WATU WATATU WAKAMATWA MKOANI MTWARA KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU
Watu watatu wanaotuhumiwa
kujihusisha na uvuvi haramu wamekamatwa mkoani Mtwara wakiwa na vifaa
vinavyotumika katika uvuvi haramu pamoja na samaki aina ya kasa.
samaki aina ya kasa Dufi {noa} aliyevuliwa na watuhumiwa uvuvi haramu katika maeneo ya miseti mjini mtwara
|
Akitoa taarifa hiyo kwa mwandishi wa
habari hii Afisa habari Mtwara Manispaa Bi. Jamadi Omari amesema kuwa wavuvi
hao wamekamatwa majira ya saa tatu asubuhi na maofisa uvuvi kwa kushirikiana na
maofisa usalama katika eneo la Miseti Mtwara manispaa walipokuwa katika
opareshini maalum ya kukamata na kukagua wavuvi wasio na lesini za uvuvi katika
vijiji vilivyo katika ukanda wa bahari ya hindi kwa upande mtwara.
Hata hivyo afisa habari huyo
amewataka wavuvi kufuata kanuki na taratibu zinazotakiwa na serikali katika
uvuvi na kuachana na uvuvi haramu usio tija na manufaa kwa jamii na serikali
kwa ujumla.
Kwa upande wake Afisa uvuvi manispaa
ya mtwara mikindani Bw Saidi Abdallah amewataka wavuvi hao kuacha kuvua samaki
aina ya kasa kwa kuwa ni viumbe vilivyo hatarini kutoweka katika bahari ya
hindi.
Sambamba na hilo afisa uvuvi huyo
amesema kuwa uvuvi haramu kwa bahari ya hindi kwa upande wa mtwara ni
changamoto kubwa ambapo kunatakiwa jitihada za dhati kupambana nalo ,kwa kutoa
elimu husika katika jamii hasa kwa wavuvi waliopo katika vijiji hivyo.
Wavuvi hao wamekamatwa na vifaa visivyo
rafiki kwa mazingira ya bahari vikiwemo
nyavu kokoro,mabomu ambazo huaribu mpaka vizalia vya samaki sambamba na samaki
aina ya kasa Dufi {Noa} ambaye kwa niaba ya sheria ya serikali ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania ni miongoni mwa nyara zake.
Hata hivyo afisa uvuvi huyo amesema
kuwa aina ya kasa aliye vuliwa hajawahi kumuona katika maisha yake ya taaluma hiyo na kasa huyo aliyevuliwa na
wavuvi anakadiliwa kufikia kilogramu 250-350.
Hii ni opareshenin kabambe
iliyoanzishwa na halmashauri ya mtwara manispaa kwa kushirikiana na halmshauri
ya mtwara vijijini katika kutokomeza uvuvi haramu mkoani hapa.
Comments
Post a Comment