ALIYEVUMBUA 'TAFADHALI NIPIGIE' AISHINDA VODACOM MAHAKAMANI


Ni NKOSANA MAKATE, kijana aliyegundua huduma ya tafadhali nipigie akiwa mfanyakazi wa Vodacom huko Johannesburg nchini Africa kusini. Hiyo ilikuwa Nov 2000. 
Ilipofika February mwaka 2001 huduma hiyo ilianza kutumiwa rasmi na Vodacom. Hata hivyo Mr. Makate alitaka kulipwa fedha kwa uvumbuzi wake huo ambao umeingizia Vodacom faida ya dola za kimarekani bilioni tano. (USD 5b). Ndipo alipofungua kesi mahakamani baada ya 'kudhurumiwa' haki yake. 
Mwaka 2014, Mahakama ya mjini Johannesburg iliipa ushindi kampuni ya Vodacom kwa kigezo kwamba Mr. Makate alikubaliana kwa maneno na Mr. Phillip Geissler ambaye alikuwa mkurugenzi wa maboresho ya huduma za kampuni. Mahakama ilisema kwamba Mr. Makate na Mr. Geissler walikubaliana kwa maneno na hivyo kampuni ya Vodacom haihusiki. 

Lakini tar. 26/04/2016 mahakama ya katiba nchini Africa kusini imeamua kuwa Vodacom imlipe Mr. Makate ndani ya siku 30. Haijajulikana Mr. Makate atalipwa kiasi gani ingawa mwenyewe alitaka kulipwa asilimia 15 ya faida iliyopatikana.
Makate amekuwa akipambana na Vodacom mahakamani kwa miaka 10. 

15/100 × 5billion dollars. (Tsh. trilion 10) = 750 million dollars. (Tsh. 1.5 trillion)

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI