandaji huo mkuu wa wilaya Mtwara Bi Fatuma Alli amesema kuwa tukio hilo lililofanywa na ofisi ya Tanroad Mtwara ni jambo la kuigwa na kuwataka wananchi kuhifadhi mazingira kwa kufanya usafi,kupangilia ujenzi wa makazi na kupanda miti katika maeneo tunayoishi.
Pia mkuu wa wilaya mtwara amewataka wananchi kushirikiana na Tanroad kwa kuwa makini na wale wanaovamia hifadhi ya barabara kwa kujenga na kuweka mabango pasipo fuata taratibu za kuhifadhi wa barabara kwani kama wanauhitaji wa kuweka mabango wafuate taratibu husika ili wasijikute wanaingia katika mikono ya kisheria kupitia ofisi husika.
Naye mhandisi kutoka Tanroad Bw Edward kokina amesema kuwa hii ni katika kuunga mkono siku ya mazingira iliyo azimishwa tareh 6/6/2016 na kuamua kupanda miti ikiwa na lengo kuwasaidia wananchi kwa kupata kivuli na kupendezesha mji wa mtwara ambao upo katika mchakato wa kuwa jiji.
Katika upandaji huo ulihusha pia wanafunzi wa shule ya sekondari ya kiislamu AL-SAFAH inayopatika manispaa ya mtwara mikindani ambao nao kwa pamoja walisema miti ni uhai na wao kama wanafuzi hawana budi kushiriki katika zoezi hilo ili kuunga mkono jitihada za serikali za kupitia Tanroad mkoa.
Naye Bi Salma kayaga ambaye pia ni Mwalimu wa shule hiyo amewapongeza tanroad kwa kitendo cha kupanda miti na kushauri wananchi kuwa na utaratibu wa huo ili kuweka mji wa mtwara katika hali ya usafi na ya kuvutia.
Manispaa ya mtwara mikindani ni moja kati ya manispaaTanzania zilizopo katika mchakato wa kupandishwa hadhi na kutoka katika manispaa na kuwa hadhi ya mji, na hili limetokana na maombi yaliyokubaliwa na baraza la madiwa kupeleka maombi Tamisemi kwa ajiri ya kuwa katika hadhi hiyo.
Comments
Post a Comment