BAVICHA MKOA WA IRINGA WALAANI VIKALI SIASA CHAFU

BAVICHA MKOA WA IRINGA INALAANI VIKALI SIASA CHAFU  ZA CCM

Na Baraka Mfilinge


Pichani ni Mwenyekiti BAVICHA. Mkoa wa Iringa, kamanda Baraka Leornad Mfiringe


Ndugu zangu mtakumbuka usiku wa jana tarehe 18/05/2015 gari ya mwenyekiti wa bavicha jimbo la Iringa mjini ndugu Leonce Marto  yenye namba za usajili T 108 CKR ilichomwa moto na mahasimu wetu wa kisiasa, baada ya mashindano makali wakati walipokuwa vituoni wakati wa uandikishaji wapigakura kwenye kituo cha zahanati kata ya Isakalilo mchana wa juzi.

Ndugu zangu mkumbuke kuwa hili sio tukio la kwanza kwa mahasimu wetu kisiasa kufanya hizi siasa chafu na mbaya ndani ya mkoa wa Iringa ambazo kimsingi huongozwa na hila kwa madai kuwa wanataka kulikomboa jimbo la Iringa mjini kutoka kwa Chadema chini ya Mh. Peter Msigwa ambazo ni ndoto za alinacha na hazitekelezeki.

Ndugu zangu kumekuwa na hila nyingi dhidi ya viongozi wa Chadema Diaspora na mali za chadema mkoa wa Iringa hususa ni jimbo la Iringa mjini, kwani itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 16/04/2015 pikipiki ya chadema yenye namba za usajili T 414 CZY ilipotea katika mazingira ya kutatanisha kwenye viwanja vya mahakama kuu ya mkoa wa Iringa nayo mpaka sasa haijapatikana, lakini kama haitoshi gari ya mwenyekiti wa Chadema jimbo la Iringa mjini ndugu, Frank Nyalusi ilipigwa mawe na kuvunjwa vioo, swali la kujiuliza ni kwanini matukio haya yote dhidi ya viongozi wetu wa Chadema tu?

Ndugu zangu kwa matukio haya yote baraza la vijana la chadema mkoa wa Iringa linalaani vikali siasa hizi za ovyo na za hila zinazoongozwa na viongozi ambao hawajui siasa safi bali wamegeuza siasa kuwa ni vita, na kimsingi jeshi la polisi mkoa wa Iringa linapaswa kujua kuwa lisipodhibiti vitendo hivi viovu mapema kuelekea kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu machafuko makubwa yaweza kujitokeza ndani ya mkoa wetu wa Iringa, kwani nasi hatutakuwa tayari kuendelea kulalamika sisi tu ila hali wenzetu wakiendelea kufanya siasa chafu huku wakibaki wakirandaranda mitaani bila kuchukua hatua zozote.

Ndugu zangu nitoe rai kwa vijana wote wa chadema mkoa wa Iringa kuanzia vyuo vikuu, sekondari, machinga, mama ntilie na wengine wote kulinda viongozi wa chama kikamilifu na mali zake zote kwani hizi ni dalili za kuonyesha kuwa jeshi la polisi limeshindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo wa kulinda raia na mali zake
Pili tunalitaka jeshi la polisi kushughulikia mambo haya yote mapema iwezekanavyo kwani ndio njia pekee ya kurejesha imani kwa wananchi

Mwisho tuwnaaomba wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwani ndio njia pekee ya kuwasulubu watesi wetu ccm mwezi oktoba mwaka huu 2015.
Gari la kamanda Leonce Marto kabla ya kuchomwa moto

Muonekano wa gari baada ya kuchomwa na kufanikiwa kuuzima


Petrol iliyokutwa eneo la tukio 


                                     

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI