LEICESTER CITY KUITIA HASARA KAMPUNI YA KAMALI

Timu LEICESTER CITY wakishangilia goli katika moja ya mechi zao.

Kushoto chini ni Washambuliaji, Vardya na Mahrez. Kulia ni Leigh Hebert, mashabiki anayesubiri kushinda kitita cha Pauni 25,000 endapo timu yake ya LEICESTER CITY itabeba ubingwa wa ligi kuu msimu huu. 

   
                                                     Mazoezi ya LEICESTER CITY.

Endapo LEICESTER CITY itashinda kombe la ligi kuu Uingereza msimu huu, basi fundi seremala kutoka kitongoji cha Guildford huko Uingereza atashinda kiasi cha pound 25,000, zaidi ya Tsh milioni 75 baada ya kuweka 'bid' ya paund 5 (Tsh. Elfu 15) kwenye mchezo wa kamali; Fundi Leigh Hebert, amekataa ofa ya paund 3200 (Tsh milioni 9.6) aliyopewa na kampuni hiyo ya kamali ili aondoe utabiri wake na kusema anataka kushinda paund zote 25000 au hata akipoteza paund 5 aliyoweka haina noma.
"Nataka kushinda kiasi cha paund 25,000 nitumie na mchumba wangu KERRY, nimechoka kuishi nyumba za kupanga" anasema Leigh Hebert mwenye umri wa miaka 38.
Kampuni hiyo ya kuchezesha kamali ya William Hill itapata hasara ya karibu paund milioni 4 (Tsh. Bilion 12) kwa kuwalipa mashabiki wa LEICESTER,  wanaume 24 na mwanamke mmoja waliotabiri kuwa LEICESTER CITY itashinda kombe la ligi kuu msimu huu.
Hata hivyo mtu atakayeshinda pesa nyingi zaidi ni 'Andrew', mwenye umri wa miaka 52. Andrew atashinda paundi 33,333 (Tsh. Milion 100).

LEICESTER CITY imebakiza point 3 ili kujinyakulia Ubingwa kati ya mechi tatu zilizobaki dhidi ya Man Utd; Tar 30 April, Everton; Tar 7 mei na Chelsea Tar 15 mei.

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI