MTOTO WA UMRI WA MIAKA 8 ABAKWA MKOANI MTWARA, MTUHUMIWA KUFIKISHWA MAHAKAMANI TAREHE 22/6/2016

Kamanda wa polisi mkoani   ACP HENRY MWAIBAMBE
akizungumza na waandishi juu y taarifan ya ubakaji

Jeshi la polisi mkoani mtwara linamshikiria ANDREA  DANIEL MICHAEL ,miaka 28 ,mkzi wa kijiji cha Magumchila kata ya Jida ,Wilayani masasi kwa kosa la kumbaka mtoto wa  umri wa mika ‘8’ ambaye pia ni mwanafunzi wa Darasa la pili shule ya msingi Magumchila.

Akitoa taarifa hiyo kamanda wa polisi mkoani mtwara ACP HENRY MWAIBAMBE anesema kuwa tukio hilo limetoke tarehe 16/6/2016 majira ya saa 10;00 asubuhi siku ya alhamisi ,ambapo mama mzazi wa binti huyo alishtukia nyendo za mtoto wake ,kwamba hatembei vizuri na ndipo alipoanza kumuuliza nini kimemsibu kinachosababisha kutotembea vizuri.

Hata hivyo mama wa mtoto huyo aliendelea kumuuliza mara kwa mara na mtoto kukataa kuwa haja faywa kitu chochote  ndipo mama huyo alipo amua kumchukua na kumpeleka kituo cha polisi alipoulizwa tena mbele ya polisi akakiri  na kumtaja mtuhumiwa huyo na kueleza kwamba huwa anamvizia akitoka shuleni na kumpeleka kwenye nyumba bovu na kumfanyia kitendo na kumtishia asiwaambie wazazi wake.

Sambamba na hilo taarifa za ndani la tukio hilo linaeleza kuwa mtuhumiwa alikuwa anampatia mtoto huyo kati ya Tsh 500 hadi 1,000/= na ni muda mrefu huwa anafanya vitendo hivi.

Kwa taarifa ya mganga wa hospitali ya wilaya masasi mkomaindo baada ya kufanyiwa vipimo vilionyesha ni kweli alifanyiwa kitendo cha kikatili na kuambukizwa magonjwa ya zinaa (KASWENDE).


Upelelezi umekamilika na mtuhumiwa kukamatwa na kupelekwa mahakamani kwa kesi no.93/2016,usikilizwaji wa awali unaanza tarehe 22/06/2016.

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI