KILIMO CHA NYANYA NCHINI TANZANIA Na Goliath Mfalamagoha Wahenga wanasema “kilimo ni uti wa mgongo” ikiwa na maana kilimo ndio nguzo kuu ya maisha ya mwanadamu pia nami sipingani na kauli hii ya wahenga wetu japo kwa miaka hii ya karibuni imekuwa kinyume na kauli mbiu hii ya wahenga.Nami ningependa kuangazia zaidi juu ya kilimo cha nyanya ambalo ni zao kuu aina ya mbogamboga au tunda ,nyanya inalimwa sana mikoa ya iringa ,Morogoro,Arusha,Shinyanga n.k . Mkulima wa nyanya katika kijiji cha Mgama Bwana Raphael Kihongosi, akifurahia zao la nyanya shambani kwake, anasema pamoja na elimu yake aliyoipata ya Iniformation technology (IT) lakini kwake kilimo ndio baba na mama, hajutii kuwa mkulima japo changamoto ni nyingi. Kuna aina kuu mbili za nyanya ambazo ni nyanya ndefu na nyanya fupi hivyo wakulima hulima kutegemea na aina ipi inastawi zaidi katika eneo lao na urahisi wa kuzitunza,japo asilimia kubwa hupendelea nyanya ndefu kwa sababu fupi huhitaji matunzo makubwa sana
Comments
Post a Comment