HAYA NAWEZA ANDIKA BAADA YA KAULI YA MKUU WA WILAYA ROMBO

HAYA NAWEZA ANDIKA BAADA YA KAULI ILE YA MKUU WA WILAYA YA ROMBO

Na mwl.  Denis Bongole


Kuna kundi moja linaitwa ROMBO UNION ambalo kwa sasa siwezi kupata wala kuandika taarifa baada ya wenyemamlaka walinitoa ili kudhibiti sauti yangu isisikike. kabla ya taarrifa kuhusu wanawake wa rombo kuzagaa nilipata kubishana sana na wanaccmpale kwenye group ya Rombo Union kuhusu suala la kumbebesha lawama mbunge wetu bwana Joseph selasini na kadhia ya kufurika kwa pombe nyingi sana.

Na nilichokielewa kwa haraka baada ya mjadala ule  sakata la ulevi ilikua ni jambo ambalo lipo kisiasa badala ya kuwaza kama jamii. Niliuliza swali jepesi sana je majukumu ya mbunge ni yapi? Na katika udhibiti wa pombe haramu nani aliepo karibu zaidi na udhibiti? Ni mbunge ambaye anapaswa kua mwakilishi wetu bungeni ama ni mkuu wa wilaya, watendaji wa kata, mkurugenzi, jeshi la polisi ama sisi raia tunaoishi pale kijijini?

Nilienda mbali zaidi na kusema inakuaje waliopaswa kufunga na kupiga marufuku kabisa viwanda bubu vinavyozalisha pombe haramu na kuhakikisha hakuna uzalishaji au hata usambazaji wanakua sehemu ya malalamiko?

Hapa nitafafanua kidogo, chukulia mfano vijana waliopo rombo wenda wenye marafiki ama ndugu walioathiriwa na pombe kali wameshindwa kutumia nafasi zao kuwashawishi wahusika waache pombe hatimaye wamegeuka sehemu ya lawama.

Pili vijana hao hao wenye uwezo wa kutambua na kuelewa wamepata taarifa iliyotolewa na mkuu wa wilaya ambaye kiuhalisia hakupaswa kulalamika bali kuchukua hatua kudhibiti badala ya kumpinga mkuu wa wilaya tumejigeuza kua sehemu ya propaganda chafu za kisiasa. Nahisi sisi vijana tuna tatizo mahali fulani.

Tatu kwa kua mkuu wa wilaya anasimamia shughuli mbali mbali wilayani na mkurugenzi kua mtendaji mkuu wilayani walishindwaje kudhibiti uzalishaji na baadaye usambazaji wa pombe haramu? Vijana tunapotea kama hatujui hili

Nne zipo mamlaka za serikali zinazohusika moja kwa moja na udhibiti wa pombe haramu na kwa mkuu wa wilaya kutamka yale maana yake kuna madhaifu katika utendaji wa serikali na baadhi ya taasisi zake. Taasisi kama jeshi la polisi Rombo, mamlaka ya  dawa na chakula(TFDA), TBS na TRA wote hawa kuna madhaifu ya kiutendaji ndio maana haya yakatokea Yani uzalishaji upo usambazaji upo na kisha utumiaji upo alafu idara zipo kimya. Tukienda mbele zaidi tutagundua hadi idara ya uhamiaji ina matatizo ndio maana hata wakenya wakapita mpakani kutoa huduma ya kindoa kwa wanawake wa Rombo. Kama ni kweli.

Tujiulize haya

Moja: Sasa kama mlevi anayekunywa pombe na baadaye kwa kua pombe si salama akapata upungufu wa nguvu za kiume analalamikia ukosefu wa ajira kama chanzo cha ulevi na sababu zingine mnazozijua.

Pili: mke wa kijana yule ama baba yule ambaye anakosa haki yake kama mke wa mhusika naye analalamika kuwa mumewe hawezi kumtimizia haja yake kimapenzi na ni haki yake lakini anaikosa kutokana na kishindwa kwa mumewe

Tatu: vijana ambao hatujaathirika na ulevi ama kwa maneno mengine tumeona tatizo lipo na wahusika ni ndugu zetu wa karibu ama marafiki zetu basi badala ya kushauri hawa jamaa waache pombe na sisi tunalalamika

Nne: mkuu wa wilaya ambaye alipaswa kua sehemu ya suluhisho naye analalamika wakati uwezo mamlaka na mikakati ya kuzuia uzalishaji na usambazaji naye analalamika

TUNATAKA NANI ACHUKUE HATUA?

Mkuu wa wilaya kateleza. Tuache siasa tushirikiane kuijenga Rombo.

NANI AFIKIRI KWA NIABA YAKO?
Wasalaam.

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI