MKAZI MMOJA ALALA JUU YA DARI KWAZAIDI YA MIEZI NANE MKOANI MTWARA

Na Ernest Hyera

MKAZI mmoja wa manispaa ya Mikindani mkoa mtwara amekuwa akilala juu ya dari kwa zaidi ya miezi nane sasa kutokana na nyumba yake kukumbwa na mafuriko kila mwaka.

Pichani ni nyumba ambayo bi Zainabu anekuwa akilala juu ya dari ili kukwepa mafuriko kipindi cha mvua

Akizungumnza na mwandishi wa blog hii Bi zainabu Musa Lipuga amesema toka mwaka jana mwezi wa kumi na moja amekuwa akilala juu ya dari kutokana na mvua iliyokuwa inanyesha na kubomoa sehemu ya chini ya nyumba anayoishi.

Amesema hadi kufikia sasa hajamuona kiongozi yeyote waserikali ambaye ametoa msaada kwake zaidi ya vyama vya siasa vya upinzani ambao walifika na kumsaidia.

Bi Zainabu amesema kwa sasa Chama Cha Wananchi CUF ndio walifika hapo na kumjengea chumba kimoja kilicho gharimu zaidi ya milion 2, kwa ajili ya kuishi kwamuda.

Pichani ni ni ujenzi wachumba ambacho Cha Wananchi CUF wamemjengia bi Zainabu

Kwa upande wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kupitia kwa mwenyekiti wake Ibrahim Mandoa wamempa Bi Zainabu vitu mbalimbali kwajili ya matumizi ya nyumbani

Mwandishi wa Blog hii alifanikiwa kuwasiliana na mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bi Fatma ally nakuthibitisha kuwa anamfahamu Zainabu Lipuga na swala lake lilishafika ofisini kwake na akamkabidhi afisa tarafa alishughulikie.

Mwandishi wetu alipomtafuta Afisa tarafa hakufanikiwa kumpata kwani alikuwa kwenye majukumu ya mengine ya kitaifa


Nyumba ya Bi Zainabu

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI