Posts

Showing posts from 2021

𝐊𝐈𝐓𝐔 𝐆𝐀𝐍𝐈 𝐊𝐈𝐍𝐀𝐓𝐎𝐊𝐄𝐀 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐓𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐅𝐀

Image
Na Dr Elimina Chuma Leo nita-share stori moja iliyotokea kipindi naanza kazi takribani miaka nane iliyopita. Palikuwa na mama mmoja aliyekuwa na miaka 90 na alikuwa amelazwa kwa sababu ya moyo wake kushindwa kufanya kazi vizuri.  Tatizo hilo lililotokana na kuwa na shinikizo la juu la damu kwa miaka mingi. Wakati analetwa alikuwa amevimba miguu na alikuwa analala akiwa amekaa. Siku za mwanzoni alikuwa kwenye oksijeni lakini baadae alitolewa baada ya kupata nafuu; kila saa alikuwa anasema, “jamani nimechoka mwenzenu, nitakuja hospitali hadi lini?” Ilipita kama wiki mbili hivi yule mama akiwa bado wodini, nakumbuka ilikuwa jumanne na nilikuwa zamu siku hiyo. Nilipita round wodini pamoja na daktari mkuu wa  hospitali ile. Yule mama alikuwa amepata nafuu sana, miguu ilikuwa imenywea, alikuwa anapumua kawaida na kila kitu chake kilikuwa kawaida. Tulipanga kumruhusu kwenda nyumbani kesho yake. Baada ya kuwaona wagonjwa wa wodini nilielekea kliniki kuona wagonjwa wa nje. Nikiwa kliniki, muda

MOYO KUSHINDWA KUFANYA KAZI

Image
 Na Dr Elimina Chuma ,MD Pichani: Inaonesha jinsi  Moyo unavyofanya kazi na mgawanyo wa mishipa ya damu. Utangulizi Umewahi kuona mtu anayejisikia kuchoka sana huku amevimba tumbo na miguu, anapata tabu kufanya shughuli za kawaida mf. Kuinuka na akilala chali anaishiwa pumzi? Inawezekana moyo wake ulikuwa umeshindwa kufanya kazi kwa jinsi inavyotakiwa. Mara nyingi moyo ukishindwa kufanya kazi utahitaji matibabu kwa maisha yote ili uweze kuishi kawaida.  Kitu gani husababisha moyo kushindwa kufanya kazi? 1. Magonjwa ya mishipa ya damu ya moyo; 2. Shinikizo la juu la damu; 3. Magonjwa ya valvu za moyo; 4. Magonjwa ya misuli ya moyo; 5. Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo mf. Matundu kwenye moyo; 6. Mapigo ya moyo yasiyo na mpangilio na 7. Magonjwa mengine sugu mf. UKIMWI na Kisukari. Unaweza kuona dalili zifuatazo kama moyo wako umeshindwa kufanya kazi: 1. Kuishiwa pumzi unapojaribu kutembea/kusimama; 2. Kushindwa kupumua ukiwa umelala; 3. Kuishiwa nguvu na kusikia kuchoka sana; 4. Kuvimb

𝐅𝐀𝐈𝐃𝐀 𝟓 𝐀𝐌𝐁𝐀𝐙𝐎 𝐔𝐁𝐎𝐍𝐆𝐎 𝐖𝐀𝐊𝐎 𝐔𝐍𝐀𝐏𝐀𝐓𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐙𝐎𝐄𝐙𝐈

Image
Na Dr.Elimina Chuma,MD Unapofanya mazoezi kuna kemikali na homoni mbalimbali zinazotengenezwa ambazo zina faida kubwa kwa ubongo na afya ya akili. 𝐊𝐢𝐥𝐚 𝐦𝐨𝐣𝐚 𝐲𝐚 𝐤𝐞𝐦𝐢𝐤𝐚𝐥𝐢/𝐡𝐨𝐦𝐨𝐧𝐢 𝐡𝐢𝐳𝐨 𝐢𝐧𝐚 𝐟𝐚𝐢𝐝𝐚 𝐳𝐚𝐤𝐞 𝐤𝐚𝐦𝐚 𝐢𝐟𝐮𝐚𝐭𝐚𝐯𝐲𝐨: 1. Endofini- hupunguza maumivu; 2. Serotonini- hukusaidia kujisikia vizuri kwa ujumla; 3. Dopamini- hukuchangamsha, zinakupa motisha, umakini na zinakusaidia kujifunza; 4. Norepinefrini- huongeza umakini, mtazamo na hukupa motisha na 5. Zipo homoni zingine ambazo zinasaidia kukarabati mishipa ya fahamu, kuunganisha seli mbalimbali za ubongo na kusaidia akili kufunguka zaidi. Taja faida zingine za mazoezi. #exercise #fitness #workout #gym #motivation #health #fit #training #fitnessmotivation #healthy #healthylifestyle