MH. SUGU AKIUNGURUMA BUNGENI
BUNGE LIMEANZA KWA SUGU KUHAKIKISHIWA UMEME
Na Elly Anangasye
Bunge la Bajeti ya mwaka 2015/2016 limeanza leo kwa Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Osmund Mbilinyi " Sugu " kuhakikishiwa kuwa ahadi ya serikali ya kuweka umeme katika kata za Mbeya Mjini iko palepale.
Katika swali lake la nyongeza ambapo alitaka kujua kauli ya serikali kuhusu ahadi ya serikali ya kufikisha umeme katika Kata za Mbeya Mjini ambazo serikali iliahidi kuwa kufika mwezi juni umeme utakuwa umefika, Mbunge huyo alisema " ni nini kauli ya serikali kuhusu ahadi ya kufikisha umeme katika kata ambazo iliahidi kuwa zitakuwa zimepatiwa umeme kufikia mwezi juni mwaka huu licha ya kuwa shughuli za uwekwaji wa nguzo unaendelea", alimalizia Mbunge huyo.
Katika jibu lake kwa Niaba ya Waziri wa wizara ya Nishati na Madini, Naibu Waziri wa Wizara hiyo alimhakikishia Mbunge wa Mbeya Mjini kuwa ahadi ya serikali ya kuhakikisha umeme utakuwa umefika katika kata hizo kufika mwezi juni iko palepale na shughuli hiyo ilianza na akaongeza kuwa ikitokea kuna jambo lolote Mbunge huyo atataarifiwa, hali iliyopelekea Mbunge huyo kuonyesha kidole ishara ya kutoa onyo kwa kutoridhishwa na kauli ya pili ya Naibu Waziri huyo aliyosema kuwa kama kuna jambo lolote litatokea Mbunge huyo atataarifiwa.
Ikumbuke kwamba katika Bunge lililopita Mbunge Mbilinyi aligeuka mbogo Bungeni kutokana na majibu mawili tofauti aliyopewa katika swali moja ambapo jibu la mwaka jana lilikuwa tofauti na la mwaka huu hali iliyopelekea Waziri wa Nishati kuwaita haraka Viongozi watendaji wa TANESCO kutoka Mbeya na makao makuu DSM kuja kumjibu Mbunge huyo ambapo walimhakikishia kuwa umeme kufika mwezi juni mwaka huu utakuwa umefika katika kata hizo sababu vifaa vyote husika wanavyo.
Baadhi ya Kata za Mbeya Mjini ambazo nguzo zimeanza kusimikwa tangu Mbunge aahidiwe katika Bunge lililopita ni pamoja na Iziwa, Itagano, Iduda, Tembela, Mwasanga na Kalobe.
Na Elly Anangasye
Mh. JOSEPH MBILINYI alimaarufu kwa jina la Sugu akiunguruma bungeni

Comments
Post a Comment