GARI LA MWENYEKITI BAVICHA IRINGA MJINI LACHOMWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA



Pichani ni gari na petrol iliyokuwa tayari kwa kuliteketeza kabisa gari mwenyekiti BAVICHA Iringa mjini

Siasa za aina hii ni hatari kwa ustawi wa jamii zetu, huu sio ungwana kabisa, hakika nilipozipata hizi taarifa za watu kulichoma gari la mwenyekiti BAVICHA IRINGA MJINI Zinenipa masikitiko sana na nimeumizwa sana, nimelazimika kumpigia kujua nini chazo lakin hajaweza kujua nini  chazo cha moto huo na hajajua watu waliofanya tukio hilo. Nimebaki na maswali mengi kichwani ambayo yanakosa majibu
Je waliofanya haya ni wapinzani wake kisiasa?
Je waliofanya haya ni rafiki zake?
Je ni kwanini wamefanya haya?
Je wangemkuta mmiliki wa gari wangemfanyaje?
Je intelegensia ya polisi itawabaini whusika?
Ni kwanini aliyechomewa gari ni kiongozi wa upinzani na nimtia nia udiwani?
Je hii ni vita endelevu au ya mda na nanu mhusika mkuu?

Hayo ni baadhi ya maswali niliyojiuliza hata baada ya kupata taarifa hizi zinazoleta simanzi kubwa kwa wapenda maendeleo,
Namnukuu mumiliki wa gari hiyo mwenyekiti BAVICHA Iringa mjini Bwana Leonce Marto, alisema..."Gari yangu ya chomwa moto usiku huu kwa  PETROLI. Leo saa 6 kamili usiku nimeamka nikakuta gari yangu inawaka moto nje, nilipotoka nje nimekuta dumu la petrol lita tano chini ya gari.....nimefanikiwa kuuzima moto ..."
By M/kiti Bavicha Iringa Mjini

Hebu tafakari mara mia na uone hii ni ishara gani kama si vita baina ya watu wa pande mbili zinazokizana. Maumivu haya sio madogo, naomba nimnukuu makam mwenyekiti BAVICHA Bara na mwenyekiti BAVICHA Isimani pia mtia nia Ubunge jimbo la Isimani kamanda Patrick Ole Sosopi

"Nipo eneo la tukio hapa kwakweli hii ni zaidi ya vita, nipo hapa nyumbani kwa Kamanda Marto baada ya kunitaarifa na kufika.
Tumeshafanya mawasiliano na RPC wa Iringa na RCO ameshawasili hapa"

Kamanda Ole Sosopi alionesha kusikitishwa sana na tukio hilo ambalo limeonekana kuwa ni vita kubwa.

Hadi hapo vita hii sio ya mchezo tunapaswa kupambana haswa
Napenda nichukue nafasi hii kwa niaba ya BAVICHA wilaya ya Iringa vijin nikupe pole kwa matatizo

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI