SIKU YA MANESI DUNIANI IWE NI SIKU YA NEEMA BADALA YA KARAHA KWAO
Manesi wa hospital ya Lutheran Haydom wakiwa katika maandamano ya kusherehekea siku yao ya manesi.
Na Kilawa.
Awali ya yote napenda kuwasalimu manesi wote duniani, shikamoni kwa mlionizidi umri pia habari za leo kwa niliowazidi umri.
Naandika ukurasa huu mhimu na maridhawa kwa manesi wote duniani bila kujali jinsia wala umri.
Kwanini nimeamua kuandika ukurasa huu siku hii ya leo ambayo ni siku mhimu sana kwa manesi hawa?
Nimeamua kuandika ukurasa huu kwa sababu nyingi kama ifuatavyo:-
1.Nesi ni mtu mhimu sana katika utoaji wa huduma za afya kwa wagonjwa katika hospitali zetu, vituo vya afya na zahanati zetu.
2.Nesi na daktari ni kama samaki na maji, Daktari hawezi kufanya kazi zake kwa ufasaha na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa bila msaada wa nesi.
3.Nesi ni kama moyo wa hospitali, kituo cha afya au zahanati katika kuhudumia wagonjwa.Kwani nesi ndiye mtu pekee anayekaa na mgonjwa kwa mda mrefu kuliko wafanyakazi wengine wa kada ya afya katika utoaji wa huduma za afya kwa siku.
4.Wanafanya kazi katika mazingira magumu lakini wanavumilia yote,kuna wakati wanatukanwa na hata kupigwa na wagonjwa au ndugu wa wagonjwa, kusengenywa na kudhihakiwa kwa kejeli, wanadharauliwa lakini wao hawajali, zaidi wanahangaika na kuokoa maisha ya watu ambao wanawahudumia.
Pamoja na hayo yote, nesi ni mtu aliyesahaurika kabisa katika maswala ya maslahi kwa ujumla.
Ukitembelea hospitali zetu hasa nchini Tanzania unamkuta nesi anafanya kazi zaidi ya punda,
Nesi ndo anagawa dawa, anachoma sindano, anatandika kitanda, anamlisha mgonjwa, anasafisha na kufanya kila linalowezekana katika kumusaidia mgonjwa lakini bado masilahi yake yapo duni sana ilihali wapo watu wamaolipwa hadi milioni,15, hadi 35.
Usiku mzima mzima nesi anakesha halali, anakubali kuiacha familia yake nyumbani na kukubali kulala na wagonjwa hospitali bila kujali kuwa anaweza pata maambukizi kutoka kwa wagonjwa wake kama vile TB, Hepatitis,na hata HIV na mengineyo, wanafanya kazi katika mazingira hatarishi sana kwa ukosefu wa vitendeo kazi lakini bado maslahi kwao ni kilio cha kudumu. Ni nani wa kuwasaidia manesi wetu ili nao wafurahie kazi yao walioisotea darasani.
Hizo zote ni sababu zinazonifanya nitamani siku hii iwe ya furaha badala ya karaha kwao Manesi.
Sasa tuone ni vitu gani vitafanya siku hii kuwa ya furaha kwao badala ya karaha?
1.Kwa ujumla wake serikali itazame kwa jicho la ziada, iangaze kwa kina katika sekta ya afya kwa ujumla, na kutatua changamoto zinazoikabiri sekta hii, Iboreshe mazingira ya kazi yawe rafiki kwa manesi hawa ili wawe na moyo ambao haujapondeka katika utendaji wao wa kazi.
2.Serikali iboreshe maslahi ya manesi hawa na kada nyingine angalau wanapohudumia wagonjwa wao wasiwe na mawazo ya hapa na pale kwani utoaji wa huduma za afya unahitaji kichwa kutulia kwakuwa manesi hawa wakiwa na mawazo hawatakuwa na moyo wa dhati katika utendaji wao wa kazi.
3.Serikali iwape mazingira mazuri ya kuishi, mazingira rafiki yenye hadhi inayoendana na kazi zao.
4.Serikali iwapromote kwa wakati manesi wanaistahili kuwa promoted badala ya kuwasumbua, pia wanaohamishwa vituo walipwe kwa wakati.
5.Serikali iwe na utaratibu mzuri wa kuwa encourage wafanyakazi wa kada hii ili kuwatia moyo na wengine wapende kazi hii.
6.Manesi wathaminiwe ili nawao waone wanathamani katika ulimwengu huu ili wafanye kazi kwa moyo.
Ninamengi ya kusema juu ya manesi hawa ambao binafsi huwa na wafananisha wao kama mama, wagonjwa kama watoto wao na madaktari baba akina baba wa familia katika hospitali na ikumbukwe katika familia zote mama huwa ni mtu pekee anayeweza kuwa karibu na watoto.
NAWATAKIA SIKU NJEMA KWENU NYOTE
Comments
Post a Comment