OPERATION DELETE CCM ISIMANI



OPERATION DELETE FUTA KABISA CCM JIMBO LA ISIMANI



          Mcheza kwao hutuzwa, hakika makam mwenyekiti BAVICHA Bara na mwenyekiti BAVICHA ISIMANI kamanda Patrick Ole Sosopi ameonekana kuwa shupavu katika kila nyanja katika mapambano. Anaonekana akiwa anaendelea kupambana kuhakikisha anamng'oa mkoloni mweusi Mh. William Ngelimembe Lukuvi siku zote. Licha ya kukumbana na nguvu ya dola na kujikuta mikononi mwa polisi mara kadhaa lakini dhamira yake imekuwa ikimuongoza  vyema hali ambayo inamuweka kuwa imara zaidi.

         Amekuwa akiingoza  Operation ya kudelete ccm  mara kwa mara ndani ya jimbo la Ismani na hata mikoa mingine ikiwa na lengo moja tu la kuwakomboa wana Isimani katika lindi kubwa la umasikini uliokithiri japo jimbo hilo limekuwa chini ya mbunge aliyebahatika kupata nyadhifa kubwa sana serikalini, na ni aibu sana kwa hali ilivyo sijui wageni wake wakija huwa anaficha wapi uso wake huyu Mbunge na waziri wa ardhi nyumba na makazi.

        Wananchi wa Isimani wamekosa huduma bora za kijamii kabisa kwani kamanda Sosopi amekutana na wananchi ambao wamemueleza matatizo yao yanayoweza kutatuliwa kwa wepesi kama endapo atapewa ridhaa na hayo yote mbunge wa sasa kaelemewa na hofu ataweza kuyatatua hata miaka mia ijayo.

         Siku ya leo alisikitishwa sana alipokuta wananchi wakihangaika kuchimba kisima ili wapate maji kwa matumizi ya nyumbani na mifugo hali iliyopelekea Makamu mwenyekiti BAVICHA BARA, Mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Mwanza, Katibu BAVICHA Iringa mjini kuamua kuungana nao kukichimba kisima hicho.  
 Makamu mwenyekiti Bwana Sosopi alionekana kusikitishwa na hali hiyo akasema
"Ni jambo la ajabu sana kuwa na mbunge kwa miaka ishirini(20) mfululizo lakini jimboni kumelala, hakuna maji safi na salama, hakuna huduma nzuri"
          Kinachotia moyo na kufurahisha zaidi ni mwitikio mzuri wa wananchi na kupokea mabadiriko ya kweli.
Wanasema wananoa kisu cha kumchinja mkoloni CCM,
Nawatakia kila la kheri makamanda

Makamu mwenyekiti BAVICHA BARA, Kamanda Patrick Ole Sosopi akiwasaidia wananchi

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI