MUOGOPENI BAHATI BUKUKU


MUOGOPENI BAHATI BUKUKU.!

Na Malisa Godlisten
             Msanii wa nyimbo za injili aliyeona ni bora aimbe nyimbo za kumsifu EDWARD LOWASSA,ama kweli makanisa yameingiliwa na watu wa mataifa. Yy 


Nimesikitika sana kuusikia wimbo wa Bahati Bukuku aliomuimbia Lowassa na kumpamba kuhusu mbio zake za Urais. Sina tatizo la Lowassa kutafuta Urais maana ni haki yake kikatiba. Ana haki ya kugombea, kupigiwa kura na hata kushinda. Ila nina tatizo na Bukuku aliyeamua kuacha kumuimbia Mungu na kumtukuza mwanadamu.
Nimeainisha makosa 10 ya Bahati Bukuku yanayohusiana na wimbo huo;
1. Bukuku anasema Lowassa atatawala kwa amani na ubora ambao Rais yoyote hataweza kufikia. Hapa kuna makosa mawili. La kwanza ni kusema atatawala.
Nani kamhakikishia Bukuku kuwa Lowassa atatawala? Hivi Bukuku anajua kuwa jina la Lowassa linaweza kupelekwa NEC na lisirudi? Au likarudi halafu wananchi wakamkataa? Sasa yeye anajihakikishiaje kuwa Lowassa atatawala?
2. Pili kasema Lowassa ataongoza kwa ufanisi kuliko wote waliomtangulia na watakaomfuatia. Huu ni ujuha wa kiwango cha "PhD". Hivi unawezaje kupima uwezo wa mtu kabla hajafanya kazi? Ni sawa na kununua nguo za mtoto wa kiume kisa mkeo akiwa na mimba alipenda kula sana ugali, mwishowe anazaliwa wa kike..!
3. Bukuku anasema Lowassa ana hekima kama Suleimani. Hii ni kufuru kubwa kwa Mungu. Maandiko yanasema hakuwahi kutokea mtu mwenye hekima kama Suleimani na hatatokea. Sasa Bukuku kamtoa wapi Lowassa? Ina maana Bukuku ana akili kuliko Mungu aliyeruhusu maandiko hayo?
4. Bukuku anasema Lowassa amepakwa mafuta kama Daudi. Maandiko yanasema Daudi alikuwa Mteule wa Mungu na alipakwa mafuta na Kuhani mkuu Samuel. Kujaribu kumfananisha Lowassa na Daudi ni makosa makubwa. Ni Kuhani gani amempaka mafuta Lowassa? Labda Kuhani Yusuph Makamba.. Na alimpaka mafuta gani? Ya Alizeti au Baby Care.!
5. Si sahihi kwa mtumishi wa kiroho kumfanyia kampeni mgombea waziwazi. Either ni Mchungaji, Padri, Askofu, Sheikh, Ustaadh etc sio sahihi kumsifia mgombea hadharani. Kama unampenda mgombe ibaki moyoni mwako na ufanye maamuzi mwenyewe bila kushawishi wengine.
6. Kumpigia debe mgombea ni kuwagawa waumini. Kuna wafuasi wa Bahati Bukuku hawamkubali Lowassa, sasa haoni anawakwaza?
7. Pia Kuna wafuasi wa Lowassa si Wakristo. Wengine ni waislamu na wengine hawana dini. Sasa Bukuku haoni anawakwaza kwa wimbo wake?
8. Wimbo huu unaibua chuki za kidini na kuonekana Lowassa yupo kwa ajili ya wakristo tu. Kama Lowassa anawapenda pia Waislamu mbona hatujasikia akiimbiwa "Kaswida"? Kumuimbia "mapambio" tu ni ishara ya kuwatenga waislamu na kuwaonesha kuwa Lowassa si mtu wao.
9. Wimbo huu unajenga ushawishi upande mmoja tu wa wakristo. Mbona Waislamu hawakuguswa na wimbo huu? Hivi unawezaje kumshawishi Muumini safi wa kiislamu amkubali Lowassa kwa kusikiliza Pambio??
10. Wimbo huu umemfanya Bukuku kuonekana "Changudoa wa kiroho". Hawezi kuwacheka wanawake wanaouza miili yao kwa fedha, maana na yeye kauza utu wake wa kiroho kwa tamaa ya fedha na mali za dunia.
NB: Kwa ujumla Bukuku amejipunguzia sana heshima yake mbele ya jamii. Waislamu wamemuona ni mdini, wakristo tumemuona mnafiki. Wapo wakristo kadhaa waliojiapiza kutonunua tena kazi zake kutokana na upuuzi alioufanya.
Najua njaa ya pesa ndiyo imemfanya akaamua kuwa vuvuzela la Lowassa. Lakini kwa heshima kubwa aliyokua ameijenga kwenye jamii ni bora asingefanya hiyo kazi. Bora angekubali kukosa hizo hela kuliko upuuzi alioufanya. Njaa ya siku moja haiuwi.
Pesa alizozipata atazitumia na zitaisha lakini doa alilojiwekea halitatoka hata siku anaingia kaburini.
Muasisi wa taaluma ya Public Relations, Arthur Page aliwahi kusema "You may need 20 years to build your reputation, but it takes only 5 seconds to destroy it". Akimaanisha unaweza kutumia miaka 20 kujenga haiba yako mbele ya jamii lakini sekunde 5 tu zinatosha kuharibu kile ulichokijenga kwa miaka 20. Na hivi ndivyo alivyofanya Bahati Bukuku. R.I.P Bukuku.!

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI