TATIZO LABDA NI MWALIMU NYERERE NA CCM YAKE.
Na Mwl Bongole
Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu
Yapo mambo muhimu mengi na muhimu sana yanayopaswa kuzingatiwa na kuangalia kama kweli leo hii tunahitaji kukomesha ufisadi rushwa kuongeza fursa za ajira na kutoa huduma za jamii kwa kiwango ambacho kinaweza kukidhi haja ya watanzania.
Ili kufikia mabadiliko ya kimfumo ambayo kiuhalisia chanzo chake ni kupoteza dira kwa chama cha mapinduzi basi tunahitaji mtu imara, jasiri, mwelewa, mwenye malengo na uzoefu wa kubadilisha mifumo iliyomibovu na kuleta mfumo mzuri.
Kwa hapa tulipofikia ni vigumu sana yeyote ndani ya ccm kufumua mfumo uliozeeka wa kifisadi kibaguzi kandamizi na usiopenda mabadiliko. Mfumo uliopo ndani ya ccm umejikita katika kuangalia kulinda na kutetea CHAMA KWANZA huku vipaumbele kama afya elimu na aina zote za huduma za jamii zikiwa duni.
Ni mfumo wa kutizama maslahi ya vyombo vya ulinzi kama vile Polisi kwa kuwekeza nguvu kubwa huko ili kuendelea kulitumia katika kufanikisha maslahi yake.
Si jambo la ajabu kuona magari lukuki ya polisi yakiagizwa lakini ni mara chache kuona magari ya kubebea wagonjwa yakiagizwa kwa ajili ya kutoa huduma muhimu kwa taifa linalojinasibu kua taifa la amani.
Napenda kuhimiza zaidi kua kwa kua CCM haina mpango wa kuibadili mifumo yao kandamizi, wakati ndio huu. Tunaye DR WILBROAD SLAA kiongozi makini mwenye sifa lukuki za kiutendaji. Ni kiongozi wa pekee barani africa mwenye uwezo wa kuitumia taasisi anayoiongoza na kuhudumu kwa maslahi ya wategemezi wa taasisi husika.
Ni kiongozi pekee barani africa ambaye anaamini katika matumizi bora ya rasilimali za kila aina katika kupata mawazo mapya ambayo yana maslahi kwa nchi yake.
Kwa muda sasa amesimamia taasisi isiyo ya kisiasa CCBRT na kufikia malengo yake kwa zaidi ya asilimia 89 katika harakati za kutokomeza magonjwa ya uzazi n.k
Amekisimamia chama chake katika kufanya mabadiliko ndani ya chama na hatimaye chama muhimu cha siasa chenye viongozi makini na tegemeo kubwa hapa Tanzania.
Kiongozi huyu amejaaliwa safu ya wasaidizi vijana wenye mawazo chanya na yenye mrengo wa kimapinduzi hasa kwa taifa hili lenye rasilimali lukuki na uchumi mbovu.
Kwa kua tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu kama tumedhamiria kuibadili mifumo kandamizi basi ipo haja ya kuepuka mambo kadhaa.
Moja; tuepuke tabia ya kutumia mfumo ule ule unaosimamiwa na watu wale wale alafu eti tutarajie matokeo tofauti. HAIWEZEKANI.
Mbili; tuepuke "ukale" kwa namna nyingine tuepuke uzamani wa kuamini kua upinzani ama kutokuichagua ccm basi mambo hayawezekani. Wakati huo umepikwa na wakati. Kizazi hiki hakiitaji watu waliokua ndani ya CCM miaka nenda rudi na bado wakashindwa kufanya mambo ambayo wanakuja leo kutuahidi.
Kwangu mimi
Dr WILBROAD PETER SLAA anaweza. Anavijana ambao wakisimama kama mawaziri na makatibu watatupeleka katika hatua njema ya maendeleo hata kama ni kwa miaka mitano pekee.

Comments
Post a Comment