GIZA NENE VYUO VIKUU

NALIONA GIZA NENE OCTOBER KWA VYUO VIKUU

Na Alex Elifuraha

kwanza Jiulize kwa sekunde takatifu.
wewe ni mtanzania,mtanganyika au mzanzibar???
Je una umri gani?
Je utapiga kura?
Je ni haki yako kupiga kura?
Je utahama Tanzania?

Vyuo vikuu ni Tunu ya fikra endelevu za mabadiliko na sababu kubwa ni mfumo wa elimu pana inayopatikana na pia ni Jukwaa kubwa ni umri wa mabadiliko ya kimtizamo,


Mapinduzi ya falsafa za kimfumo yanayopatikana vyuo vikuu yanatakiwa kuonekana katika matunda ya mabadiliko katika sura ya dunia.

Katika mabadiliko yoyote umoja ni silaha muhimu sana na hii inadhihirishwaa na umoja ulioonyeshwaa kipindi cha kutafuta uhuru katika mabara mbalimbali ulimwenguni na hasa bara la Afrika.

Na mabadiliko ya mfumo ni ndoto kama hayataongozwa kwa njia za kidiplomasia na demokrasia iliyokoma kupitia vijana makini walioko vyuo vikuu.

Nianze kwa nchi yetu ambayo kwa sasa inahitaji mabadiliko makubwa sana ya kimfumo kwa kupitia wanazuoni na hasa katika karne hii ambayo tuna vyuo vikuu zaidi ya 50 kuzungaka Tanzania.

Njia kuu ni utayari,kuaminiana katika mabadiliko tunayoyaamini kwanza tuanze kwa kuuliza Je tutapiga kura na Je mikakati ipi inaonyesha kuwaa wanazuoni tutapiga kura?? kama tumekubali haki yetu ipotee ipo wazi kuwa mabadiliko tunayoyataka yatakua ni Ndoto za alinacha.

Naamini katika msafara wa mamba kenge pia wamo,ila wanakua hawana madhara katika Jamii ya wasomi .


Tena kwa sasa ambapo mfumo uliopo umekataliwa na makanisa,makasisi,waalimu,madereva,wauguzi,....nk tuhakikishe tunashinikiza kupata haki yetu ya msingi ya kupiga kura.

Ni bora kutumia asasi za kiraia,haki za binadamu na asasi za kisheria kujua mstakabali wa upigaji kura wetu.

Alex Elifuraha

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI