CHAMA CHA USHIRIKA MKOANI MTWARA CHAWATAKA WAFANYA BIASHARA WA MAZAO KUFUATA MISINGI NA TARATIBU ZA KIBIASHARA

Chama cha ushirika wa wakulima mkoani Mtwara kimewataka wanunuzi wa mazao mbalimbali kuacha kutumia mizani kwa kuwa ni kosa kisheria na ni unyonyaji kwa wakulima.

Wito huo umetolewa na Kamimu Mkurugenzi wa chama hicho mkoani hapa Bw. Laurence Njozi ambapo amesema kuwa chama hicho hakitasita kuwachukulia hatua wale wote watakaobanika kufanya manunuzi kwa njia hiyo isiyo halali.

Amesema kuwa ili kuepukana na tatizo hilo pia ni vema kwa wakulima kuwa na subira ya kuuza mazao yao ghalani na kuachana na utaratibu wa kuuza reja reja kwa kuwa unawaumiza.

Ameongeza kuwa chama hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya wakulima kukosa uvumilivu kwa kucheleweshewa malipo yao pamoja na wanunuzi hao wadogo ambao hununua kinyume cha sheria.

Aidha serikali imepiga marufuku uuzaji wa mazao kwa kutumia mizani kwa wanunuzi wa reja reja na kujaza rumbesa kwa kuwa inawanyonya wakulima.


Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI