Posts

Showing posts from May, 2016

TATIZO SUGU LA MAJI MIKUMI LATAFUTIWA MUAROBAINI

Image
MBUNGE WA MIKUMI ALIMAARUFU KWA JINA LA PROF JAY, AFANIKIWA KUPATA Sh. Milioni 208.6 ILI KUMALIZIA MRADI MKUBWA WA WORLD BANK KWENYE  MJI MDOGO WA MIKUMI; Siku ya tar 5 february 2016 kwenye kikao cha Tisa cha Mkutano wa pili wa bunge la 11  Mbunge wa MIKUMI Mtumishi Joseph Leonard Haule Aliuliza swali la nyongeza kwenda Wizara ya MAJI NA UMWAGILIAJI Kuna tatizo sugu la maji kwenye jimbo la Mikumi , Je Serikali ina mpango gani wa kuondoa kero ya maji katika kata ya Mikumi, Ruaha, Uleling'ombe na maeneo ya Tindiga? ? MAJIBU ya Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji ni kama ifuatavyo; Mheshimiwa naibu spika na waheshimiwa wabunge, Mheshimiwa waziri katika majibu yake ametoa taarifa kwamba tunaingia katika program ya pili kupitia sera ya mwaka 2002 ya kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2020 asilimia 85 ya watanzania wote watakuwa wanapata maji katika vijiji na asilimia 95 katika Miji. Mheshimiwa mbunge, Kwa upande wa jimbo lako la MIKUMI na kata zake, tutahakikisha kwamba tunazip

Upungufu wa madaktari,serikali inahusika

NA RUSTON MSANGI Watu husema “mtu ni afya.” Ina maana,afya ya mtu ikizorota kwa magonjwa au majeraha,shughuli au kazi zake za maendeleo hukwama.Nafsi mtu inaweza kupotea.Taifa linapoteza nguvu kazi. Afya ya binadamu ni muhimu.Daktari ni mtaalamu wa afya anayeweza kutibu,kuimarisha,kurejesha afya ya binadamu.kupuuza daktari ni kupuuza afya ya binadamu. Mahali kokote duniani,haiwezekani kujadili suala la afya ya binadamu bila kumtaja mtalaamu wa afya au daktari. Madaktari au wataalamu wa afya,wana umuhimu mkubwa kwa  afya ya binadamu.Haiwezekani kumtenganisha daktari na afya ya binadamu. Tanzania yenye idadi kubwa ya watu,ni miongoni mwa nchi zinaongoza kwa upungufu mkubwa  watalaamu wa afya kwenye  taasisi zake. Kwa Tanzania,Upungufu huu, unachangiwa na serikali kuwapuuza madaktari.Hata wachache waliopo kazini, wanamekuwa wakilalamikia kupuuzwa na serikali. Matokeo yake;maelfu ya watu wanaugua na kuteseka kwa kukosa  huduma bora.Baadhi,wamepoteza maisha wakiwa ndani ya  

JE SERIKALI INA NIA YA DHATI NA THABITI KATIKA KUBORESHA SEKTA YA AFYA AU NI KIINI MACHO KWA WATANZANIA?

Image
Na Kilawa Kilawa Wahenga walisema "Mtaka cha uvunguni sharti ainame"  nami sina budi kuyaishi maneno haya yaliyosemwa na wahenga kwani "penye nia pana njia" Naomba niaze na neno BIG RESULTS NOW (BRN) ambalo natambua kwa ujumla wake sio neno geni sana miongoni mwetu ,tuliowengi au tulio wachache bila kujali ni wasomi au sio wasomi ,masikini au matajiri,weusi au weupe, wanawake au  wanume. Naomba tuelewe  kwamba wanaoratibu mpango huu ,wametafsiri neno hili kwa lugha rahisi sana  kwamba BRN ni "MATOKEO MAKUBWA SASA". Lakini nakosa majibu kabisa katika sekta hii ya afya wanaposema matokeo makubwa sasa ilihali hadi sasa sekta hii inadolola na haina unafuu kwa Mtanzania. Neno hili BRN limekuwa likitumiwa sana na wanasiasa wengi hasa wa chama tawala pia hata wataalamu mbalimbali katika sekta mbalimbali nchini wamekuwa wakilitumia Bila kupepesa macho yangu upande wowote naomba niende moja kwa moja kwenye mjadala, kwa ujumla wake sekta ya afya ni mo

WALIMU SASA WATUMBUE JIPU LAO

Image
Hili ni moja ya bango lilokuwa limeshikwa na wafanyakazi siku ya May Mosi mwaka huu  Na Ruston Msangi. Vyama vya wafanyakazi ni taasisi kongwe.Kulingana na historia,vilianzia Ulaya wakati wa mapinduzi ya viwanda Karne ya 18 na 19. Mapinduzi ya viwanda yalitengeneza tabaka la wafanyakazi  walinyonywa na kukandamizwa na mabepari-wamiliki wa viwanda. Wafanyakazi wa viwandani,walilazimika kufanya kazi muda mrefu na katika mazingira magumu kwa malipo ya mshahara mdogo.Kulitokea vuguvugu la wafanyakazi la kudai haki. Vuguvugu hili la waajiriwa wa viwandani ndilo ambalo baadaye lilizaa vyama vya wafanyakazi wenye mshikamano wa kitaifa na kimataifa. Mshikamano wa wafanyakazi kimataifa ni chimbuko la  kuanzishwa kwa shirika la kazi duniani(ILO).Uwepo wa Vyama vya wafanyakazi unatambuliwa kwenye katiba  za mataifa mbalimbali duniani. Nchini Tanzania, Ibara ya 20 (1) ya katiba ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania(JMT) ya mwaka 1977, inatoa haki ya wafanyakazi kuunda vyama vya kut

UKUSANYAJI WA MAPATO WASHUKA KATIKA HALMASHAURI YA NANYAMBA MKOANI MTWARA

Image
mkurugenzi wa hamashauri Nanyamba Bw Oscar Ng'itu akizungumza na waandishi wa habari Katika kuunga mkonojitihada za Mh Rais wa jamhuri ya muungano   wa Tanzania Dk John Magufuli katika uhakikishaji, upatikanaji ,uthibiti na uongezekaji   mapato nchini halmashauri mpya ya Nanyamba mkoani mtwara imebainika kushuka katika ukusanyaji wa mapato kwa mwezi januari hadi Aprili. Akizungumza na blog hii mkurugenzi wa halmashauri ya Nanyamba  Bw Oscar Ng'itu  amesema kuwa ukusanyaji wa mapato  umeshuka   kwa asilimia 35% mwezi januari - April ukilinganisha oktoba –januari kutokana na asili ya wakazi wa halmashauri hiyo kwani ,wakazi wengi ni wakulima wanaotegemea kipato kupitia uzalishaji wa Korosho  zao ambalo ni la msimu kwa kuanzia mwezi wa oktoba hadi January  ,hivyo kwa miezi mingine kipato hushuka  kutokana na wengi wao kutojihusisha tena katika kilimo. Bw Ng’tu amesema kuwa kwakuwa halmashauri  hiyo kuwa ni changa kunakila jitihada  za dhati kutengeneza mifumo mipya ya

SIKU YA MANESI DUNIANI IWE NI SIKU YA NEEMA BADALA YA KARAHA KWAO

Image
Manesi wa hospital ya Lutheran Haydom wakiwa katika maandamano ya kusherehekea siku yao ya manesi.  Na Kilawa. Awali ya yote napenda kuwasalimu manesi wote duniani, shikamoni kwa mlionizidi umri pia habari za leo kwa niliowazidi umri. Naandika ukurasa huu mhimu na maridhawa kwa manesi wote duniani bila kujali jinsia wala umri. Kwanini nimeamua kuandika ukurasa huu siku hii ya leo ambayo ni siku mhimu sana kwa manesi hawa? Nimeamua kuandika ukurasa huu kwa sababu nyingi kama ifuatavyo:- 1.Nesi ni mtu mhimu sana katika utoaji wa huduma za afya kwa wagonjwa katika hospitali zetu, vituo vya afya na zahanati zetu. 2.Nesi na daktari ni kama samaki na maji, Daktari hawezi kufanya kazi zake kwa ufasaha na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa bila msaada wa nesi. 3.Nesi ni kama moyo wa hospitali, kituo cha afya au zahanati katika kuhudumia wagonjwa.Kwani nesi ndiye mtu pekee anayekaa na mgonjwa kwa mda mrefu kuliko wafanyakazi wengine wa kada ya afya katika utoaji wa huduma za af

WAKUU WA IDARA WASHAURIWA KUWA NA USHIRIKIANO NA WADAU WA ELIMU KATIKA HALMASHAURI YA NANYAMBA MKOANI MTWARA

Image
Katika kuboresha na utoaji elimu bora kwa wanafunzi wakuu wa  idara ya elimu wameshauriwa kusimamia na kuwa na ushirikiano baina ya maofisa elimu na wadau wa elimu katika halmashauri ya Nanyamba.  Akizungumza katika kikao cha  baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Maarifa ya nyumbani Nanyamba Diwani wa Kata ya kilomba Mh Majali Hamisi Majali amesema kuwa  idara ya elimu imekuwa na tabia ya kutotembelea mashuleni kujionea changamoto mbalimbali za elimu zinazo ikabili halmashauri hiyo. Sambamba na hilo  Mh Majali ameitaka idara hiyo kutumia muda huu mdogo ulio Salia kuhakikisha wanakamilisha na kutekeleza agizo la Mh Rais la utekelezaji na uondoaji wa changamoto ya madawati mashuleni. Akiupokea ushauri huo kaimu afisa elimu Nanyamba Bw Deusi Mkumbo amesema kuwa tatizo kubwa linalopekea kutotembelea kwa wakati kujione changamoto katika shule hizo ni kutokana na kutokuwepo kwa usafiri wa uhakika katika ofisi yake kunakosababishwa na uchanga wa

WATU WATATU WAKAMATWA MKOANI MTWARA KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU

Image
Watu watatu wanaotuhumiwa kujihusisha na uvuvi haramu wamekamatwa mkoani Mtwara wakiwa na vifaa vinavyotumika katika uvuvi haramu pamoja na samaki aina ya kasa. samaki aina ya kasa Dufi {noa} aliyevuliwa na watuhumiwa uvuvi haramu katika maeneo ya miseti mjini mtwara Akitoa taarifa hiyo kwa mwandishi wa habari hii Afisa habari Mtwara Manispaa Bi. Jamadi Omari amesema kuwa wavuvi hao wamekamatwa majira ya saa tatu asubuhi na maofisa uvuvi kwa kushirikiana na maofisa usalama katika eneo la Miseti Mtwara manispaa walipokuwa katika opareshini maalum ya kukamata na kukagua wavuvi wasio na lesini za uvuvi katika vijiji vilivyo katika ukanda wa bahari ya hindi kwa upande mtwara. Hata hivyo afisa habari huyo amewataka wavuvi kufuata kanuki na taratibu zinazotakiwa na serikali katika uvuvi na kuachana na uvuvi haramu usio tija na manufaa kwa jamii na serikali kwa ujumla. Kwa upande wake Afisa uvuvi manispaa ya mtwara mikindani Bw Saidi Abdallah ame

PATA ELIMU BURE KUHUSU MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII, NI ELIMU ITAKAYOKUSAIDIA KUCHAGUA MFUKO SAHIHI KWA AJILI YA MAISHA YAKO.

Na Laurent Mifuko ya hifadhi ya jamii (social security funds) ni mifuko inayotoa mafao pindi mwanachama apotezapo uwezo wa kupata kipato kwa kudumu(permanent loss of income) Hii inaweza sababishwa na 1.uzee(old age/retirement) 2.ulemavu(disability) 3.kifo (death) Kuna aina mbili za mifuko ya hifadhi ya jamii 1.defined benefits schemes-ambapo  fomula ya kukokotoa mafao atakayolipwa mwanachama inajulikana lakini fomula ya kukokotoa kiasi anachochangia hakijulikani. 2.Defined contributions schemes-ambapo fomula ya michango inajulikana lakini hakuna fomula ya mafao. Mara nyingi defined contributions schemes inatumika hasa kwa wafanyakazi wasio na mikataba ya kudumu ya ajira.. Tanzania bara kuna mifuko 5 1.National social security fund (NSSF) 2.PPF pensions fund (zamani parastatal pensions fund) 3.LAPF Pensions fund(zamani local authorities pension fund) 4.Public employees pensions fund(PSPF) 5.GEPF pension fund(zaman Government employees providend fund) Mifuko yote hi

KUTATUA CRISIS YA SUKARI: INAMPASA JPM KUSIKIA ASIYOPENDA KUSIKIA.

By Malisa GJ Kama tuna nia ya dhati ya kumsaidia Rais Magufuli kutatua changamoto ya sukari nchini, hatuna budi kumshauri kitaalamu, na sio kishabiki. Majuzi niliweka andiko hapa juu ya crisis ya sukari nchini nikieleza mbinu za kiuchumi za kukabiliana na changamoto hii na sio kutumia ubabe. Kama kweli unaipenda Tanzania na unamtakia heri Rais JPM afanikiwe ni vizuri kumshauri, kumpongeza na kumkosoa pale anapoteleza. Kuna watu wamenifuata inbox wanalalamika "Malisa hii serikali haina jema kwako, kila siku kuiponda?" Kwanza nieleza wazi kuwa huwa sipondi serikali. Kuponda maana yake ni kupinga tu bila kuwa na hoja. Mimi huwa nafanya "intellectual critics" (kukosoa kwa hoja na kushauri kwa kupendekeza alternatives ili kuleta ustawi kwa wananchi). Na Hii ndio maana ya usomi. Rafiki yangu mmoja yeye kila jambo analofanya Magufuli anashangilia na kusema "NINA IMANI NA MAGUFULI". Ni jambo jema kuwa na imani na mtu lakini kama humsaidii wala kumshauri