HEKAHEKA ZA WANAVYUO NA NEC KUHUSU KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

Na Alex Elifurah



Kweli vyuo vikuu tukinyamaza na kutokupiga kura October 2015,itabidi tupimwe akili au tupewe chanjo ya Akili,

Kuelekea October  hii chanjo ni muhimu sana.

waraka wa vyuo vikuu kuomba hatma yao kuelekea uchaguzi mkuu umewasili kwa Jaji Lubuva,Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguzi, na tumefanya NAE mazungumzo ya pamoja na ametupa mrejesho kwa maandishi.


Lazima  vyuo vikuu vijiandae kisaikolojia kupoteza haki yao ya msingi ya kupiga kura kwani majibu ya waraka ule una mapungufu mengi sana.

Mahojiano kati yetu na mwenyekiti wa  Tume ya uchaguzi kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari moja kwa moja amedai zoezi limefeli hivyo ni mapungufu yao.

Maamuzi yetu ni kufungua shauri mahakamani na kupeleka waraka kwa tume ya haki za binadamu baadaya ya Tar 18. August 2015 ambayo ni mwisho ya kuboresha na kuhamisha Taarifa kwa wapiga kura.

Pia kutokana na  rekodi za utendaji mbovu wa tume kwanzia kura za maoni ya katiba,uandikishaji na ukusanyaji wa  taarifa kihesabu kwa kutumia katiba ya nchi tutapeleka ombi tume ya haki za binadamu ili uteuzi mwingine wa mwenyekiti wa tume ya Taifa ya uchaguzi ufanyike mapema.


Mikakati hii ikifanikiwa mapema tutapata uhakika wa kupiga kura.

Tumeamua kujitolea kwa dhati ili kufanikisha haki yetu kikatiba.


Aluta Continua,Victory Ascerta.

Sir Alex Elifuraha(Muhas)
0767528900
Lusekelo Amimu(Ardhi)
0684615128

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI