Posts

Showing posts from April, 2015

BIG RESULTS NOW YENYE MATESO KWA WANANCHI

I BIG RESULTS NOW (BRN) KWA TAFSIRI YA MAFANIKIO MAKUBWA SASA KATIKA SEKTA YA AFYA NCHINI TANZANIA. Na mwandishi wako,Waziri Martine Kindole            BIG RESULTS NOW sio neno geni sana miongoni mwetu ,tuliowengi au tulio wachache bila kujali ni wasomi,sio wasomi ,masikini,tajiri,weusi,weupe,au wanawake kwa wanume.Naomba ieleweke kwamba wanaoratibu mpango huu ,wametafsiri neno hili kwa lugha rahisi kwamba BRN ni “MATOKEO MAKUBWA SASA”. Neno hili limekuwa likitumiwa sana na wanasiasa wengi,pia hata wataalamu mbalimbali katika sekta mbalimbali nchini, ikiwemo sekta ya afya.  Kwa ujumla wake sekta ya afya ni moja ya sekta muhimu katika ustawi wa taifa lolote na watu wake duniani kote, kwani afya ndio msingi thabiti wa mtu yoyote  bila kujali cheo chake au pesa zake na ndio maana sekta muhimu kama hii inahitaji sera thabiti zinazotekelezeka.               Katika taifa letu, kumekuwa na MWENDELEZO WA EPISODE ambayo hubadilishwa jina kila kukicha, ila picha kuwa ile ile mifano yake ha