UKIMYA KATIKA SEKTA YA KILIMO
UKIMYA KATIKA SEKTA YA KILIMO
Na Mwl. Bongole
Si kila anayeanza safari hufika mwisho wa safari husika. Naaam japo bado tunasafiri matumaini ya kufika yapo ila si kwa siku chache. Sizungumzii kupanda daladala na kuelekea machinjioni au mahali popote pale nikiwa na maana ya mtaa ama kijiweni. La hasha!!
Nazungumzia safari katika usimamizi bora wa idara ama sekta ya kilimo ili kufikia mahali ambapo tutakua na uwezo wa kuzalisha chakula cha kututosha na kuuza nje ya nchi tena si uarabuni ama ulaya na marekani hapana tuwauzie warundi waganda na hata wasudani na wakenya ambao kwao ardhi ni kidogo. Wanunue kwetu, tuzalishe kwa ajili yao. Nilifundishwa darasani kwangu kua ukizalisha bidhaa na kuuza kwa wenzio hasa nje ya nchi utajipatia fedha za kigeni.
Naam hatuna usimamizi bora katika kilimo. Sera ya kilimo na ufugaji ni nzuri sana ina kila aina ya mikakati na namna sahihi ya kufikia mapinduzi ya kilimo. Najikuta na maswali mengi sana hasa baada ya kusoma "agriculture and marketing policy (2008)" japo imebadilishwa mara kwa mara na ile inafahamika kama "agriculture and rural development strategy (2005-2030)" alafu baadae tizama mambo yanayoendelea kwenye kilimo, chakula matunda na maua, uvuvi, idara ya misitu na ufugaji nyuki nastaajabu sana. Bado tuna safari ndefu kufika tunapotaka.
Katika maeneo hayo yote niliyotaja bado hatujafikia kiwango cha kuzalisha na kuwa na uhakika wa kutokuagiza chakula kutoka nje ya nchi, yaani tuwe na uwezo wa kuzalisha samaki kwa gharama ambayo kila mtanzania anaweza kumudu lakini pia zipatikane kwa wakati.
Pili tumeshindwa kuzalisha asali katika kiwango ambacho kila anayehitaji hapa nje ya nchi ataipata kwa gharama nafuu anayoweza kuimudu.
Tatu tumeshindwa kuzalisha matunda kwa kiwango ambacho tunapohitaji tunda fulani sokoni lipatikane kwa wakati lakini pia kwa gharama ambayo ni nafuu kwa mtumiaji.
Nne tumeshindwa kuzalisha mazao ya biashara na kufikia uwezo wa kudhibiti soko la ndani pekee. Kwa mfano. Ni jambo la kustaajabisha tunaagiza ngano nje ya nchi kwa ajili ya kuhudumia viwanda vya unga wa ngano vilivyoko dar es salaam na maeneo mengine. Yaani pamoja na kua na eneo kubwa sana la ardhi ambayo haijaendelezwa tumeshindwa kuzalisha ngano kwa ajili ya kiwanda cha Bakhresa? Kaazi ipo.
Sasa tujiulize tunachohitaji ni kitu gani?
Katika kufikiri kwangu nimeona kuna mapungufu kadha wa kadha. Katika hayo
1)Tumekua tegemezi sana katika kufadhili bajeti husika katika kilimo kwa mfano. Tutegemee nini kama chakula tunachozalisha ni kwa ajili ya matumbo yetu kisha mfadhili awe ni wa kutoka norway? yaani ni sawa na kule nyumbani kwako unataka unataka kula ugali kwa kutegemea jirani yako akupe fedha kwa ajili ya kununua unga. Na asipokupa kwa wakati je? Si utakufa njaa?
2) Kuendelea katika idara hizo kwa kutegemea misaada na wasimamizi ambao kila siku wanabadili majina bila kujua hasa lengo napo ni tabu na kikwazo kingine. Utasikia leo wanaitwa PADEP kesho MKUKUTA keshokutwa wanakuja na jina jipya japo malengo yao wanadai ni yale yale hiyo nayo ni shida.
3) Hatuwezi kuendelea kwa kutegemea miundombinu hii michache na duni isiyo na viwango halisi katika kuruhusu vyombo vya usafirishaji kupita kwa uhakika. Kwa mfano. Mashamba mengi ya mkonge ambayo yalianzishwa miaka mingi iliyopita na njia kuwekwa leo hii huwezi pita na ukafika salama na kwa wakati. Lakini pia kuna maeneo yaliopo mbeya vijijin njombe na iringa bila kusahau morogoro tanga na babati ambayo ni muhimu sana kwa uzalishaji na ina manufaa kwa kilimo lakini hayapitiki. Hii ni changamoto.
4) Tuna viongozi wasionamalengo kabisa hawawezi kufikiri na hawafai katika usimamizi wa sera. Kwa mfano, Toka miaka ya 2000 kuna mashamba yaliyokua yanasimamiwa na serikali na yakafanya vizuri sana lakini kutokea hapo tayari kadri mahitaji yanapoongezeka mashamba yanadidimia. Mfano mzuri ni mashamba ya ngano karibu hekari elfu 70 huko manyara leo hii yako wapi.
Kinachoendelea ni sawa na unamlea mtoto na kila anapokua uwezo wa kifikiri lakini pia wa kutenda na mafanikio yake ni kutoka kuelewa sana kuelekea kua mbumbumbu. Hili nalo ni tatizo tena kubwa.
5) Ili kuendelea kwenye kilimo ni vyema kua na nyenzo za kurahisisha utendaji katika kilimo. Maana yake ni kua kuendelea katika kilimo kuendane na mapokezi ya mfumo mpya wa mapinduzi katika sayansi (zana na dawa za wadudu) ili kurahisisha shughuli za kilimo. kwetu sisi bado tumekua nyuma katikamaendeleo ya sayansi katika kilimo.
6) Sijui ni kwa kiwango gani tumejifunza kutoka kwa wenzetu kwa kiwango gani tumewekeza katika ujasusi katika sekta ya kilimo ili walao tupate siri ya mafanikio katika nchi za wenzetu. Sijui maana sioni hata faida ya safari tunazozifanya nje ya Tanzania kama idara ya kilimo nchini kwa lengo la kujifunza. Tumepata uhuru mwaka 1961 huu ni mwaka 2015 sijui tunatatizo gani katika kumtambua na kumwajibisha adui yetu.
Yerico nyerere ana majibu kwa jinsi ya kusolve haya anaamini tatizo si chama kileee. tukikitoa tu dawa imepatikana, kaazi kwangu mimi nimeandika tena kwa uhuru kabisa. Sina uhakika wa uhuru baada ya kuandika
Nawatakia siku njema
Na Mwl. Bongole
Pichani ni wakulima ambao wanapumzika baada ya kuchuma nyanya zao

Comments
Post a Comment