Muuguzi mahiri kutoka hospitali ya Taifa ya Mhimbili -Mloganzila aipaisha fani ya uuguzi nchini

 Na mwandishi wetu. 


Muuguzi wa hospitali ya Taifa ya Mhimbili-Mloganzola, Bw. Wilson Fungameza Gwesa  ameibuka mshindi kwa nafasi ya tano kati ya wauguzi hamsini na mbili elfu (52,000) walioshindwa  kutoka nchi zaidi ya 200 duniani.

Kwa lugha nyingine amekuwa miongoni mwa wauguzi watano bora duniani.

Mashindano haya ya wauguzi yaliandaliwa na Aster Guardian Nursing Award kutoka London.

Kwa namna moja au nyingine Bw.Fungameza ameliwakilisha taifa na hospitali ya MNH-Mloganzila kwa umahiri mkubwa lakini pia ameipa heshima kubwa sana fani ya uuguzi nchini.

Mmoja wa watumishi kutoka hospital ya Mloganzila anamesema "Wilson fungameza amekuwa ni mbunifu na anajituma sana katika kutoa huduma za kiuuguzi kwa ufanisi mkubwa sana"

Bw.Fungameza ameandika kitabu katika fani ya uuguzi kinachotumika vyuoni na maeneo ya kazi ,kwa mjibu wa mtoa taarifa anasema ukisoma kitabu hicho utajifunza mambo mengi juu ya kutambua matatizo ya wagonjwa na namna ya kuwahudumia.


Mbali na uandishi wa kitabu Bw.Fungameza amefanikiwa kugundua kifaa kinachosaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga hasa watoto njiti.

Anasema kifaa hicho kinawasaidia katika upumuaji wale watoto ambao wamezaliwa kabla ya mda wao na mapafu yao hayajakoma.



Umahiri wake uwe chachu kwa wengine ili kuboresha huduma za wagonjwa nchini.






Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI