MICHIRIZI

 

Utangulizi


Ipo mistari inayoweza kutokea mwilini maarufu kama “mistari ya unene”. Mistari hii hutokea zaidi kwa sababu ya mabadiliko katika uzito wa mwili. Unaweza kuona mistari hii katika sehemu mbalimbali za mwili wako hasa kwenye matiti, nyonga na makalio.

Mistari hii haina madhara yoyote kwa mwili lakini baadhi ya watu hawafurahii muonekano huo. Mistari hii hufifia kadri muda unavyokwenda hata bila matibabu yoyote.


Una uwezekano mkubwa zaidi wa kupata mistari hii kama ni:

i. Mwanamke;

ii. Una ndugu wenye mistari hii;

iii. U mjauzito;

iv. Umeongezeka uzito wa mwili kwa ghafla;

v. Unapitia kipindi cha balehe;

vi. Unatumia dawa za steroids

vii. Misuli yako imekua kwa ghafla kwa kunyanyua vitu vizito na

viii. Kama una baadhi ya magonjwa mf. "Cushing syndrome" (kwenye ugonjwa huu homoni ya cortisol inakuwa juu mwilini. Mbali na kujitokeza mistari hii, kunakuwa na dalili zingine pia kama pressure kuwa juu, mafuta kujaa zaidi kuzunguka tumbo na shingoni, ngozi kuchubuka kirahisi zaidi n.k)


Wakati gani uonane na daktari

1. Onana na daktari kama una wasiwasi kuhusiana na muonekano wa ngozi yako na

2. Michirizi yako imekuja ghafla na inaambatana na dalili zingine mf. kuongezeka uzito  hasa eneo la shingoni, sura kuwa ya duara na kuchubuka kirahisi.


Matibabu

Michirizi hii ina kawaida ya kufifia kadri muda unavyokwenda. Hakuna tiba inayoweza kumaliza kabisa shida hii lakini yafuatayo yanaweza kuifanya ikafifia isionekane sana:


i. Cream ya retinoid;

ii. Matibabu ya mwanga/mionzi na

iii. Matibabu ya kuchomwa visindano vidogo vidogo.


Vitu vifuatavyo havina madhara LAKINI havijathibitishwa kuzuia au kuondoa michirizi.

i. Cocoa butter;

ii. Vitamin E;


Kuzuia

Hakuna namna ya kuzuia michirizi hii isitokee, lakini unaweza kufanya yafuatayo ili kuiweka Ngozi yako katika hali nzuri; 


i. Paka cream/mafuta za kusaidia ngozi yako kubaki na unyevunyevu;

ii. Ongeza sana matunda na mbogamboga za majani kwenye milo yako na

iii. Shughulisha mwili wako zaidi.


Uliza maswali yako kwenye comments.


#StretchMarks#SkinCare#CushingSyndrome#HealthyLiving#

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI