UJASIRI WA PROF LIPUMBA

Ukweli ni Lazima usemwe.

Na Ben Wa Saa Nane

Pichani. Ni Prof. IBRAHIMU HARUNA LIPUMBA mtaalamu wa mambo ya kiuchumi japo nabii hakubariki nyumbani lakini kaonesha uwezo wake kupitia mataifa mengine.

Ni Prof.Ibrahim Haruna Lipumba pekee(Kama yupo Mwingine sikumbuki,Kumradhi) miongoni mwa viongozi wa juu wa Vyama vya siasa aliyetoa msimamo wake hadharani bila kumung'unya maneno kuhusu mgogoro wa Burundi na kumtaka Nkurunzinza aheshimu katiba,mkataba wa Amani wa Arusha na Misingi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki .

Kama ambavyo tumekua tukijadiliana hapa amewataka akina Rais Kikwete kumshinikiza kuachana na mpango wa Kugombea Urais kwa awamu ya Tatu

Hoja yangu hapa ni nini? Ni lazima tuwe na Viongozi wenye uwezo wa kusema bila kuhofia lolote juu ya masuala ya ndani na nje ya mipaka.Tanzania is not an isolated Island.Ni nchi Mwanachama wa EAC.Kutoa msimamo kwa mambo yanayoathiri Tanzania na Mkataba wa EAC ni ujasiri ambao unatoa ishara ya kuwa hata ukiwa madarakani kama kiongozi wa nchi unaweza kutoa misimamo isiyoyumba kwenye majukwaa ya kimataifa

Makala ya Prof.Lipumba kwenye Gazeti la Mwananchi la Leo Uk.30 ni Makala Radical Kabisa ya Kiongozi wa Chama cha Upinzani ndani ya nchi Mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambako Kiongozi wa nchi mijawapo Mwanachama wa Jumuiya Ameonywa hadharani.

Ujasiri huu nimekua nikiuona kwa Raila Odinga akiwa serikalini kama Waziri Mkuu au akiwa kama Kiongozi wa Upinzani.Hukemea na kuonya madikteta hata nje ya Mipaka ya nchi yake bila woga

Huonyesha misimamo kwenye masuala ya kitaifa na kimataifa bila hofu na Unafiki

Steven Kalonzo Musyoka ,kiongozi ndani ya Muungano wa CORD nchini Kenya ambae akikua waziri wa mambo ya nje kipindi cha makubaliano ya amani ya Arusha na tena alishiriki  yeye hakutaka kusema waziwazi kwamba Nkurunzinza anavuruga makubaliano ya amani na katiba ya Burundi.Diplomasia ya aina hiyo huchochea vurugu,ni diplomasia inayomchochechea Perpetrator zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI