MOYO KUSHINDWA KUFANYA KAZI
Na Dr Elimina Chuma ,MD
Pichani: Inaonesha jinsi Moyo unavyofanya kazi na mgawanyo wa mishipa ya damu.
Utangulizi
Umewahi kuona mtu anayejisikia kuchoka sana huku amevimba tumbo na miguu, anapata tabu kufanya shughuli za kawaida mf. Kuinuka na akilala chali anaishiwa pumzi? Inawezekana moyo wake ulikuwa umeshindwa kufanya kazi kwa jinsi inavyotakiwa. Mara nyingi moyo ukishindwa kufanya kazi utahitaji matibabu kwa maisha yote ili uweze kuishi kawaida.
Kitu gani husababisha moyo kushindwa kufanya kazi?
1. Magonjwa ya mishipa ya damu ya moyo;
2. Shinikizo la juu la damu;
3. Magonjwa ya valvu za moyo;
4. Magonjwa ya misuli ya moyo;
5. Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo mf. Matundu kwenye moyo;
6. Mapigo ya moyo yasiyo na mpangilio na
7. Magonjwa mengine sugu mf. UKIMWI na Kisukari.
Unaweza kuona dalili zifuatazo kama moyo wako umeshindwa kufanya kazi:
1. Kuishiwa pumzi unapojaribu kutembea/kusimama;
2. Kushindwa kupumua ukiwa umelala;
3. Kuishiwa nguvu na kusikia kuchoka sana;
4. Kuvimba miguu. Ukiiminya inaacha kishimo#Swipe picha kuona;
5. Kuvimba tumbo
6. Kuusikia moyo wako ukienda kasi;
7. Kikohozi kisichoisha na
8. Kuongezeka uzito kwa sababu ya mwili kujaa maji.
NB: Dalili hizi zinaweza kujitokeza kwenye magonjwa mengine pia hivyo ni muhimu sana kuonana na daktari mapema ili kupata suluhisho.
Picha 2 :Kuvimba tumbo ni dalili moja wapo ya tatizo la moyo kushindwa kufanya kazi vizuri
Pichani :Kuvimba miguu ni dalili moja wapo ya tatizo la moyo kushindwa kufanya kazi vizuri
Matibabu
1. Dawa za makundi mbalimbali za kusaidia moyo mf. Captopril, Losartan, Atenolol, Lasix, Digoxin na Aldactone. Aina ya dawa itategemea dalili ulizonazo na mara nyingi utakuwa na dawa zaidi ya moja;
2. Upasuaji wa moyo au
3. Kuwekewa moyo wa mtu mwingine.
Vitu vinavyoweza kukuweka kwenye hatari ya moyo kufeli
1. Shinikizo la juu la damu;
2. Magonjwa ya mishipa ya damu ya kwenye moyo;
3. Kisukari;
4. Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo;
5. Matumizi ya pombe kupita kiasi na
6. Uvutaji sigara;
Fanya haya kulinda moyo wako
1. Usivute sigara;
2. Punguza kiasi cha pombe, mwanamke< kipimo 1 na mwanaume <vipimo 2 kwa siku;
3. Kunywa dawa za shinikizo la damu na kisukari kama ulivyoelekezwa;
4. Fanya mazoezi, dk 150-300 kwa mazoezi mepesi, dk 75-150 kwa mazoezi magumu, kwa wiki;
5. Ongeza mboga za majani na matunda kwenye milo yako #Fuatisha sahani ya mlo unaofaa na
6. Kabili msongo wa mawazo kwa kupumzika, kufanya shughuli unazopenda au kuonana na mwanasaikolojia katika hospitali za Wilaya na Mikoa.
Uliza maswali yako kwenye comments.
#HeartFailure#Heart #HeartDisease #HeartHealth #Medicine #Diabetes#Cardiovascular #HeartTransplant #CardiovascularDisease #HeartDiseaseAwareness #Hypertension
Comments
Post a Comment