UKUSANYAJI WA MAPATO WASHUKA KATIKA HALMASHAURI YA NANYAMBA MKOANI MTWARA
mkurugenzi wa hamashauri Nanyamba Bw Oscar Ng'itu akizungumza na waandishi wa habari |
Katika kuunga mkonojitihada za Mh Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Magufuli katika uhakikishaji,
upatikanaji ,uthibiti na uongezekaji mapato nchini halmashauri mpya ya Nanyamba
mkoani mtwara imebainika kushuka katika ukusanyaji wa mapato kwa mwezi januari hadi
Aprili.
Akizungumza na blog hii mkurugenzi wa halmashauri ya Nanyamba Bw Oscar Ng'itu amesema kuwa ukusanyaji
wa mapato umeshuka kwa asilimia 35% mwezi januari - April ukilinganisha
oktoba –januari kutokana na asili ya wakazi wa halmashauri hiyo kwani ,wakazi
wengi ni wakulima wanaotegemea kipato kupitia uzalishaji wa Korosho zao
ambalo ni la msimu kwa kuanzia mwezi wa oktoba hadi January ,hivyo kwa miezi mingine kipato hushuka
kutokana na wengi wao kutojihusisha tena katika kilimo.
Bw Ng’tu amesema kuwa kwakuwa halmashauri hiyo kuwa ni
changa kunakila jitihada za dhati kutengeneza mifumo mipya ya uingizaji
kipato kwa wananchi na serikali kwa ujumla na pia kuzitaji mifumo hiyo kuwa ni
uanzishwa ulipaji kodi majengo,wafanya biashara na kutoa elimu kwa wakulima
juu ya uanzishwaji wa kulima aina mbalimbali ya mazao ya biashara ikiwemo
ufuta,karanga,njugu mawe,uwele,njegere,mbaazi na kuacha kutegemea zao moja la korosho
ambalo ndio zao mama katika halmashauri hiyo.
mbunge wa jimbo la Nanyamba Mh Abdalah Chikota akizungumza na wandishi wa habari nje a ukumbi wa mikutanao nanyamba |
Kwa upande wa mbunge wa jimbo hilo Mh Abdallah chikota amesema
kuwa kuna uzembe na kutokuwa makini kwa watumishi wa halmashauri hiyo
kunakopelekea kushuka kwa mapato na kuhitaji kujituma nasio kukaa ofisi kwani
wameajiriwa na serikali kwa ajiri ya kuwatumikia wananchi na sio kukaa na
kusubiria mwisho wa mwezi kupata ujira usio stahili, pia amewataka viongozi wa
halmashauri hiyo kutogemea kupandishwa kazi katika idara mbalimbali pasipo
onesha juhudi za thati walizozifanya katika kuiletea mafaniki halmashauri ya
Nanyamba.
Hata Mh
Chikota amesema kuwa yeye kama mbunge wa jimbo hilo atahakikisha wananchi na
viongozi wa halmashauri hiyo ku hakikisha mapato yanaongeza kwa kutumia
mbinu mbalimbali hasa kwa kutoa elimu kwa wananchi ya uzalishaji mazao tofauti
na Korosho .
Nanyamba ni miongoni mwa halmashauri tano mkoani mtwara zenye
utajiri wa uzalishaji wa zao la Korosho ambalo ndio nguzo kubwa ya kiuchumi kwa
wananchi wa halmashauri hizo.
Comments
Post a Comment