MEYA WA KINONDONI AGAWA BURE MAENEO YA BIASHARA ASUBUHI YA LEO

Meya akiongea na wafanyabiashara leo la asubuhi



Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob leo Ijumaa 29/04/2016 amefanya ziara katika eneo la ubungo na kuongea na wafanyabiashara ikiwemo kuwaonyesha eneo la kufanya biashara zao.

Amewataka wafanyabiashara hao kesho wasiwepo maeneo hayo na kuhamishia biashara zao katika eneo la soko la Mawasiliano (Sinza), kwani wasipofanya hivyo Kamati ya usalama na ulinzi  na usalama Manispaa ya Kinondoni imeshakaa na imepanga kuwaondoa.

Meya ameona isingekuwa busara kuwaondoa bila kujua watakwenda wapi, Meya amewakabidhi wafanyabiashara hao kadi ambazo watazionyesha ili  wasisumbuliwe,pia amewataka wasilipe pesa yeyote endapo watatakiwa walipie maeneo ya biashara waliyopewa.

Pia amesema kuhusu ushuru hawatalipa kwa muda wa mwezi mmoja baada ya hapo watalipia, amewahakikishia wafanyabiashara hao hakuna atakayekosa eneo la kufanya biashara.

Afisa biashara wa Manispaa ya Kinondoni amewataka wafanyabiashara kutokaidi agizo hilo kwani Meya aliomba aje azungumze nao kwanza ili wasishtukizwe bila kupewa taarifa,hivyo kuanzia kesho wataondolewa kwa nguvu.

Meya amesema kuna maeneo wamepewa madiwani akiwemo yeye na hayafanyiwi biashara, hivyi sio sawa maeneo hayo wapewe wafanyabiashara.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, amewaahidi wafanyabiashara hao kwamba kesho atafika katika eneo hilo ili kuona jinsi wafanyabiashara hao wanavyoendelea na kuangalia changamoto zilizopo ili zitatuliwe kwa haraka ili wafanyabiashara hao wafanye biashara zao katika hali nzuri.

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI