BIG RESULTS NOW YENYE MATESO KWA WANANCHI

I BIG RESULTS NOW (BRN) KWA TAFSIRI YA MAFANIKIO MAKUBWA SASA KATIKA SEKTA YA AFYA NCHINI TANZANIA.
Na mwandishi wako,Waziri Martine Kindole 

          BIG RESULTS NOW sio neno geni sana miongoni mwetu ,tuliowengi au tulio wachache bila kujali ni wasomi,sio wasomi ,masikini,tajiri,weusi,weupe,au wanawake kwa wanume.Naomba ieleweke kwamba wanaoratibu mpango huu ,wametafsiri neno hili kwa lugha rahisi kwamba BRN ni “MATOKEO MAKUBWA SASA”. Neno hili limekuwa likitumiwa sana na wanasiasa wengi,pia hata wataalamu mbalimbali katika sekta mbalimbali nchini, ikiwemo sekta ya afya.  Kwa ujumla wake sekta ya afya ni moja ya sekta muhimu katika ustawi wa taifa lolote na watu wake duniani kote, kwani afya ndio msingi thabiti wa mtu yoyote  bila kujali cheo chake au pesa zake na ndio maana sekta muhimu kama hii inahitaji sera thabiti zinazotekelezeka.

              Katika taifa letu, kumekuwa na MWENDELEZO WA EPISODE ambayo hubadilishwa jina kila kukicha, ila picha kuwa ile ile mifano yake halisi ni kama;"MKUKUTA 1&2","MPANGO WA MIAKA MITANO (5),MPANGO WA MIAKA 25 " na mipango mingine kedekede.Na sasa  tuna  huu tena ambao umekuwa ukitangazwa sana kwa jina la ''BIG RESULTS NOW'' (BRN) hata kabla mipango mingine haijafanikiwa na mingine haijamalizika.Na sina hakika kama twayafanya haya yote sijui kwa kutumia tafiti zipi,au mtu akiamka anasema anayoyaona yafaa. Yawezekana waliobuni na kuratibu mpango huu wa BIG RESULTS NOW walikuwa na nia nzuri japo sina imani na nia yao sana.

               Ukiangalia kwa makini BRN katika sekta ya afya wameainisha kutekeleza mambo mengi sana ambayo sitayaweka yote bayana, kwa mfano mpango wa kuwa na Zahanati Vijiji vyote,Vituo vya afya Kata zote ,Hospitali Wilaya zote na kuzipa hadhi ya Rufaa hospitali za Mikoa zinazokidhi vigezo.Sambamba na hayo yote wameonesha kuwa walilenga kuboresha huduma za afya kwa kuboresha mazingira ya kufanyia kazi ili yawe rafiki kwa wagonjwa na wafanyakazi wote.Walilenga kuboresha mazingira kwa kuhakikisha vitendea kazi vinakuwepo vya kutosha (uwepo wa dawa ,damu salama,maabara safi na vifaa vyote kulingana na hadhi ya ngazi ya kituo husika) na kuhakiksha upatikanaji wa rasilimali watu kama vile madaktari,wauuguzi,watalaamu wa maabara n.k,ili zikidhi vigezo na viwango vya kimataifa kama shirika la afya duniani (WHO) linavyoyataka mataifa kufanya hivyo. Katika hili sina budi kuwapongeza kwani sasa vyuo vingi vinazalisha madaktari, wauguzi na wafanyakazi wa kada nyingine zote japo kitendawili kipo na hakuna wakukitegua hadi sasa.

                   Kwa kuangalia mambo yote niliyoainisha hapo juu nitajikita zaidi Tanzania bara( iliitwa Tanganyika enzi za ukoloni,uhuru hadi 1964 kabla ya Muungano) kwa sababu swala la afya si la Muungano, Tanzania bara ina mikoa 25,wilaya 133 ,vijiji 19200 na kata elfu tatu na ushee pamoja na mipango yote thabiti  hadi sasa tuna Hospitali 21 tu za Mkoa,86 za Wilaya,Vituo vya afya 578 na Zahanati zisizozidi 6,000. Jiulize mwananchi mwenzangu wa bara Je,’BRN’ inawasaidia wananchi wote au wakubwa tu? Majibu unayo mwenyewe.

                   Nakukumbusha tena jambo la msingi zaidi katika sekta ya afya,SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO) wameweka vigezo katika kila jambo kukidhi matakwa ya wananchi wote ,shirika hili la afya duniani linataka Daktari mmoja ahudumie wagonjwa 1000 kwa mwaka, lakini imekuwa kinyume katika nchi nyingi Afrika ikiwemo Tanzania.Nchini Tanzania Daktari mmoja anahudumia wagonjwa zaidi ya 20,000 hii ikiwa na maana ya kwamba hatujakidhi viwango vya Shirika la Afya Duniani mara 20 zaidi.Na hiki ndicho kiini kikuu kilichonifanya niandike unayoyasoma ndugu msomaji wa makala zangu.Pamoja na uwepo wa madaktari wachache ukilinganisha na hitaji la kimataifa bado kumekuwa na wimbi kubwa la uwepo wa madaktari mtaani wasio na ajira. Sasa sijui ni ukata wa serikali? Au wameona afya sio muhimu na kuona ni bora BVR,KURA YA MAONI na UCHAGUZI MKUU ? lakini swali linakuja mgonjwa atapata fursa ya kupiga kura huku anakosa wa kumuhudumia? Mimi sijui najiuliza tu kwa mnaojua hayo mpo.

                 Niliumia sana,nilisikitika sana,niliwaza na kuwazua sana,nilitafakari sana ,nilikosa nguvu mithili ya mtu aliyekosa chakula siku tatu nilipokutana na kijana mwenzangu niliyesoma naye Sekondari (O’LEVEL) na alikuwa ana uwezo mkubwa kitaaluma darasani ni balaa, (Tulimwita shetani au Genius),Nilipomuuliza mbona upo tu mtaani na umepungua sana mkuu?ukumbuke mi namiliki usafiri wangu na nyumba yangu kwakuwa familia yangu ilikuwa ni yenye uwezo kidogo,kwahiyo sikupata shida toka nasoma hivyo niliaza na masihala ya shuleni hapa na pale, sikia majibu yake sasa “Asiyesikia la mkuu ……mmmmh, ndugu yangu ni stori ndefu sana, nilipomaliza kidato cha sita nilishauriwa na wengi sana,ndugu na jamaa zangu,waliniambia  nikasome hata socialogy tu au  education au faculty yoyote ya miaka mitatu nikaona wananipotezea muda nikawapuuza tu sikuwasikiliza, kama unavyojua mtu wangu ukionja radha ya sayansi unahisi wa tofauti.Nakumbuka hata nilipokuwa O’ LEVEL wewe ni miongoni mwa walionishauri nikasome HGK  au HKL ,au  yoyote ile, ila sio sayansi nikawaona hamfikirii,sasa kama unavyoona ndugu yangu mguu wangu umeota tende, japo mvumilivu hula mbivu lakini kwangu imekuwa kinyume” 

                      Duuuuh vipi mbona unanititisha kuna nini kimekukuta au ulifukuzwa chuo? Nilimuuliza,Akanijibu kwa upole huku machozi yakibubujika “Nilisoma kwa juhudi sana wewe ni shahidi toka umefahamiana nami ,nimesoma miaka mitano chuo lakini hadi sasa nipo mtaani kama unavyoona nafanya mishe za hapa na pale nafikiria kurudi kijijini nikalime tu,hapa ninapoongea na wewe kuna wenzangu zaidi ya 110 tuliotakiwa kuaza Mafunzo kwa vitendo (internship) mwenzi wa pili hatujui hatima yetu japo ni haki yetu kisheria baada ya kumaliza masomo yetu” Alisema walitakiwa kupata usajili wa kuanza mafunzo hayo kuanzia tr 15/02/2015 na kufungwa  tr 30/04/2015, lakini kila wakifuatilia majibu ni yale yale ya bado swala lenu linafanyiwa kazi. Aliongeza kwa kusema wenye pesa za kujikimu (yaani wenye uwezo wa pesa) waliambiwa wanaweza kuandika barua kukubali kufanya kazi bila kulipwa kwa mda wote hadi pesa zitakapotoka (commitment letter) ili wasije kudai baadaye, ikiwa na maana wafanye kazi hadi Augost bila malipo.Wapo waliofanya hivyo kwa kuwa wametoka familia kama yangu na wapo walioshindwa kufanya hivyo,wale wenye uwezo mdogo kama rafiki yangu wakae mtaani toka mwaka jana 2014 walipomaliza chuo hadi mwaka huu Augost au September pesa itakapopatikana .Kwani anasema hadi sasa waliishia kuandika majina na mahali wanapotaka kwenda, waliambiwa yanakwenda HAZINA toka trh kumi 15 feb wanaambiwa yanafanyiwa kazi japo hawakati tamaa kufutilia na hali hii inaweza kuleta migogoro baina yao.Nilijikuta nakosa nguvu zaidi baada ya story yake.Ikumbukwe wapo wanaotumia milion 10 kwa kununua mboga tu na milion 20 sijui 40 kwa ugolo,na haya NI MATUNDA YA ESCROW.Waziri wa afya sijui kama anajua kuwa tunakosa wakutuhudumia huku madaktari wanauza nyanya kariarkoo na mitaa mingine na wengine wanakwenda kulima mmmmh ama kweli dunia tambala bovu.Nilifikiria zaidi na kuona hali hii itakatisha tamaa wanaopenda masomo ya sayansi na pia madaktari hawa hawatukua na moyo wa kibinadamu wanapotoa huduma kwani wakikumbuka wanayotendewa na serikali wakati ni haki yao kisheria mmmmmmmmmmmmmmmh 

                       Kwa maelezo hayo  tunashuhudia falsafa mpya kutoka kwa Rais Kikwete ya 'Big Results Now' (BRN).Hii ni falsafa isiyo na mashiko hata kidogo iliyoratibiwa na kuanzishwa kwenye vyumba vya Ikulu ya Tanzania, eti ije kulibadili Taifa kwa haraka sana!!!!  Sitaki kuwa msemaji mkuu,ila tunashuhudia kweli Taifa likibadilishwa kwa haraka sana na hiyo falsafa ya 'BRN'.Taifa ndani ya miaka miwili limebadilika sana kwa mfano katika sekta afya ukilinganisha  bajeti ya mwaka 2013/2014  ambayo ilikuwa ni Tsh bilioni 753 katika hii Tsh billion 282 ni matumizi ya kawaida, na bajeti ya mwaka wa fedha 2014/2015  ambayo imepungua na kufikia Tsh bilioni 622 katika hii matumizi ya kawaida ni billion 317.Kumbuka malengo niliyoainisha kule juu na yanayowakuta wasomi wa kada hii,kwa mantiki hii moja kwa moja utaona BRN ilivyo tamu kwa wakubwa na chungu kwa wananchi.Jiulize kwa mapungufu ya bajeti hii kuna uwezekano wa kuyatekeleza maswala yaliyoainishwa na ikumbukwe nimeweka baadhi tu.Vitu vingi vinaenda hovyo hovyo kwa kutumia falsafa ya 'Big Results Now' iliyoasisiwa na Rais Kikwete kupitia washauri wake.Jambo la kujifunza ni kwamba matokeo ya hiyo 'BRN' hayako mbali na tutashuhudia mengi katika sekta zote nchini,kwani sijaeleza adha ya damu salamu miezi michache iliyopita,kwani kalamu imeisha wino nitaleta part 2 na nyinginezo muone uozo kwenye sekta mbalimbali leo nimejikta sekta ya afya.

                 Mimi kama mwanaharakati namtaka Mh.Rais, Prof.Dr.Jakaya Mrisho  Kikwete aelewe kwamba falsafa ya 'BRN' ni kula fedha za umma kifisadi na kuharibu kizazi ambacho kinatengenezwa na hiyo 'BRN' na hakuna lingine.Narudia tutashudia mSengi sana ndani ya taifa hili lenye utajiri mkubwa kama Mh hataona umuhimu wakulifanyia kazi na mawaziri wote kwa nafasi zao na watendaji wengine wa serikali.
USITAFUTE MCHAWI TEKELEZA MAJUKUMU YAKO 
NAJENGA TANZANIA kwa kusema ukweli CYBERCRIME USINIGUSE kwa maslahi ya wananchi 




  , 

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI