SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI

KWANINI WASOMI WENGI NI MASIKINI NA WANAISHI MAISHA MAGUMU?
Ukichunguza katika jamii zetu, utabaini kuwa
sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana
elimu ndogo ama hawakusoma kabisa. Katika
miji na maeneo yote; wenye majengo ya
maana, wenye makampuni makubwa, wenye
utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka
makubwa ni wale wa "darasa la saba B", ama
ambao hawakuingia kabisa darasani.

Wasomi wengi wana maisha ya kawaida (yaani yale ya
kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi
sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi na
magari ya kutembelea baaasi tena kwa
mikopo!). Na tena wapo wasomi wengi tu
wanaoishi kimasikini (kistaarabu tunaita wana
maisha ya kuungaunga). Kiukweli idadi ya
wasomi walio matajiri ni ndogo sana. Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga.

Mosi; wameelezwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli.Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio. Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa! Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee (kwa sababu ndio ina uhakika).

Pili; madarasani kunahimizwa ubinafsi lbadala ya umoja. Utaniuliza nimejuaje? Jibu lipo!
Angalia namna mitihani inavyofanyika; ni
sheria kwamba kila mwanafunzi afanye mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama
mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani! Katika maisha ya kawaida(hasa ya kusaka fedha), unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja,wafanyakazi n.k. Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani! Simaanishi kusoma hakuna maana (hata mimi nimesoma nina digrii na vyeti vya kozi za kumwaga) isipokuwa ninakwambia hivi: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani. Mtaani panahitaji akili ambayo ni
tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia hayo
makaratasi wanayokuzawadia yaitwayo vyeti.
Ukitaka kutajirika usiulete "u-smart" wa
darasani huku mtaani!
Tuyajue hayo kupitia kwa wataalamu waliogundua haya......... Ahsante

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA