UPATIKANAJI AJIRA KIWANDA CHA CEMENT MTWARA CHA KUTWA NA KASHIFA NZITO
Wananchi na viongozi wa vijiji vinavyo zunguka kiwanda cha
cement cha DANGOTE mkoani mtwara wamewalalamikia wajiri wa kiwanda hicho kuwepo kwa upendeleo na
harufu ya rushwa katika upatikanaji wa
ajira kiwandani hapo.
mwonekano wa nje wa kiwanda cha Dangote |
Akizungumza kwa hisia kali katiak kiakao kilichofanyika
kwenye ukumbi wa shule ya msingi msijute mwenyekiti wa kijiji cha Naumbu kusini
Bwa Hamza Fuja amesema kuwa matakwa na utaratibu ambao wao walipewa na mmiliki
wa kiwanda hicho mwanzoni wakati kinajengwa imekuwa tofauti na utaratibu
unafanywa hivi sasa’’ siku ya ufunguzi
wa wa ujenzi wa kiwanda hicho Mh Alhaji Aliko Dangote alisema kuwa vijana na
wananchi wa eneo linalozunguka kiwanda watapewa kipaumbele kwa nafasi za ajira
lakini sasa hivi imekuwa tofauti na kauli hiyo’’.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa taratibu na matangazo ya ajira
umekuwa usio ridhisha kwani hutoa matangazo ya kazi siku moja kabla ya usaili
hali ambayo viongozi,vijana na wazee wa maeneo husika kupatwa na mshaka ya
upataji ajira na kupelekea tuhuma za uwepo wa vitendo vya rushwa katika upatika
naji wa kazi katika kiwanda hicho kwa kuwepo baadhi ya wageni kutoka nje ya
mikoa ya lindi na mtwara wanao pewa nafasi ya kazi katika
kiwanda hicho.
Mkuu wa wilaya akiwa na baadhi ya viongozi wa kiwanda cha cement cha Dangote katika mkutano wa kupokea malalamiko ya wananchi wa vijij vinavyo zunguka kiwanda hicho |
Ali Nalinga ambaye alikaimu nafasi ya mwenyekiti wa kijiji
cha Hiari eneo ambalo kiwanda kimejengwa amesema kuwa akiwa kaimu mwenyekiti
alipokea vijana kutoka mikoa tofauti na mtwara wakiwa wakiwa na fedha zao
wakihitaji kupata muhuri wa kijiji ili watambulike kuwa wanakijiji wa kijiji
hicho hali iliyo mpa mashaka kwatekelezea mahitaji yao.
Naye mwanasheria wa kiwanda hicho {unique consultance
company} ucc Bwana Robert Mwakaia amesema kuwa wanaajiri wafanya kazi kwa
kufuata taratibu na kanuni zinazo waongoza na huajiri wafanyakazi kwa misingi
ya sheria na kuzingatia taaluma husika kwa mwaajiriwa.pia amesema tatizo kubwa
linalo wakuta vijana na wakazi wa maeneo husika kutopata ajira ni kutokidhi
vigezo na mahitaji ya nafasi husika
,hata hivyo amewahakikishia vijana hao kupewa kipaumbele pindi zitakapo
tokea nafasi za kazi hasa zisizo hitaji taaluma ya kutosha.
Meneja rasilimali watu na utawala kiwanda cha Dangote GERVARS CHAPARWA akizungumza na wananchi wa tarafa ya mayangana na mpapura |
Naye meneja rasilimali watu na utawala Gervas Chparwa
amewataka wananchi wanao zunguka kiwanda hicho kutoa ushirikiano pindi waonapo
vitendo vya uvunjifu wa maadili kutoka kwa watumishi na wafanya kazi wa kiwanda
hicho kwani manufaa na faida ya kiwanda hicho ni kwa ajiri ya wote nasio
wamilki pekee.
Pia amewahidi kutekeleza ahadi zilizo tolewa wakati kiwanda
kinajengwa kwa vijiji vinavyo zunguka mradi huo ambapo kati ya ahadi hizo ni
pmoja na kujenga soko ,stendi za kisasa,shule,kituo cha afya na fedha shilingi
mili 450 kwa ajiri ya kusaidia maendeleo ya vijiji rafiki na kiwanda hicho.
Sijakuelewa mr miller porter
ReplyDelete