Posts

Showing posts from May, 2023

Muuguzi mahiri kutoka hospitali ya Taifa ya Mhimbili -Mloganzila aipaisha fani ya uuguzi nchini

 Na mwandishi wetu.  Muuguzi wa hospitali ya Taifa ya Mhimbili-Mloganzola, Bw. Wilson Fungameza Gwesa  ameibuka mshindi kwa nafasi ya tano kati ya wauguzi hamsini na mbili elfu (52,000) walioshindwa  kutoka nchi zaidi ya 200 duniani. Kwa lugha nyingine amekuwa miongoni mwa wauguzi watano bora duniani. Mashindano haya ya wauguzi yaliandaliwa na Aster Guardian Nursing Award kutoka London. Kwa namna moja au nyingine Bw.Fungameza ameliwakilisha taifa na hospitali ya MNH-Mloganzila kwa umahiri mkubwa lakini pia ameipa heshima kubwa sana fani ya uuguzi nchini. Mmoja wa watumishi kutoka hospital ya Mloganzila anamesema "Wilson fungameza amekuwa ni mbunifu na anajituma sana katika kutoa huduma za kiuuguzi kwa ufanisi mkubwa sana" Bw.Fungameza ameandika kitabu katika fani ya uuguzi kinachotumika vyuoni na maeneo ya kazi ,kwa mjibu wa mtoa taarifa anasema ukisoma kitabu hicho utajifunza mambo mengi juu ya kutambua matatizo ya wagonjwa na namna ya kuwahudumia. Mbali na uandishi wa kitab

MICHIRIZI

  Utangulizi Ipo mistari inayoweza kutokea mwilini maarufu kama “mistari ya unene”. Mistari hii hutokea zaidi kwa sababu ya mabadiliko katika uzito wa mwili. Unaweza kuona mistari hii katika sehemu mbalimbali za mwili wako hasa kwenye matiti, nyonga na makalio. Mistari hii haina madhara yoyote kwa mwili lakini baadhi ya watu hawafurahii muonekano huo. Mistari hii hufifia kadri muda unavyokwenda hata bila matibabu yoyote. Una uwezekano mkubwa zaidi wa kupata mistari hii kama ni: i. Mwanamke; ii. Una ndugu wenye mistari hii; iii. U mjauzito; iv. Umeongezeka uzito wa mwili kwa ghafla; v. Unapitia kipindi cha balehe; vi. Unatumia dawa za steroids vii. Misuli yako imekua kwa ghafla kwa kunyanyua vitu vizito na viii. Kama una baadhi ya magonjwa mf. "Cushing syndrome" (kwenye ugonjwa huu homoni ya cortisol inakuwa juu mwilini. Mbali na kujitokeza mistari hii, kunakuwa na dalili zingine pia kama pressure kuwa juu, mafuta kujaa zaidi kuzunguka tumbo na shingoni, ngozi kuchubuka kirahi