Posts

Showing posts from 2018

Walimu tujitafakari katika utoaji wa adhabu, hatma yetu iko mikononi mwetu

Image
NA RUSTON MSANGI. Kuna msemo unasema  kinga ni bora kuliko tiba, yaani ni bora uwe na tahadhari ya kukabiliana au kujihami na jambo lolote na si kusubiria hadi tatizo lijitokeze. Siku za hivi karibuni kumejitokeza matukio makubwa mawili nchini yanayohusisha walimu na wanafunzi. Tukio la kwanza ni la Agosti 27, 2018 ambapo mwalimu Respicius Patrick na mwenzake Herieth Gerald wa shule ya msingi Kibeta mkoani Kagera, wanatuhumiwa kwa kumuadhibu hadi kumsababishia kifo mwanafunzi wao Sperius Eradius wa darasa la tano. Chanzo cha tukio hili inasemekana ni mwanafunzi huyo kuhusishwa na wizi wa pochi ya mwalimu. Na hadi sasa walimu hawa wamesomewa mashtaka ya kuua kwa kukusudia katika kesi ya mauaji namba 18 ya mwaka 2018. Tukio lingine ni lile la mwalimu wa sekondari ya Kalangalala mkoani Geita aliyejulikana kwa jina la Rauson Lechapia anatuhumiwa kumshambulia kwa ngumi mwanafunzi wa kidato cha sita Jonathan Mkono hadi kupelekea kulazwa hospitali kutokana na maumivu makali. Kosa

Uchambuzi wa kifasihi katika wimbo wa Roma na Stamina uitwao Parapanda!

Image
NA RUSTON MSANGI. Fasihi ni sanaa itumiayo lugha kufikisha ujumbe kwa hadhira/jamii iliyokusudiwa. Nyimbo ni aina ya sanaa katika fasihi ambayo hutumia lugha teule, sauti na kiimbo maalum. Nyimbo huburudisha, kuelimisha, kusifia, kuliwaza nk. Hivi karibuni msanii Roma kwa mara nyingine, na kwasasa akiwa na mwenzake Stamina wamekonga nyoyo za mashabiki wa muziki na fasihi kwa ujumla kutokana na wimbo wao maarufu wa Parapanda. Wafuatiliaji wa mashairi ya Roma kwa muda mrefu, watakubaliana nami kwamba Roma amepiga hatua kubwa sana hasa katika matumizi ya fasihi. Katika wimbo huo wasanii Roma na Stamina wamekuja na aina tofauti kabisa. Wasanii hawa wamevaa uhusika wa watu wawili maarufu kwenye historia ya taifa letu, ambao kwa sasa hatuko nao hapa duniani. Yaani Baba wa taifa Mwal. Julius Kambarage Nyerere na Kingunge Ngombare Mwiru. Roma akiwa ni Nyerere na Stamina akivaa uhusika wa mzee Kingunge. Wasanii hawa wamefanya hivi kuvuta taswira juu ya mtazamo wa watu maarufu na

Wakuu wa shule wapata nafasi ya kukomoa walimu.

Image
NA RUSTON MSANGI. Ni wiki kadhaa sasa walimu wengi nchini wamekuwa katika msongo wa mawazo, hii ni kutokana na agizo la serikali linalotaka walimu wa sekondari wa stashahada na shahada wanaosemekana ni wa ziada kwa masomo ya sanaa wapelekwe shule za msingi. Mapema sana nilionesha kutokukubaliana na agizo hili kwa kuwa ni kimyume na mkataba, humuathiri mwalimu kisaikolojia, humshusha mwalimu cheo, hunyima wahusika ajira, nk. Katika utekelezaji wa agizo hili ambalo limepingwa na walimu wengi wenye akili, kumezuka matatizo makubwa zaidi. Baadhi ya wakuu wa shule za sekondari nchini wamepata nafasi ya kuonyesha chuki za wazi kabisa kwa walimu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa namna moja au nyingine wakuu wa shule wamehusika moja kwa moja katika zoezi la kuhamisha walimu kutoka sekondari kwenda shule za msingi. Na ushiriki wa wakuu wa shule haujawa wa heri wala haki, bali imekuwa ni nafasi kwao kuadhibu, kukomoa na kuondoa watu ambao wanahisi ni kero kwao. Nayasema hay

Adui mkubwa wa walimu ni CWT.

Image
NA RUSTON MSANGI. Adui ni kiumbe au mtu anayemtendea mwingine uovu, kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili sanifu. Uovu unaweza kuwa wa moja kwa moja au hata kwa njia ya kutotimiza majukumu vizuri. Chama cha walimu Tanzania CWT,  ni miongoni mwa vyama vya wafanyakazi nchini, kinachoshughulika na walimu. Kwa mujibu wa katiba ya CWT, pamoja na madhumuni mengi ya chama hiki, jukumu kubwa na la pekee ni kusimamia hadhi, haki na maslahi ya walimu kitaaluma, kiuchumi, kijamii nk. Ni ukweli usiopingika kwamba ni vigumu kwa mwalimu mmojammoja kujitetea lakini kupitia umoja au taasisi ya CWT inakuwa rahisi zaidi. Kauli mbiu ya CWT ni HAKI na WAJIBU. Kwa miaka mingi kinachoangaliwa ni WAJIBU huku HAKI ikiwa imezikwa na kuachiwa kila mmoja kujitetea. CWT inaendeshwa kwa pesa za wanachama wake ambao ni walimu, kwa makato ya 2% ya mshahara kila mwisho wa mwezi. Hivyo kama ni rasilimali fedha ipo ya kutosha kufanya kazi kwa maslahi ya walimu. Nitakupa mfano kiduchu wa mapato ya CWT:

Mohamed Hamisi ni mlemavu mwenye malengo makubwa na yenye tija

Image
Pichan:Mlemavu anayependa kujishughulisha Pichan:Mh Ally Bananga Diwani wa kata ya Sombetini kupitia Chadema akiwa na Mohamed Hamisi ambaye ni mlemavu mwenye nia ya kujishughulisha badala ya kuishi kama omba omba wakijadili maswala mbalimbali ya kimaendeleo Mohamed Hamisi ni mkazi wa Sombetini. Ana umri wa miaka 24. Ni mtoto wa marehemu Hamisi Faustine. Ni mlemavu wa miguu na mkono mmoja pia una shida. Hapendi kuomba, anapenda kujishughulisha. Kwa sasa anafanya vikazi vidogo vidogo vya kuweka tinted kwenye magari lakini anakabiliwa na changamoto kadhaa.   Anatamani  kuwa na biashara nyingine ndogo ili aweze kuongeza kipato kuwasaidia wadogo zake watano ambapo mdogo kabisa ana miaka minne.    Anaomba msaada afungue ofisi yake ili achanganye kazi zake ya kuweka tinted (maana sasa anafanya kwa mtu) na pia ofisi hiyo ataweza kuongeza biashara nyingine ya kuuza na kuburn VCD, kuuza mitumba vocha na kadhalika. Pia baiskeli yake ni nzito, ni ya mbao na chuma hasa ukizingatia anatu

RICHARD TAMBWE HIZA KUZIKWA LEO

Image
Pichani:Ratiba ya mazishi ya Mh Richard Tambwe Hiza aliyefariki ghafla juzi asubuhi kwa tatizo la Pumu lilokuwa likimsumbua kwa Mda mrefu.

Pata vichwa vya habari katika magazeti ya leo

Image

BREAKING NEWS:MH SUGU NA MASONGA WAACHIWA HURU KWA DHAMANA

MH. SUGU NA MSONGA  WAACHIWA HURU KWA DHAMANA MUDA HUU SAA 19: 03 USIKU KATIKA MAHAKAMA YA MKOA WA MBEYA BAADA YA KESI YAO KUSIKILIZWA KWA SIKU NBILI MFULULIZO . HUKUMU ITATOLEWA TAR 26/02/2018. Leonce Marto  Mwenyekiti Bavicha Iringa mjini amethibitisha akiwa katika mahojiano mwandishi wetu Leonce Marto ametoa Shukrani za dhati kwa Wakili Kibatala na wenzake pamoja na wananchi wote wa jiji la  Mbeya

CHADEMA YAENDELEA KUCHANJA MBUGA KINONDONI HUKU MAELFU YA WANANCHI WAKIWAUNGA MKONO

Image
Pichani:Wananchi wa kata ya Magomeni waliojitokeza kwa wingi kuwasikiliza viongozi na Mgombea wa Chadema Pichan:Wanachi wa kata ya magomeni wakiwa na nyuso za furaha wakati wakisikiliza sera za mgombea wa chadema  kata ya magomeni Pichani:Mgombea wa Chadema Salum Mwalimu  akiomba kura kwa wananchi wa Kata ya Magomeni waliofurika kumsikiliza Pichani:Mh Boniface Jacob ,Mstahiki Meya wa Ubungo akimnadi Mgombea wa Chadema Ndg Salumu Mwalimu, katika  Mkutano wa Kampeni za CHADEMA uliofanyika leo Kata ya Magomeni jijini Dar Es Salaam ambapo Meya wa Ubungo Boniface Jacob alikuwa Mgeni rasmi wa Mkutano huu.

BREAKING NEWS: WAKILI ANAYEMTETEA SUGU NA MASONGA ACHARUKA

Image
Pichani:Wakili Peter Kibatala Mabishano makali ya kisheria yasababisha kesi kuiarishwa kwa mda........ Wakili Kibatala amecharuka na kutaka aombwe radhi na wakili wa Serikali Joseph Pandu baada ya kumuita yeye ni mwanasiasa na  anaendesha hiyo kesi kisiasa. " Wewe ni mwanasiasa na una uanachama wa CHADEMA ......"Acha kuendesha hii kesi kisiasa na endapo nitatakiwa na Mahakama hii kuthibitisha uanachama wako nitafanya hivyo ndani ya miezi miwili".... Joseph Pandu. Kesi itarejea baadaye , Hakimu amewaita mawakili wote kwenda ofisini kwake kuweka mambo sawa ......

MASAA SABA YA MH.SUGU (MBUNGE) uuNA MASONGA MAHAKANI

Image
Kesi ya Mh , Sugu na Masonga imenguruma leo kwa saa saba , kuanzia saa 5:00 asubuhi mpaka saa 12 : 08 Jioni. Kesi itaendelea kesho saa 3 :00 asubuhi kwa RCO na RPC  wa Mkoa wa Mbeya kuja kutoa ushahidi wao. Sugu na Masonga wamerudi gerezani mpaka kesho. Mwenyekiti Bavicha manispaa ya Iringa mjini Alonga na mwandishi wetu kutoka nyanda za juu kusini.

TANZIA:MH TAMBWE HIZA, KIONGOZI NA KADA MAARUFU WA CHADEMA AFARIKI DUNIA ASUBUHI YA LEO

Image
Mwanasiasa maarufu na wa siku nyingi Tambwe Hizza amefariki leo alfajiri nyumbani kwake jijini Dar es salaam.Marehemu Tambwe Hizza amefariki akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa pumu na amefariki akiwa ni mmoja wa waratibu wa kampeni za chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) katika jimbo la Kinondoni:Taarifa hizi zimethibitishwa na Mstahiki Meya wa Ubungo@Boniface Jacob Na mmoja wa wanafamilia

Serikali yawaweka walimu mtegoni.

Image
NA RUSTON MSANGI. Ualimu ni kada pekee nchini yenye watumishi wengi kuliko kada nyinginezo. Waswahili husema penye wengi kuna mengi pia. Ni ukweli usiopinginga kwamba kila kada ina changamoto zake, lakini ualimu umekuwa na zaidi ya changamoto, ni matatizo. Tumeshuhudia mara nyingi sana walimu nchini wakinyanyaswa kwa kupigwa, kunyimwa haki zao za msingi zilizipo kisheria, kufedheheshwa, na kudhalilishwa kwa kudekishwa na watendaji wa serikali. Mara kadhaa pia wazazi na wanafunzi wamekuwa watu wasiojali walimu. Wakati haya yanafanyika kuna mwalimu mmoja aliwahi kutamka, nanukuu ''Hata nikipigwa ilimradi mshahara unaingia'' mwisho wa kunukuu. Kwa kauli hii inadhihirisha wazi hata walimu wenyewe hawathamini utu wao, na kazi wanazofanya wanaona ni hisani na huruma ya serikali na si haki zao. Serikali inayokata kodi ya mwalimu 11% hadi 12% na bodi ya mkopo 15% katika mshahara kiduchu wala haimjali mwalimu. Chama cha walimu CWT kinachokata 2% ya mshahara wa m