MALEZI YA MTOTO, DEMOKRASIA NA HATIMA YA MAENDELEO YA NCHI YETU.

Na Dr. Elias Mwakapimba


Katika malezi ya mtoto kuna vitu vingi ambavyo vinaathiri afya kwa ukuaji mzuri. Vitu hivi ni elemu/uelewa wa mzazi, uwezo wao wa kiuchumi/kipato na mazingira wanamoishi. Haya mambo ni nguzo muhimu katika kuimarisha afya thabiti kwa ukuaji na mafanikio ya mtoto baadaye.

Wazazi wa mtoto wanaweza kuwa na elimu/uelewa wa kulea mtoto lakini hawana uwezo wa kumudu mahitaji kwa afya njema ya mtoto. Wanaweza wakawa na kipato kizuri lakini wasiwe na elimu/uelewa wa namna ya kuanda lishe nzuri ya mtoto.

Au wanaweza wakawa navyo vyote lakini mazingira yasiwe rafiki katika kuandaa lishe ambayo ni muhimu kwa afya ya mtoto (mfano vita/ukimbizi) au wakaweza kuandaa lishe lakini mazingira tena yasiwe rafiki kuruhusu mtoto kufaidi virutubisho vya lishe na asiweze kukua katika afya (mfano magonjwa).

Katika makundi mawili ya awali: ukosefu wa elimu au kipato, au ukosefu wa vyote au uwepo wa vyote lakini mazingira yasiwe rafiki hupelekea mtoto kuwa na utapia mlo (mtoto kudumaa). Katika kukosa elimu/uelewa au kipato lengo kwa walezi litabakia moja tu, nalo ni kiasi na sio ubora wa chakula kutosheleza mahitaji muhimu ya mtoto. Basi inakuwa ni kuandaa chakula cha aina moja, km ni ugali basi ugali na maharage, km ni ndizi basi ni ndizi na parachichi, kama ni muhogo basi ni muhogo na kisamvu.

Matamanio yao yanabaki kuona tumbo la mtoto limevimba: linakuwa kubwa ishara ya kushiba. Mara ingine hadi mtoto atapumua kwa shida. Kwamba sasa wanataka tu kuona mtoto ameshiba na sio chakula cha aina gani kimeenda tumboni-ni vita ya kiasi dhidi ya ubora (quantity against quality).

Hivyo kila leo watahangaika huku na kule ili wajaze tumbo la mtoto, na mtoto anakula. Tumbo likivimba wanashangilia mtoto amekula. Kwa sababu ya kuamini ktk kiasi na sio ubora, mtoto anadumaa-hakui. Atavimba tu tumbo na kuanza kushambuliwa na magonjwa, mara hii tumbo halivimbi baada ya kupokea chakula bali litavimba wakati wote-wa njaa na wa shibe.

Mtoto anaanza kuumwa, kikohozi, kuharisha, mara vidonda. Hayo ndio madhara ya kuamini ktk kiasi kuliko ubora, kudumaa kwa mtoto na hatimaye magonjwa. Na hali itabaki hivyo hadi pale wazazi/walezi watakapowezeshwa kwa mawazo mbadala juu ya njia bora za malezi, mara nyingi nguvu itatoka nje na wazazi/walezi.

 Demokrasia na maendeleo ya taifa. Demokrasia ni ulimwengu ambao ni sawa na malezi ya mtoto, wakati demokrasia inatambua umuhimu wa kiasi/idadi ya watu katika kutoa maamuzi juu ya kiongozi wanaemtaka, lakini demokrasia ni ulimwengu mbaya, kwa msingi wa idadi/wingi katika kufikia maamuzi ya zipi njia sahihi kwa maendeleo ya taifa.

Taifa letu (mtoto) limedumaa kwa sababu ya kuamini katika idadi/kiasi kuliko ubora wa hoja/chakula. Bungeni tumeshuhudia 'quantity of opinion' ina nguvu kuliko 'quality of opinion'. Matokeo yake taifa limezidi kudumaa, taifa la Tanzania lina utapiamlo; haliendelei.

Wabunge wa CCM wamekuwa km wazazi wasio na elimu/uelewa na pia km wazazi wasio na kipato badala yake wameamini ktk kiasi cha chakula (idadi ya wanaounga mkono hoja) na wameweka kama ndio msingi wa ukuaji/maendeleo ya mtoto (maendeleo ya nchi) na sio ubora wa hoja zinazosanifu kila aina ya virutubisho muhimu kwa maendeleo ya nchi. Matokeo yake nchi yetu inadumaa (utapiamlo) huku tumbo (deni la taifa) linazidi kuwa kubwa na hatimaye kukumbwa na magonjwa yatokanayo na utapiamlo: mfano migomo ya kila kundi la jamii.

Ubovu wa huduma za afya, elimu duni na umaskini wa watanzania ni matokeo ya kuamini ktk wingi wa hoja kuliko ubora wa hoja (quantity of opinion against quality of opinion) km zitolewazo na wapinzani. Hv karibuni tayari wamebuni aina mpya ya chakula kwa njia ya sheria tatu zilizopitishwa hovyo hovyo, na kwa sababu zimekosa virutubisho tutarajie nchi yetu kudumaa zaidi na kupata magonjwa zaidi. By Dr Elly

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI