Posts

Showing posts from 2015

MWENYEKITI WA CCM MKOA NA KATIBU MWENEZI WA MKOA WA ARUSHA WAIBWAGA CCM NA KUTIMUKIA CHADEMA

Image
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Onesmo Ole Nangoro na Katibu Mwenezi wa mkoa Joseph Kadogoo wamejiunga na CHADEMA leo

JIPATIE NYUMBA YA KISASA YENYE HADHI YA KIMATAIFA KWA BEI POA ILIYOPO MKOANI GEITA, KWA MAELEZO ZAIDI PIGA NAMBA 0687812220 au 0659970824

Image
Hii ndio nyumba ya kisasa inayouzwa mkoani Geita kwa mawasiliano zaidi piga  0687812220 au 0659970824 Ewee Mdau wa maendeleo, mpenda maendeleo, mpambanaji wa ukweli jipatie nyumba nzuri yenye hadhi nzuri kwa bei poa kabisa. "Nyumba hii ipo sehemu nzuri sana eneo la Mtaa wa Msufini katika kata ya Kalangalala, Makao makuu ya mkoa wa Geita" Kwa mjibu wa mmiliki wa nyumba hiyo alisema Nyumba yake ina vyumba 17 kila chumba kina ofisi yake kubwa yaani" Toilet" kwa kifupi  ni kwamba kila chumba ni  Self. Mmiliki huyo alisema pia "Nyumba yangu inafaa kwa kukaa familia  au biashara kutakana na uwingi wa idadi ya vyumba, ni nyumba yenye ubora na muonekano mzuri tena wa kisa

MALIMU SEIF,MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR AFUNGUKA BAADA YA MWENYEKITI WA CUF PROF. LIPUMBA KUJIUZULU

Fungua hapa umsikie alichosema

Mh EDWARD NGOYAI LOWASSA NI MSAFI

Image
Na Dr. Shindo Kilawa Mh Edward Lowassa  akiwa ameshika fomu ya kuwania urais kupitia Chadema Watu wengi wataishangaa kauli yangu, watakaa midomo wazi na kujiuliza maswali kibao moja ya maswali watakayojiuliza ni kama yafuatayo. Anasema EL ni msafi wakati alithubutu kumuita Fisadi? Usafi wake uko wapi au kwa kuwa kahamia Chadema? Huyu anayesema haya ni mamluki au Chadema kweli? Hayo ni baadhi tu ya maswali japo najua kuna maswali mengine mengi zaidi juu ya mh EL. Wanapoendelea kujiuliza ni vyema na mm niwaulize maswali kadhaa kama ifuatavyo? Kama EL ni mwizi au fisadi ni kwanini hadi leo hajakamatwa na kupelekwa Mahakamani? Je hajakamatwa kwakuwa serikali ni dhaifu au haijui sheria inazosimamia yenyewe au iliogopa kuumbuliwa zaidi? Toka 2008 hadi leo nini kimefanyika baada ya EL kwa kulinda heshima yake na kuamua kujiweka pembeni? Tunadhani ni kwanini jina lake liliishia njiani? papo hapo jiulize kwanini Rizone alitweete akionesha hayupo tayari kuona Rais akit

MALEZI YA MTOTO, DEMOKRASIA NA HATIMA YA MAENDELEO YA NCHI YETU.

Image
Na Dr. Elias Mwakapimba Katika malezi ya mtoto kuna vitu vingi ambavyo vinaathiri afya kwa ukuaji mzuri. Vitu hivi ni elemu/uelewa wa mzazi, uwezo wao wa kiuchumi/kipato na mazingira wanamoishi. Haya mambo ni nguzo muhimu katika kuimarisha afya thabiti kwa ukuaji na mafanikio ya mtoto baadaye. Wazazi wa mtoto wanaweza kuwa na elimu/uelewa wa kulea mtoto lakini hawana uwezo wa kumudu mahitaji kwa afya njema ya mtoto. Wanaweza wakawa na kipato kizuri lakini wasiwe na elimu/uelewa wa namna ya kuanda lishe nzuri ya mtoto. Au wanaweza wakawa navyo vyote lakini mazingira yasiwe rafiki katika kuandaa lishe ambayo ni muhimu kwa afya ya mtoto (mfano vita/ukimbizi) au wakaweza kuandaa lishe lakini mazingira tena yasiwe rafiki kuruhusu mtoto kufaidi virutubisho vya lishe na asiweze kukua katika afya (mfano magonjwa). Katika makundi mawili ya awali: ukosefu wa elimu au kipato, au ukosefu wa vyote au uwepo wa vyote lakini mazingira yasiwe rafiki hupelekea mtoto kuwa na utapia mlo (mtoto

TATIZO LABDA NI MWALIMU NYERERE NA CCM YAKE.

Image
Na Mwl Bongole Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu  Yapo mambo muhimu mengi na muhimu sana yanayopaswa kuzingatiwa na kuangalia kama kweli leo hii tunahitaji kukomesha ufisadi rushwa kuongeza fursa za ajira na kutoa huduma za jamii kwa kiwango ambacho kinaweza kukidhi haja ya watanzania. Ili kufikia mabadiliko ya kimfumo ambayo kiuhalisia chanzo chake ni kupoteza dira kwa chama cha mapinduzi basi tunahitaji mtu imara, jasiri, mwelewa, mwenye malengo na uzoefu wa kubadilisha mifumo iliyomibovu na kuleta mfumo mzuri. Kwa hapa tulipofikia ni vigumu sana yeyote ndani ya ccm kufumua mfumo uliozeeka wa kifisadi kibaguzi kandamizi na usiopenda mabadiliko. Mfumo uliopo ndani ya ccm umejikita katika kuangalia kulinda na kutetea CHAMA KWANZA huku vipaumbele kama afya elimu na aina zote za huduma za jamii zikiwa duni. Ni mfumo wa kutizama maslahi ya vyombo vya ulinzi kama vile Polisi kwa kuwekeza nguvu kubwa huko ili kuendelea kulitumia katika kufanikisha maslahi yake. Si jambo la aja

HAKUNA MATARAJIO MAPYA KWENYE MFUMO ULE ULE

Image
Na Musa Makongoro Tayari chama cha mapinduzi kimempata, mgombea urais wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa njia za mizengwe na kupelekea mpasuko ndani ya chama hicho kuonekana hadharani. Mgombea huyu ni Dr John Pombe Maghufuli, ambaye ni waziri wa ujenzi wa serikali inayoondoka madarakani. Ni kama vile watanzania wengi, wanakubali kwamba huyu ndiye anaeweza kuirudisha nchi pale ilipokuwa na kwamba atakidhi matarajio yao. Pamoja na umahili wake wa kukariri takwimu mbalimbali, kitendo kilichomjengea umaarufu miongoni mwa watanzania wengi wasiofuatilia mambo, John Pombe Magufuri ataingia kusimamia mfumo ule ule. Tumesahau kwamba ni Magufuri huyuhuyu, ameshiriki kupitisha sheria mbovu kabisa na zenye maslahi binafsi ya baadhi ya wana CCM bungeni. Wakati bunge maalumu la katiba likiizika rasimu ya jaji waryoba, iliyokuwa imesheni maoni ya wananchi alikuwamo bungeni na hakuonyesha nia yoyote ya kutetea wananchi wa Tanzania. Rundo la kashfa zikiwemo za upotevu wa m

JOHN POMBE MAGHUFULI AIBUKA KIDEDEA KWA 87.1%

Image
Ni saa 12:49  Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM), Dr Kikwete alipoanza kutangaza rasmi na kumuomba Spika wa Bunge aje mbele na kutangaza matokeo ya nani atapeperusha Bendera. Kwa maelezo ya Dr Kikwete alisema kura hizo zilihesabiwa na Spika wa bunge Anna Makinda wakishirikiana na Spika wa Zanzibar bwana Kificho  na wengine aliwataja, Anna Makinda ndiye alipewa fursa na Mwenyekiti wa CCM kutangaza rasmi matokeo hayo. Anna makinda aliaza kwa furaha na bashasha huku akipiga vijembe upande wa pili Aidha alimsifia Rais JK kwa kukamirisha ukumbi wao wa CCM  na mambo mengine aliyoyafanya. Pia hakusita kuwapongeza wanawake waliojitokeza kuwania nafasi ya urais wa Tanzania kwa ticket ya ccm.Alisema" kwa wanawake kugombea nafasi ya juu haijawahi kutokea, lakini Awamu ya nne imetokea" Alitaja matokeo kama  ifuatavyo Jumla ya kura zilizopigwa ni 2422, zilizoharibika ni kura 6. Asha  Rose Migiro  alipata kura 59 sawa na 2.4% Amina Salumu alipata kura 253   sawa na  

HAYA NI MATOKEO RASMI DR JOHN POMBE MAGHUFULI AIBUKA KIDEDEA KWA ASILIMIA KUBWA.

SOMA HAPA Jumla ya kura zilizopigwa ni 2422, zilizoharibika ni kura 6. Asha  Rose Migiro  alipata kura 59 sawa na 2.4% Amina Salumu alipata kura 253   sawa na  10.5% Na Dr. John Pombe Maghufuli alipata kura 2104 sawa  87.1%  Huyu ndiye atakayepeperusha bendera ya CHAMA CHA MAPINDUZI.

TANO BORA YA CCM IMEZUA MASWALI MENGI JUU YA WALIOZUNGUMZA WANAZUONI KABLA YA MCHAKATO WA KUPATA TANO BORA

Image
HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUA NDANI YA CCM, Hii ndo tano bora ndani ya CCM Wahenga walisema "Lisemwalo lipo na kama halipo lipo linakuja" usemi huu umejidhihirisha wazi baada ya kamati kuu kutoa tano bora. Kulikuwa na minong'ono ya mda mrefu kuwa Mh Bernad  Membe ndiye atakayekuwa mrithi wa Mh Dr. J. M. Kikwete na sababu kuu iliyotelewa ni kwamba inasemekana wawili hawa ni ndugu wa damu japo Mh Bernard  Membe alikanusha undugu wao hawa wawili na hakika halijathibitishwa kisayansi kama ni ndugu au la? Sasa swali linajirudia je ni kweli huyu ni chagua la J. K Kama wachambuzi wa siasa walivyosema mwanzo na mara zote waliyasema hayo,?  tusubiri  Tatu bora tutajua kama nani ni nani?  ila akishinda ningetamani kipimo cha DNA kifanyike kwa uwazi kutotoa hofu ya kurithishana uongozi watu wa familia moja (ndugu wa damu) huku kuna watu makini zaidi Kwa upande mwingine ilisemekana kuwa Mh Lowassa hatafika tano bora na hili pia limetimia na sababu kuu ilikuwa ni magovi ka
Image
RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO AMEWATEUWA WASAIDIZI WAWILI Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua wasaidizi wake wawili. Uteuzi huo unaanza mara moja. Katika uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Bwana Jumaa George Bwando kuwa Mnikulu. Bwana Bwando ni mtumishi wa miaka mingi wa Serikali. Rais pia amemteua Bwana Martine Shigela kuwa Msaidizi wa Rais (siasa). Bwana Shigela anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Rajab Luhwavi ambaye karibuni aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara)
Image
MKAZI MMOJA ALALA JUU YA DARI KWAZAIDI YA MIEZI NANE MKOANI MTWARA Na Ernest Hyera MKAZI mmoja wa manispaa ya Mikindani mkoa mtwara amekuwa akilala juu ya dari kwa zaidi ya miezi nane sasa kutokana na nyumba yake kukumbwa na mafuriko kila mwaka. Pichani ni nyumba ambayo bi Zainabu anekuwa akilala juu ya dari ili kukwepa mafuriko kipindi cha mvua Akizungumnza na mwandishi wa blog hii Bi zainabu Musa Lipuga amesema toka mwaka jana mwezi wa kumi na moja amekuwa akilala juu ya dari kutokana na mvua iliyokuwa inanyesha na kubomoa sehemu ya chini ya nyumba anayoishi. Amesema hadi kufikia sasa hajamuona kiongozi yeyote waserikali ambaye ametoa msaada kwake zaidi ya vyama vya siasa vya upinzani ambao walifika na kumsaidia. Bi Zainabu amesema kwa sasa Chama Cha Wananchi CUF ndio walifika hapo na kumjengea chumba kimoja kilicho gharimu zaidi ya milion 2, kwa ajili ya kuishi kwamuda. Pichani ni ni ujenzi wachumba ambacho Cha Wananchi CUF wamemjengia bi Zainabu Kwa upande wa Ch

HALI BADO NI TETE KUMPATA MGOMBEA ATAKAYEPEPERUSHA BENDERA YA CCM

Image
Mapigo ya moyo yanakwenda kwa kasi sana ,si mchezo Habari kutoka mjini Dodoma baada ya  Nape Nnauye katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) kuongea na waandishi wa habari ,anasema vikao vyote vitakaa leo kuanzia SAA 4:00 Asubuhi ili kumpata atakayepeperusha bendera ya chama chao,aidha amesema baada ya kamati kuu kutoa tano bora majina yatepelekwa kwenye kamati ya mashauriano na taratibu nyingine zitafuata. Endelea kufuatilia kujua kinachojili huko

UKAWA INATAKA KUSHINDA AU KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU 2015?

Image
UKAWA inataka kushinda Uchaguzi au inataka Kushiriki Uchaguzi? Yericko Nyerere  Kushindwa kwa upinzani nchni kwa kiwango kikubwa katika chaguzi hizi kunatokana na muundo wa vyombo vya maamuzi ya uchaguzi wa nchi yetu, mathalani, Katiba, Tume. Kwasasa Katiba inasema kuwa matokeo ya urais hayatahojiwa na mtu yeyote ama chombo chochote wala mahali popote, hii inamaana kuwa Mwenyekiti wa Tume anayechaguliwa na Mwenyekiti wa CCM na anayelipwa na Mwenyekiti wa ccm akitangaza jina fulani hata kwa bahati mbaya tu baai haruhusiwi kurekebisha. Mwaka 2010 baada ya kushindwa uchaguzi mkuu, Upinzani chini ya Chadema uliituhumu sana tume Uchaguzi kwakuchakachua matokeo ambayo ilipoka ushindi wa 64% wa Dr Slaa malalamiko yao ndiyo yalipelekea kuwepo mchakato wa kuandika katiba mpya. Mchakato huo umeishia kwa zengwe la CCM kuvuruga maoni ya umma na kuweka maoni yao ambayo ni kinyume kabisa na matakwa ya umma, Maridhiano ya upinzani na msanii wa ccm baada ya dalili za uwepo finyu wa kati

Mh.KAFULILA AWALIPUA MAWAZIRI UFISADI MABEHEWA, ALITAKA BUNGE KUWAJIBISHA VIGOGO UFISADI WA MABEHEWA

Image
Na Shindo Kilawa Pichani ni Mh KAFULILA 

BENSON KIGAILA AONESHA UWEZO WA KIPEKEE KATIKA KUPAMBANUA MAMBO

Na Mhere Mwita Majira ya saa 2:30 Ndugu Benson Kigaila ambaye ni mkurugenzi wa organization ya CHADEMA ngazi ya Taifa na ni mtia nia ubunge jimbo la Dodoma mjini alifanikiwa kufanya mdahalo na wanachama ,baadhi ya viongozi na watia nia wa  Ubunge na Udiwani toka sehemu mbalimbali za nchi.Kijana haya alijidhihirisha kuwa anauwezo wa kipekee na ana kaliba ya kiuongozi kwa kujib maswali kwa ufasaha zaidi ya matarajio ya wengi. Uwezo wake ulitambulisha kuwa CHADEMA ina hazina kubwa ya viongozi tens waliomakini nitaweka baadhi ya maswali na majibu aliyoulizwa na wajumbe hao hapa chini:- swali 1:Kwanini umeamua kugombea ubunge? Majibu:Nimeamua kugombea ubunge kwa lengo la kusaidia kujenga jamii ya watu walio sawa mbele ya sharia,jamii guru na inayongozwa kwa haki na kuwatatulia kero zinazowakabili sasa ambazo waliopita hawajazitatua hadi leo kwa mfano Tatizo la Ardhi ya watu wa Dodoma dhidi ya CDA,ni tatizo kubwa linalohitaji mtu anayelijua na ana dhamira ya dhati kulitatua aliweka u

RAIS WA MAREKANI BARAKI OBAMA AKERWA NA MAUAJI YA WAMAREKANI WEUSI, AMESIKITISHWA SANA NA KITENDO HICHO CHA KIKATILI NA KIBAGUZI

Image
Rais wa Marekani (USA) Barak Obama amesema mauaji ya watu tisa ndani ya Kanisa Wamarekani Weusi katika eneo la Charleston, jimbo la Carolina Kusini yanaibua maswali mengi sana Aidha Mh Barak Obama amesema chuki miongoni mwa jamii kwa misingi ya rangi na imani ni kitisho kwa demokrasia ya Marekani amelaani vikali kitendo hicho na vitendo vingine vinavyoweza kuhatarisha umoja wao, ameyasema hayo mda mfupi baada ya kijana wa kizungu aliyehusika kufanya mauaji hayo ya watu tisa kukamatwa. Pia ametaka kufanyika kwa mabadiliko ya pamoja katika fikra za Wamarekani kuhusu ghasia zinazosababishwa na matumizi ya silaha.

KAFULILA: JK KAVUNJA MISINGI YA UCHUMI ALOWEKA MKAPA.

Image
Na Mh Kafulila Huu ndio mchango wangu bungeni jioni leo.Mkapa aliweka misingi ya uchumi mkuu( macro economics) kilichopaswa kufanywa na JK ni kuhakikisha mafanikio hayo yanajitokeza kwenye uchumi wa kawaida ili kila mtanzania aone fahari ya kukua kwa uchumi wake lakn bahati mbaya amebomoa kabisa na sasa inabidi UKAWA tuanze upya baada ya uchaguzi Oct. 1. Mkapa amepokea nchi mwaka 1995  ukuaji wa uchumi ukiwa 4.2 akakuza mpaka 6.7 mwaka 2004. Leo JK kashusha uchumi mpaka 6.4 mwaka 2014. 2. Amepokea nchi riba ya mabenki ikiwa 30-26% mwaka 1995 lakn mwaka 2005 riba za mabenki ilishuka hadi 14% lakn leo JK riba zimepanda mpaka 18%. Hii inathiri sana ukuaji wa sekta binafsi na biashara nchini. 3.Mwaka 1995 mfumko wa bei ulikuwa 21% lakn mwaka 2005 mfumko ulishuka mpaka 4%. Leo JK mfumko wa bei ni 5.3% .  4. Mkapa kapewa nchi mwaka 1995 akiba ya fedha za kigeni zikiwa za miezi 2 lakn mwaka 2005 akiba ilikuwa ya miezi 8 lakn leo mwaka 2015 akiba za pesa za kigeni zinato

HEKAHEKA ZA WANAVYUO NA NEC KUHUSU KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

Image
Na Alex Elifurah Kweli vyuo vikuu tukinyamaza na kutokupiga kura October 2015,itabidi tupimwe akili au tupewe chanjo ya Akili, Kuelekea October  hii chanjo ni muhimu sana. waraka wa vyuo vikuu kuomba hatma yao kuelekea uchaguzi mkuu umewasili kwa Jaji Lubuva,Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguzi, na tumefanya NAE mazungumzo ya pamoja na ametupa mrejesho kwa maandishi. Lazima  vyuo vikuu vijiandae kisaikolojia kupoteza haki yao ya msingi ya kupiga kura kwani majibu ya waraka ule una mapungufu mengi sana. Mahojiano kati yetu na mwenyekiti wa  Tume ya uchaguzi kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari moja kwa moja amedai zoezi limefeli hivyo ni mapungufu yao. Maamuzi yetu ni kufungua shauri mahakamani na kupeleka waraka kwa tume ya haki za binadamu baadaya ya Tar 18. August 2015 ambayo ni mwisho ya kuboresha na kuhamisha Taarifa kwa wapiga kura. Pia kutokana na  rekodi za utendaji mbovu wa tume kwanzia kura za maoni ya katiba,uandikishaji na ukusanyaji wa  taarifa k

Mh. KAFULILA AFUNGUKA KUHUSU ZITTO& ESCROW

Image
Na Shindo Kilawa Pichani ni Mh David Kafulila Mbunge (NCCR MAGEUZI)  wa kiwa na mke wake Kamanda Jesca Kishoa Kutoka Singida baada ya kupokea zawadi.  Leo asubuhi katika kundi la watsap la IPTL BRING BACK OUR MONEY(IBBOM) liloundwa kipindi cha sakata la Escrow na vijana wapambanaji. Mh Kafulila alipohojiwa na vijana hao ndani ya kundi hilo juu ya Zitto Zuberi Kabwe kama alimsaidia katika kampeni za mwaka 2010 jimboni kwake, kama wanavyosema wapambe wa ZZK. Mh Kafulila akaamua kufunguka, namnukuu "Naomba kuweka kumbukumbu sawa tu kwamba Zitto ni rafiki yangu tangu nikiwa chadema lakini haimanishi tunakubaliana kila kitu. Naudhika kuona wafuasi wake wakiandika uongo ambao hata yeye mwenyewe zitto anajua ni uongo kwamba alinisaidia kwenye kampeni" Akaendelea kwa kusema "Ukweli wa Mungu zitto hakunisaidia hata lita ya mafuta kwenye kampeni kwasababu anazojua yeye ambazo nisingependa kumsemea. Aliahidi tu kwenye magazeti. Labda wafuasi wake wamrudie kumuuliza vizur

PERUZI MAGAZETI YA LEO Tr 18/06/2015

Image

CCM WANAPENDA NAMBA LAKINI HAWAJUI HESABU.!

Image
Na Malisa GJ, Leo tuongee uchumi kidogo. Kuna watu wanapenda namba lakini hawajui hesabu. Kama na wewe ni mmoja wao tafadhali usisome makala hii. Wabunge wengi na mawaziri wa chama cha mapinduzi ni wagonjwa wa namba. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu. Ukitaka wakushangilie we ongeza tarakimu tu kwenye namba. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu.! Kama ulikua unamlipa mtumishi mshahara wa laki 5 mwaka jana mwaka huu mlipe laki 7. Atashangilia na kukushukuru. Kumbe hajui upande wa pili gharama za maisha zimeifanya hiyo laki 7 iwe sawa na laki moja ya mwaka jana. Yeye atakushukuru tu, kwa sababu anapenda namba lakini hajui hesabu.! Naona wengi hamjanielewa. Ni hivi kuna faida gani kulipwa mshahara wa milioni mbili halafu ukauziwa sukari kilo moja sh.3000/=??? Si bora ulipwe laki 5 sukari uuziwe sh.500/= kwa kilo. Kama unapenda namba lakini hujui hesabu huwezi kunielewa. Twende kwenye historia kidogo. Mwaka 2005 wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani bajeti ya serikali

PERUZI MAGAZETI HAPA KILA SIKU

Image

HATIMAYE JIMBO LA RUNGWE MASHARIKI LAPATA MKOMBOZI WAO ATAKAYEWATETEA.

Image
Dr Elias akiwa katika mkutano na wananchi  wa kata ya Isange.  Pichani ni Dr Elias akiwahutubia wananchi wa kata ya Isange.  Dr Elias akiwa na wananchi wa kata ya Lutabe jimboni kwake Rungwe mashariki, nyumba kwa nyumba, shamba kwa shamba operation aliyoifanya kwa mienzi zaidi ya miwili hadi sasa anaendelea na operation hii ili kuwakombowa wakazi wa RUNGWE Hakika penye nia pana njia,jimbo la Rungwe mashariki liliongozwa kwa mda mrefu na mh Prof. Mark Mwandosya lakini hakuweza kuwasemea wananchi matatizo yao bungeni kwa mda mrefu, sijui kwakuwa alikuwa ni Waziri japo sio sababu ya kushindwa kuwasemea wananchi wa jimbo lake. Inasemekana Mh Mwandosya  kashindwa kabisa kuwatetea wakulima wa chai huku akijua kabisa chai ni zao muhimu la biashara kwa wakazi wa Rungwe, lakini hadi sasa wanauza kwa bei ya hasara sana kwa kilo. Lakini pia kama  mbunge hajafanya jitihada za kufufua na kuboresha kiwanda cha chai kilichoko Mwakaleli, hivyo kuwanyima fursa za ajira wakazi wa Bus

OMBWE LA AJALI ZA BARABARANI LAIBUKA TENA MKOANI IRINGA

Image
Ni muonekano wa gari ubavuni baada ya kupata ajali eneo hilo la kinyanambo, Mafinga Kama unavyoona katika picha hizi, hivi ndivyo gari lilivyosambaratishwa baada ya ajali iliyoleta maumivu makali na kuacha majuzi kwa taifa letu. Pichani ni Muonekano wa Gari aina ya Coaster la Another G baada ya kupata ajali eneo hilo la Kinyanambo, nje kidogo ya mji wa Mafinga wilayani Mfindi Katika ajali iliyotokea usiku wa jana japo eneo la Kinyanambo,Mafinga wilayani Mfindi katika barabara kuu nje kidogo ya Mji wa Mafinga.  Imeripotiwa Kuwa watu 23 wamepoteza maisha na wengine 34 kujeruhiwa vibaya. Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema gari aina  ya costa mali ya Another G inayofanya  safari  zake kati ya mikoa ya Iringa na Njombe ilikuwa ikitokea Iringa mjini kuelekea Njombe iligongana na lori la mizigo na kusababisha maafa hayo. Aidha Mkuu  wa wilaya ya  Mufindi Miss.  Mboni Mhita amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo  na  kueleza kuwa hii ni miongoni mwa ajali  mbaya ku

SHEIKH MKUU MUFTI ISSA BIN SHAABAN SIMBA AFARIKI DUNIA

Image
Mufti, Shekh mkuu  Tanzania Issa Bin Shaabani Simba enzi za Uhai wake.  Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Issa Bin Shaaban Simba amefariki asubuhi ya kuamkia leo majira ya saa nne kasorobo., Inasemekana kaaga dunia katika hospitali ya TMJ jijini Dar es salaamu alikokuwa akipatiwa matibabu. Huu ni msiba mkubwa kwa watanzania wote kwani alikuwa ni nguzo kubwa katika kudumisha amani ya nchi yetu. Mwenyenzi Mungu ailaze mahala pema roho ya Marehemu Sheikh Mkuu, Mufti Issa Bin Shaabani Simba. Na awape nguvu waislamu wote nchini Tanzania na ulimwengu mzima kwa kufikwa na msiba huu wa kuondokewa na kiongozi wao mkuu. R. I. P

UKISTAAJABU YA WANAWAKE WA ROMBO UTAYAONA YA WIZARA YA UCHUKUZI NA STESHENI YA RELI MOSHI MJINI.

Image
Na Mwl. Denis Bongole Hili ni Daraja la Tsavo nchini kenya, ujenzi wa mradi huu unaendelea hadi sasa Hapa ni Stesheni ya Gari moshi iliyopo mkoani Kilimanjaro, Moshi Wiki chache zilizopita gazeti la mwananchi linalomilikiwa na kampuni ya Mwananchi communication limited lilimnukuu mkuu wa wilaya ya rombo akisema kua eti "wanawake wa rombo wanakodi wanaume wakenya kutoa huduma za kindoa" Binafsi sikuona ajabu sana ila nilitafsiri kama 'vita ya kisiasa' dhidi ya mbunge aliepo sasa ndugu Joseph Selasini. Nilipata kuandika hapa juu ya hili hivyo leo nataka tuunganishe matukio katika sakata la aina yake ndani ya wizara ya uchukuzi. Majuzi hapa Raisi wa Kenya bwana Uhuru Kenyata aliandika katika ukurasa wake wa facebook kuhusu safari yake na mawaziri kadhaa ambapo walionekana katika picha wakiwa wametembelea "daraja la tsavo" kukagua ujenzi wa reli ya kisasa kabisa nchini humo. Cha ajabu zaidi ni mwaka mmoja tu toka achaguliwe ambapo pamoja na misu