TANO BORA YA CCM IMEZUA MASWALI MENGI JUU YA WALIOZUNGUMZA WANAZUONI KABLA YA MCHAKATO WA KUPATA TANO BORA
HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUA NDANI YA CCM,
Wahenga walisema "Lisemwalo lipo na kama halipo lipo linakuja" usemi huu umejidhihirisha wazi baada ya kamati kuu kutoa tano bora.
Kulikuwa na minong'ono ya mda mrefu kuwa Mh Bernad Membe ndiye atakayekuwa mrithi wa Mh Dr. J. M. Kikwete na sababu kuu iliyotelewa ni kwamba inasemekana wawili hawa ni ndugu wa damu japo Mh Bernard Membe alikanusha undugu wao hawa wawili na hakika halijathibitishwa kisayansi kama ni ndugu au la? Sasa swali linajirudia je ni kweli huyu ni chagua la J. K Kama wachambuzi wa siasa walivyosema mwanzo na mara zote waliyasema hayo,? tusubiri Tatu bora tutajua kama nani ni nani? ila akishinda ningetamani kipimo cha DNA kifanyike kwa uwazi kutotoa hofu ya kurithishana uongozi watu wa familia moja (ndugu wa damu) huku kuna watu makini zaidi
Kwa upande mwingine ilisemekana kuwa Mh Lowassa hatafika tano bora na hili pia limetimia na sababu kuu ilikuwa ni magovi kati ya Mkuu wa nchi na nguli huyu wa mazingaombwe. Japo wawili hawa walikana kabisa na kudai wao hawana uadui bali hata kidogo lakini kamati kuu haijasita kuusema ukweli kwa kumtupilia mbali.
Lakini pia ilidaiwa kuwa mh J. K alimrudisha Asha Rose migiro na kumuahidi atamfanya kuwa mmoja wa viongozi wakubwa ndani ya serikali yake ya CCM, katika haya yaliyosemwa yaliaza kutimia toka mwanzo hadi sasa kwani kada huyu hajawahi kutupwa kamwe toka amerudi.
Na mwisho wachambuzi wa siasa walisema kwamba Zanzibar katika muungano wana nafasi ndogo sana ya kumtoa mrithi wa Kikwete japo uvumi ulisambaa kuonesha kuwa jaji Ramadhani ndie atakayemrithi Kikwete, jambo hilo limejitokeza kwa utofauti kabisa, tumeweza kuona aliyefanikiwa kuingia ni Bi Balozi Amina tu huku Bilali na Ramadhani pamoja na uwezo wao makini wakitupwa kule. Pia ukichunguza kwa makini wote waliopitishwa hawawezi kuwa na uwezo kama akina Dr Mahige, Prof. Mark Mwandosya, Dr Mwakyembe. Ukiangalia kwa makini ni Bora hata Mwigulu Nchemba kuliko waliopita kwa moono ya mbali, Ni mtizamo wangu unaruhusiwa kunibeza kwa hoja sio matusi.
Msishangae hii ndo CCM watenda haki kwa maneno na si kw vitendo.
Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu daima.
Shindo Isaac Kilawa
Hii ndo tano bora ndani ya CCM

Comments
Post a Comment