HAKUNA MATARAJIO MAPYA KWENYE MFUMO ULE ULE
Na Musa Makongoro
Tayari chama cha mapinduzi kimempata, mgombea urais wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa njia za mizengwe na kupelekea mpasuko ndani ya chama hicho kuonekana hadharani.
Mgombea huyu ni Dr John Pombe Maghufuli, ambaye ni waziri wa ujenzi wa serikali inayoondoka madarakani. Ni kama vile watanzania wengi, wanakubali kwamba huyu ndiye anaeweza kuirudisha nchi pale ilipokuwa na kwamba atakidhi matarajio yao.
Pamoja na umahili wake wa kukariri takwimu mbalimbali, kitendo kilichomjengea umaarufu miongoni mwa watanzania wengi wasiofuatilia mambo, John Pombe Magufuri ataingia kusimamia mfumo ule ule.
Tumesahau kwamba ni Magufuri huyuhuyu, ameshiriki kupitisha sheria mbovu kabisa na zenye maslahi binafsi ya baadhi ya wana CCM bungeni. Wakati bunge maalumu la katiba likiizika rasimu ya jaji waryoba, iliyokuwa imesheni maoni ya wananchi alikuwamo bungeni na hakuonyesha nia yoyote ya kutetea wananchi wa Tanzania.
Rundo la kashfa zikiwemo za upotevu wa mabilioni ya fedha za umma katika wizara yake, na uuzwaji wa nyumba za serikali kwa swahiba zake ni namna ile ile ya kuhalalisha wizi na ufisadi.
Ripoti ya CAG ya mwaka huu, ilionyesha kwamba wizara anayoiongoza Bw. John Pombe Magufuri imefanya ubadhilifu wa zaidi ya shilingi bilioni 200. Kwa mujibu wa ripoti ya CAG, fedha zilitengwa na wizara yake kama fedha za kujengea barabara lakini baadae zilionekana ni barabara hewa. Haya yote ni masuala ya kujiuliza kuhusu mifumo inavyowanufaisha viongozi wala rushwa.
Makamu wake Samia Hassan Salumu, alikuwa ni makamu mwenyekiti wa bunge maalumu la katiba, ambalo kimsingi liliyazika maoni ya wananchi kwa kuikataa kwa kiasi kikubwa rasimu ya tume ya mabadiliko ya katiba,iliyokuwa chini ya jaji mstaafu Joseph Sinde Waryoba. Unategemea kwamba akiingia madarakani atayakana aliyaofanya kama kuzika maoni ya wananchi kwenye rasimu ya katiba?
Tunapaswa kufahamu kwamba tatizo kubwa la Tanzania ni MABADILIKO YA KIMFUMO, tunahitaji kuusuka upya mfumo wa nchi yetu ili kurudisha usawa kwa wananchi wote. Ukweli ni kwamba hata siku moja mtu yuleyule, kwa mfumo ule ule hajawahi kuubadili mfumo uliomnufaisha kwa namna moja au nyingine.
Ni ndoto kusema Magufuri au mtu yoyote katika mfumo ule ule uliokubuhu kuiba, kunyanyasa kukumbatia wezi na wakwepa kodi, na kutesa wananchi wake, kwamba atakuletea mabadiliko. HAIJAWAHI KUTOKEA LABDA KAMA ATAKUWA MSALITI kwa wenzake wanaofaidika na mfumo huo.
Katika namna ya kipekee kabisa, tunahitaji mtu mwenye nia ya kweli asiye na namna yoyote ya kutiliwa mashaka katika utumishi wake wa umma, mtu aliyeapa kuwashughulikia wezi na mafisadi sio kuwalinda.
Watu wenye usahaulifu tu ndiyo wanaweza kufikiria kwamba Magufuri katika mfumo ule ule wa kukandamiza wananchi ndo wanaweza kuleta mabadiliko katika nchi yetu. Hakuna ubishi kwamba, huyu atakuwa ni kwa ajili ya maslahi ya CCM. Atakuwa ni mlinzi wa maswahiba wa serikali inayoondoka madarakani ikiwa na kashfa nzito zilizotikisa nchi na kuiacha ikiwa na matobo.
Katika hali ambayo nchi yetu imefikia tunahitaji kuwa na mbadala wa uongozi, tunahitaji kuisuka mifumo yetu upya, tunataka mtu ambaye ataponya fikra za watanzania na kuuonyesha ulimwengu kwamba,katika nchi yoyote duniani, hapana maendeleo bila kuwabadilisha wananchi fikra zao.
Katika namna ambayo nchi yetu imefikia hatuhitaji mtu ambaye atasafishwa ili awe kiongozi wetu, huu ni wakati wa kupiga kura za maamuzi sahihi.
MASWALI:
Je, Magufuri anaweza kuwakamata swahiba wa Kikwete na kuwafunga kwa ubadhilifu wa mali ya umma? CCM imesheheni wala rushwa wakubwa na matajiri wakubwa ambao ni marafikki wa serikali inayoondoka madarakani, sasa Magufuri yuko tayari kuwatupa mbali na kuongoza nchi bila kukumbatia wafanyabiashara?. Je, Magufuri yupo tayari kuzifumua sheria zote kandamizi kwa maslahi ya taifa, zikiwemo ile ya mafuta na gesi, sheria ya uwekezaji ambayo inatoa mwanya kwa wafanyabiashara kukwepa kodi, sheria ya madini na nishati?
MakongoroJr.(tweeter: @macksabi)

Comments
Post a Comment