Posts

Showing posts from June, 2016

MASOKO YA MTWARA MIKINDANI YAKABILIWA NA TATIZO LA VYOO

Baadhi ya wafanyabiashara katika soko la kijiji cha mkunjanguo katika kata ya Naliendele mkoani Mtwara wamelalamikia ukosefu wa huduma muhimu ikiwemo choo katika soko hilo. Wakizungumza  sokoni hapo na mwandishi wa habari hii baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema kuwa  changamoto hiyo imekuwepo sokoni hapo kwa muda mrefu jambo ambalo limekuwa likiwapa usumbufu mkubwa na kuwaweka katika hatari ya magonjwa ya milipuko katika eneo hilo. Uongozi wa eneo hilo akiwemo mwenyekiti wa kijiji hicho wamekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kudai kuwa eneo hilo halikidhi vigezo vya kuwa soko na kuwa na kuwa awali mzabuni ambaye alipewa dhamana ya soko hilo alishindwa kujenga vyoo sokoni hapo.  Hata hivyo ameongeza kuwa jitihada zinaendelea kuhakikisha soko hilo linapata vyoo na kuwa wataanzisha utaratibu mpya wa kutoza ili kuwezesha kujenga vyoo hivyo. Aidha masoko mengi katika manispaa ya Mtwara mikindani  yanakabiliwa na uhaba wa vyoo bora jambo ambalo linatishia afya za wafanya

CHAMA CHA USHIRIKA MKOANI MTWARA CHAWATAKA WAFANYA BIASHARA WA MAZAO KUFUATA MISINGI NA TARATIBU ZA KIBIASHARA

Chama cha ushirika wa wakulima mkoani Mtwara kimewataka wanunuzi wa mazao mbalimbali kuacha kutumia mizani kwa kuwa ni kosa kisheria na ni unyonyaji kwa wakulima. Wito huo umetolewa na Kamimu Mkurugenzi wa chama hicho mkoani hapa Bw. Laurence Njozi ambapo amesema kuwa chama hicho hakitasita kuwachukulia hatua wale wote watakaobanika kufanya manunuzi kwa njia hiyo isiyo halali. Amesema kuwa ili kuepukana na tatizo hilo pia ni vema kwa wakulima kuwa na subira ya kuuza mazao yao ghalani na kuachana na utaratibu wa kuuza reja reja kwa kuwa unawaumiza. Ameongeza kuwa chama hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya wakulima kukosa uvumilivu kwa kucheleweshewa malipo yao pamoja na wanunuzi hao wadogo ambao hununua kinyume cha sheria. Aidha serikali imepiga marufuku uuzaji wa mazao kwa kutumia mizani kwa wanunuzi wa reja reja na kujaza rumbesa kwa kuwa inawanyonya wakulima.

MAKAMU MWENYEKITI BAVICHA BARA MH PATRICK OLE SOSOPI AKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI IRINGA

Image
Tayari Jeshi la  Polisi limemkamata Makamu M/kiti wa BAVICHA muda huu hapa Iringa Mjini baada tu ya kumaliza Mahafali ya CHASO. Kosa ni la uchochezi wa Kisiasa ambalo alilitenda akiwa DSM katika Mahafali ya CHASO ya tarehe 18/06/2016. Hivyo atasafirishwa kutoka Iringa kwenda DSM kwaajili ya mahojiano na baadae Mahakamani. Imetolewa June 26 Edward Simbeye Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa

DHANA YA UONGOZI NA UTAWALA WA SHERIA TANZANIA

Image
Na Emmanuel Chengula, Kiongozi ni mtu ambaye amechaguliwa na watu katika jamii ili awaonyeshe njia ya kutatua matatizo, namna ya kuhitajiana katika kuishi na namna ya kuangalia changamoto zinazoikumba jamii na kuzitatua. Aidha kiongozi hutengenezwa ama pengine mtu huzaliwa akiwa kiongozi. Utawala wa sheria ni ile hali ya uongozi kuhakikisha kwamba kila jambo linaloamuliwa kufanywa na jamii ama na uongozi uliopo unafuata misingi ya haki na utawala bora kwa mujbu wa sheria za nchi zilizopo. Inafahamika kwamba mara zote kiongozi wa mwisho katika nchi nyingi huwa ni rais/mfalme n.k na kauli zao mara nyingi zitolewapo huchukuliwa kama sheria(presidential decree/orders) ndani ya jamii husika. Sheria za jamhuri ya Muungano wa Tanzania zipo open sana mfano ukisoma ibara ya 13(6) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema every person is presumed innocent unless proved contrary ( yaani kila mtuhumiwa katika jamii hudhaniea hana kosa mpaka pale itakapothibitka kwamba kafanya

MSTAHIKI MEYA WA KINONDONI MH BONIFACE JACOB AFUNGUKA JIONI YA LEO

Image
TAARIFA KWA UMMA KUTOKA KWA MSTAHIKI MEYA BONIFACE JACOB Asalaam aleikum wananchi wa wilaya ya kinondoni na viunga vyake, niendelee kuwaombea ndugu zetu waislamu funga yao iwe na heri na baraka tele ikiwa leo ni chungu cha 19. Leo tarehe 25 june 2016, nimepigiwa simu nyingi sana na kupokea taarifa kwa njia mbalimbali, nikiulizwa nilipo? kwanini sipo kwenye tukio la Biafra la uzinduzi wa shughuli ya jeshi la polisi? na wengine wakiniuliza neno baada ya kuuliziwa hadharani na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. MHESHIMIWA RAIS John pombe Magufuli; Mstahiki meya manispaa ya kinondoni leo siku ya jumamosi kijana wako na mtumishi wa wananchi wa manipsaa ya kinondoni nilikuwa naunga mkono shughuli za usafi. Nimeshinda na wananchi wa ubungo kisiwani kutwa tukifukua mitaro ya maji machafu kuhakikisha usalama wa afya za ubungo kisiwani zipo salama na zaidi kuweka miundo mbinu yetu sawa. Nami nilitamani sana kukuona japo kwa karibu sana au kuongea na wewe mambo kadhaa k

TUKIO LA UPANDAJI MITI LILIVYOFANYIKA MKOANI MTWARA LINATIA HAMASA KWA WANANCHI

Image
Mh mkuu wa wialaya mtwara Fatuma Alli akizindua upandaji miti eneo la bodi ya  korosho tanzania mjini mtwara Othmanai Kambi mhasibu wa Tanroad mkoa mtwara akishiriki zoezi la upandaji miti M Makamu mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani mtwara Jimmy mahundi akishiriki zoezi la uapandaji miti mtwara mannispaaa Ongeza kichwa Dereva wa gari ya mkuu wa wilaya Bw Abillah akishiriki zoezi la upandaji miti 

TAKRIBANI MITI 50 YAPANDWA MKOANI MTWARA

Image
Serikali mkoani Mtwara imepanda jumla ya  miti 50 kutoka bodi ya Korosho hadi viwanja vya Mashujaa vilivyopo mtwara manispaa ili kuboresha,kupendezesha na kulinda hifadhi ya barabara . Akizindua upandaji huo mkuu wa wilaya Mtwara Bi Fatuma Alli amesema kuwa tukio hilo lililofanywa na ofisi ya Tanroad Mtwara ni jambo la kuigwa na kuwataka wananchi kuhifadhi mazingira kwa kufanya usafi,kupangilia ujenzi wa makazi na  kupanda miti katika maeneo tunayoishi. Pia  mkuu wa wilaya mtwara amewataka wananchi kushirikiana na Tanroad  kwa kuwa makini na wale wanaovamia hifadhi ya barabara  kwa kujenga na kuweka mabango pasipo fuata taratibu za kuhifadhi wa barabara kwani kama wanauhitaji wa kuweka mabango wafuate taratibu husika ili wasijikute wanaingia katika mikono ya kisheria kupitia ofisi husika. Naye mhandisi  kutoka Tanroad Bw Edward kokina amesema kuwa hii ni katika kuunga mkono siku ya mazingira iliyo azimishwa  tareh 6/6/2016 na kuamua kupanda miti ikiwa na lengo kuwasaidia w

VIJANA WASHAURIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIBIASHARA ILI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA AJIRA

Image
Vijana mkoani Mtwara wametakiwa kutambua fursa za kibiashara zilizopo kwa kuwa tayari kuungana na mashirika mbalimbali yanayo wekeza na kutoa elimu ya kibiashara hasa ya kiujasiriamali mkoani hapa. Akizungumza katika semina fupi iliyo husisha walezi  wajasiria Mali wilayani mtwara katika ukumbi wa Naville Novell hotel mtwara Manispaa kaimu mgeni rasmi Bw JOHANSEN K. BUKWALI ambaye pia katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji mkoani mtwara amewataka vijana kutobweteka kwa kukaa vijiweni bali wajiingize ktk vikundi vya uzalishaji mali na kuipa kipaumbele elimu ya ujasiriamali inayotolewa na mashirika mbalimbali mkoani humu. Bwana Bukwali ameishukuru Taasisi ya ujasiriamali na ushindani Tanzania (TECC)tawi la Mtwara kwa kuwawezesha vijana kupata elimu ya ujasiliamali na kuwaomba kuendelea na moyo huyo kwa kuwawezesha vijana kupata elimu hiyo itakayo wezesha kupunguza tatizo la aajira kwa vijana na kuwakomboa kiuchumi. Groria Nyandindi na Abdallah Chilangala ambao ni

NANYAMBA YAMALIZA TATIZO LA MADAWATI KWA ASILIMIA 100%

Image
Ongeza kichwa Meneja wa TTCL mkoa wa Bw Umishael Temba kushoto  akimkabidhi mkuu wa wilaya mtwara Fatuma Alli moja kati ya madawati 40 Katika kuunga mkono agizo la Mh Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe magufuli halmashauri mpya ya Nanyamba mkoani Mtwara imekamilisha kwa asilimia 100% utengenezaji wa madawati katika shule za msingi na sekondari. Akipokea msaada wa meza na viti 40 kutoka kwa kampuni ya mawasiliano ya simu Tanzania TTCL mkuu wa wilaya Mtwara Bi Fatuma Alli amesema kuwa anashukuru kampuni hiyo kwakuona umuhimu wa elimu  na kuahidi kutowaangusha katika utunzaji wa samani hizo. Sambamba na hilo Fatuma Alli amesema kuwa meza na madawati hayo yanapekwa katika halmashauri ya Nanyamba ambako kwa idadi hiyo itamaliza tatizo la meza na madawati  kwa asilimia 100% katika shule za msingi na sekondari. Kwa upande wa maneja wa simu Tanzania TTCL mkoa wa Mtwara Mhandisi  Rumishael Temba amesema kuwa wao kama kampuni ya mawasiliano ni sehemu ya

MTOTO WA UMRI WA MIAKA 8 ABAKWA MKOANI MTWARA, MTUHUMIWA KUFIKISHWA MAHAKAMANI TAREHE 22/6/2016

Image
Kamanda wa polisi mkoani   ACP HENRY MWAIBAMBE akizungumza na waandishi juu y taarifan ya ubakaji Jeshi la polisi mkoani mtwara linamshikiria ANDREA  DANIEL MICHAEL ,miaka 28 ,mkzi wa kijiji cha Magumchila kata ya Jida ,Wilayani masasi kwa kosa la kumbaka mtoto wa  umri wa mika ‘8’ ambaye pia ni mwanafunzi wa Darasa la pili shule ya msingi Magumchila. Akitoa taarifa hiyo kamanda wa polisi mkoani mtwara ACP HENRY MWAIBAMBE anesema kuwa tukio hilo limetoke tarehe 16/6/2016 majira ya saa 10;00 asubuhi siku ya alhamisi ,ambapo mama mzazi wa binti huyo alishtukia nyendo za mtoto wake ,kwamba hatembei vizuri na ndipo alipoanza kumuuliza nini kimemsibu kinachosababisha kutotembea vizuri. Hata hivyo mama wa mtoto huyo aliendelea kumuuliza mara kwa mara na mtoto kukataa kuwa haja faywa kitu chochote  ndipo mama huyo alipo amua kumchukua na kumpeleka kituo cha polisi alipoulizwa tena mbele ya polisi akakiri  na kumtaja mtuhumiwa huyo na kueleza kwamba huwa anamvizia akitoka shulen