KILIMO CHA NYANYA

KILIMO CHA NYANYA NCHINI TANZANIA

Na Goliath Mfalamagoha

Wahenga wanasema  “kilimo ni uti wa mgongo” ikiwa na maana kilimo ndio nguzo kuu ya maisha ya mwanadamu pia nami sipingani na kauli hii ya wahenga wetu japo kwa miaka hii ya karibuni imekuwa kinyume na kauli mbiu hii ya wahenga.Nami ningependa kuangazia zaidi juu ya kilimo cha nyanya ambalo ni zao kuu aina ya mbogamboga au tunda  ,nyanya inalimwa sana mikoa ya iringa ,Morogoro,Arusha,Shinyanga n.k .
 
Mkulima wa nyanya katika kijiji cha Mgama Bwana Raphael Kihongosi, akifurahia zao la nyanya shambani kwake, anasema pamoja na elimu yake aliyoipata ya Iniformation technology (IT)  lakini kwake kilimo ndio baba na mama, hajutii kuwa mkulima japo changamoto ni nyingi.

Kuna aina kuu mbili za nyanya ambazo ni  nyanya ndefu na nyanya fupi hivyo wakulima hulima kutegemea na aina ipi inastawi zaidi katika eneo lao na urahisi wa kuzitunza,japo asilimia kubwa hupendelea  nyanya ndefu kwa sababu fupi huhitaji matunzo makubwa sana kuliko ndefu. Nyanya zinazolimwa sana nchini kwetu ni jamii ya Tanya ,Ridomil,ONXLl,F1  na Roma ambayo ililimwa sana karne ya 20 haina maana ni hizi tu zipo nyingine nyingi zaidi lakini mda hautaniruhusu kutaja zote.

HATUA ZINAZOCHUKULIWA WAKATI WA KULIMA NYANYA.

1.Hatua ya kwanza andaa mashamba utakayolima nyanya zako na pia chagua aina ya mbegu utakayotumia katika mkoa au eneo husika utakalolima nyanaya zako.

2.Baada ya kuandaa mashamba na aina ya mbegu utakayoitumia , unatakiwa kuandaa vitalu ambavyo utawatika/utasia mbegu za nyanya zako japo unaweza kusia hata kwenye mashimo utakayochimba shambani,nyanya hii huchukua siku5 hadi 10 au 12kuota.Wakati wakusia waweza ukawa ulitumia mboji/mbolea ya asili iliyomwagwa wiki mbili kabla ya kusia au waweza tumia mbolea aina ya DAP au yoyote ya kupandia sio kukuzia

3.Huku mbegu yako uliyosia ikiendelea kuota na kukua endelea na maandalizi ya shamba utakalopanda nyanya zako,kama una mboji/mbolea asilia /samadi unaweza ukamwaga shamba lote au kwenye mashimo utakayopanda nyanya zako ili kuongeza rutuba.

4.Ikiwa shamba limekwisha andaliwa tayari ,utachimba mashimo siku mbili kabla ya siku uliyopanga kupandikiza mbegu/miche ya nyanya ili ardhi iweze kupoa kidogo.

5.Unatakiwa kuandaa mahitaji muhimu yote kama vile mbolea ya kupandia na kukuzia, dawa ya wadudu na ya ukungu, mabomba ya kunyunyizia dawa na pump ya kumwagilia na vifaa vya kuhifadhia maji kama shamba halina kisima au bwawa, majembe n. k

Baada ya kupandikiza nyanya baada ya wiki 2 au mwenzi unatakiwa kuweka mbolea ya kukuzia, na kuweka dawa,Maua yakishaaza dawa unapaswa kuweka mara moja kwa wiki hadi pale utakapomaliza michumo.

NI CHANGAMOTO ZIPI WAKULIMA WA NYANYA WANAKUTANA NAZO
1.Uhaba wa pembejeo za kilimo ni changamoto kubwa kwa wakilima wote nchini Tz.

2.Wadudu waharibifu na sugu kama vile viwavi, minyoo n. k pia ukungu hasa sehemu zenye ukungu mwingi na mvua nyingi

3.Uhaba wa maji kwa ajili ya kumwagilia kama shamba lako lipo mbali na sana na vyanzo vga maji au lipo sehemu maji ni ya shida.

4.Kukosa soko la uhakika na ikumbukwe nyanya ni mali mbichi ambayo ni rahisi sana kuharibika hali inayopelekea wakulima wengi kukata tamaa

5. Nyanya ninyanyue, nyanya ninyanyase ni neno la wakulima kwani bei huwa zinaweza kushuka au kupanda ghafla, wiki hii unaouza 20,000 - 30,000 wiki ijayo unakuta 2000-7000
Inakatisha tamaa kidogo
Nini kifanyike kutokana na changamoto?

Kutokana na changamoto hizo zote ni lazima serikali yetu iweze kufikisha pembejeo kwa wakati, kutuwekea soko la uhakika la nyanya zetu ikiwa ni pamoja na kuweka viwanda vitakavyotengeneza aina yoyote ya bidha inayotokana na nyanya.
Bei za nyanya lazima ziwe zinawiana na gharama tulizotumia kwenye maandalizi kuliko kupata chini.
Kufanya maandalizi ya kutosha na pia tuwezeshwe.


Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI