Posts

Showing posts from February, 2017

Vyama vya wafanyakazi vijifunze kwa Kituo cha Sheria na Haki za binadamu LHRC!

NA RUSTON MSANGI. Ni jukumu la kila chama cha wafanyakazi nchini  kusimamia, kulinda, kuboresha maslahi, na kuhakikisha haki za wanachama wake hazivunjwi, wala kukiukwa kwa namna yoyote ile. Majukumu hayo ya chama chochote cha wafanyakazi hayaepukiki kwa kuwa wanachama huwa na utaratibu maalumu wa kuchangia kwa njia ya ada, ili kufanikisha shughuli za chama husika. Mfano wa vyama vya wafanyakazi nchini ni kama Chama cha walimu Tanzania (CWT), Muungano wa wafanyakazi katika sekta ya viwanda na biashara (TUICO), Umoja wa wafanyakazi wa afya wa serikali (TUGHE), Muungano wa wafanyakazi wa Serikali za mitaa (TALGWU). Mwezi huu umekuwa ni pigo kwa wafanyakazi nchini, hasa wale walionufaika na mikopo ya elimu juu wakati wa masomo yao. Maumivu haya makubwa ni kuhusu mabadiliko ya sheria yaliyopelekea kuongezeka kwa makato ya marejesho ya mikopo, kutoka 8% ya awali hadi 15% iliyoanza kukatwa mwezi huu wa pili. Suala hili kiukweli limewaacha wafanyakazi wengi nchini na maumivu mak

Elimu bure imekuza tatizo la chakula mashuleni

NA RUSTON MSANGI. Ubongo wa mwanadamu ili ufanye kazi sawa sawa na kwa ufanisi,unahitaji lishe.Ni muhimu kula vizuri na kushiba. Mwanafunzi darasani,anatumia  akili nyingi.Ili aweze kufikiri vizuri na kuelewa anachofundishwa ni lazima apate chakula kwa muda sahihi na kushiba.Ni muhimu. Kabla ya waraka wa elimu bure wa serikali ya awamu na tano  mwaka 2016, wanafunzi katika shule nyingi za serikali walikuwa wanakula shuleni kutokana na michango ya  wao. Baada ya waraka wa elimu bure kuanza kutekelezwa rasmi mwaka jana 2016,kumetokea  mabadiliko makubwa ya hali ulaji wa chakula mashuleni.Wanafunzi hawali kama mwanzo. Waraka wa elimu bure umeainisha  majukumu ya serikali,  wizara ya elimu, TAMISEMI, Halmashauri, Wakuu wa shule na walimu Aidha umeanisha majukumu ya mzazi katika kutekeleza elimu bure. Mojawapo ya majukumu ya wazazi ni kuhakikisha mtoto/mwanafunzi anapata vifaa vyote muhimu vya shule kama madaftari na sare za shule . jukumu jingine kubwa na muhimu kwa wa