WAKUU WA IDARA WASHAURIWA KUWA NA USHIRIKIANO NA WADAU WA ELIMU KATIKA HALMASHAURI YA NANYAMBA MKOANI MTWARA

Katika kuboresha na utoaji elimu bora kwa wanafunzi wakuu wa  idara ya elimu wameshauriwa kusimamia na kuwa na ushirikiano baina ya maofisa elimu na wadau wa elimu katika halmashauri ya Nanyamba. 

Akizungumza katika kikao cha  baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Maarifa ya nyumbani Nanyamba Diwani wa Kata ya kilomba Mh Majali Hamisi Majali amesema kuwa  idara ya elimu imekuwa na tabia ya kutotembelea mashuleni kujionea changamoto mbalimbali za elimu zinazo ikabili halmashauri hiyo.

Sambamba na hilo  Mh Majali ameitaka idara hiyo kutumia muda huu mdogo ulio Salia kuhakikisha wanakamilisha na kutekeleza agizo la Mh Rais la utekelezaji na uondoaji wa changamoto ya madawati mashuleni.

Akiupokea ushauri huo kaimu afisa elimu Nanyamba Bw Deusi Mkumbo amesema kuwa tatizo kubwa linalopekea kutotembelea kwa wakati kujione changamoto katika shule hizo ni kutokana na kutokuwepo kwa usafiri wa uhakika katika ofisi yake kunakosababishwa na uchanga wa halmashauri hiyo, hata hivyo kuahidi kufanyia kazi changamoto hizo zinazoikabili katika idara yake.
Hata hivyo Bw Mkumbo amewataka wananchi wa halmashuari hiyo kutojenga shule pasipo husisha idara husika kwani hivi karibuni kumekuwa na tabia ya wananchi kujijengea shule katika vijiji vyao pasipo husisha wataalam kutoka halmashauri hali inayopelekea kuwepo kwa rundo la malalamiko kwa idara ya elimu kutoka kwa wananchi pasipo fahamu sheria na utaratibu za ujenzi wa shule.

Hiki ni kikao cha kisheria cha Baraza la madiwani katika robo ya pili ya mwaka  kinacho jadili hali ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika halmashauri ya Nanyamba.Hii ni halmshauri mpya iliyo tenganishwa mwaka jana kutoka katika halmashauri ya mtwara na kupekea kuongezeka kwa majimbo mengi katika mkoa wa mtwara.

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI