Posts

Showing posts from August, 2018

Uchambuzi wa kifasihi katika wimbo wa Roma na Stamina uitwao Parapanda!

Image
NA RUSTON MSANGI. Fasihi ni sanaa itumiayo lugha kufikisha ujumbe kwa hadhira/jamii iliyokusudiwa. Nyimbo ni aina ya sanaa katika fasihi ambayo hutumia lugha teule, sauti na kiimbo maalum. Nyimbo huburudisha, kuelimisha, kusifia, kuliwaza nk. Hivi karibuni msanii Roma kwa mara nyingine, na kwasasa akiwa na mwenzake Stamina wamekonga nyoyo za mashabiki wa muziki na fasihi kwa ujumla kutokana na wimbo wao maarufu wa Parapanda. Wafuatiliaji wa mashairi ya Roma kwa muda mrefu, watakubaliana nami kwamba Roma amepiga hatua kubwa sana hasa katika matumizi ya fasihi. Katika wimbo huo wasanii Roma na Stamina wamekuja na aina tofauti kabisa. Wasanii hawa wamevaa uhusika wa watu wawili maarufu kwenye historia ya taifa letu, ambao kwa sasa hatuko nao hapa duniani. Yaani Baba wa taifa Mwal. Julius Kambarage Nyerere na Kingunge Ngombare Mwiru. Roma akiwa ni Nyerere na Stamina akivaa uhusika wa mzee Kingunge. Wasanii hawa wamefanya hivi kuvuta taswira juu ya mtazamo wa watu maarufu na