TATIZO SUGU LA MAJI MIKUMI LATAFUTIWA MUAROBAINI
MBUNGE WA MIKUMI ALIMAARUFU KWA JINA LA PROF JAY,AFANIKIWA KUPATA Sh. Milioni 208.6 ILI KUMALIZIA MRADI MKUBWA WA WORLD BANK KWENYE MJI MDOGO WA MIKUMI;
Siku ya tar 5 february 2016 kwenye kikao cha Tisa cha Mkutano wa pili wa bunge la 11 Mbunge wa MIKUMI Mtumishi Joseph Leonard Haule Aliuliza swali la nyongeza kwenda Wizara ya MAJI NA UMWAGILIAJI
Kuna tatizo sugu la maji kwenye jimbo la Mikumi , Je Serikali ina mpango gani wa kuondoa kero ya maji katika kata ya Mikumi, Ruaha, Uleling'ombe na maeneo ya Tindiga? ?
MAJIBU ya Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji ni kama ifuatavyo;
Mheshimiwa naibu spika na waheshimiwa wabunge, Mheshimiwa waziri katika majibu yake ametoa taarifa kwamba tunaingia katika program ya pili kupitia sera ya mwaka 2002 ya kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2020 asilimia 85 ya watanzania wote watakuwa wanapata maji katika vijiji na asilimia 95 katika Miji.
Mheshimiwa mbunge, Kwa upande wa jimbo lako la MIKUMI na kata zake, tutahakikisha kwamba tunazipa kipaumbele kuhakikisha zinapata maji katika hii programu ya pili, Na ninakuomba sana baada ya bunge hili tuwasiliane ili tuweze kupata taarifa iliyo nzuri zaidi tuanze utekelezaji...
Mbunge alifanya vikao mbalimbali na mheshimiwa naibu waziri Eng Isaac mjini Dodoma na ofisi kwa waziri jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kupatiwa Pesa za kumalizia mradi huu wa maji uliofadhiliwa na world Bank na kufanikiwa kutupatia sh milioni 208,600,000 ili zilipwe kwa Mkandarasi Anayejulikana kama MALAIKA BUILDING CONSTRUCTION and Civil works ili kuweza kumalizia asilimia 25 iliyobaki ya kukamilisha mradi huu na maji yaweze kutoka kwa wingi, Mradi huu ambao ulianza mwaka 2012 na tank lake lina uwezo wa kuhifadhi lita 300,000 za maji na kuna vituo 52 vya kuchotea maji katika sehemu mbalimbali za mji mdogo wa Mikumi umegharimu takribani shilingi za kitanzania milioni 800!! Tunaishukuru sana wizara kwa kusikia kilio cha wana MIKUMI,
Pamoja tunakwenda kuipata Mikumi Tuitakayo
#MIKUMI MPYA KWA MAENDELEO YA WATU WOTE!
Comments
Post a Comment