MH HALIMA MDEE AIBUKA KIDEDEA DHIDI YA SERIKALI JUU YA MGOGORO WA ARDHI JIMBONI KWAKE KAWE ENEO LA CHASIMBA
Na Shindo Isaac
Hatimaye leo Mh Halima Mdee ametangaza rasmi ushindi dhidi ya serikali dhalimu ya chama cha mapinduzi (CCM) juu ya mgogoro wa ardhi uliodumu kwa mda mrefu katika kata ya Bunju Chasimba, serikali imeamua kunyoosha mikono na kuwaachia wananchi hao kuendelea na maisha yao kama ilivyokuwa kabla ya mgogoro.
Hakika mwanadada huyu ambaye ni mbunge wa Kawe na mwenyekiti BAWACHA taifa kaonesha na kadhihirisha kuwa ana uwezo mkubwa na anafaa kuendelea kuwatumikia wana wa Kawe. Kashirikiana vyema na madiwani wake pamoja na wananchi wa Chasimba kwa ujumla hatua kwa hatua.
Mgogoro huu wa ardhi ulikuwa ukiwahusisha wananchi na muwekezaji wa kiwanda cha Cement cha wazo
Wananchi wapongeza sana juhudi binafsi zilizofanywa na mbunge matata Halima Mdee kwa kushirikiana na madiwani makini wa CHADEMA, Janeth Rithe,Deus Mtiro na Esther Samany ambao kwa mda mrefu wameonekana kupanda vilivyo na kuikomalia serikali kuhakikisha inamaliza mgogoro huo kwa maslahi ya ustawi wa jamii
Waliitupia serikali lawama bila kuchoka kwa kuendelea kumkumbatia mwekezaji wa kiwanda hicho huku ikiwatupa wananchi ambao ni wazawa na wamiliki halali wa ardhi hiyo.
Ilipofika saa 7:00 mchana wa leo, Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi pamoja (Mh Wilium Lukuvi) akiongozana na Naibu wake walifika pamoja na timu nzima ya wizara yake, hapakuwa na namna zaidi ya kukubali kuwa wananchi wa Chasimba,Chachui na Chatembo ni wamiliki halali wa ardhi hiyo na sio mwekezaji tena.
Mkutano mkubwa ulifanyika eneo hilo na wananchi wanaselebuka na kumpongeza Mbunge wao na wanajivunia kuwa na mbunge wa aina yake.
Hongera sana kwako Mh Mdee
Aliyesimama ni Mh Halima Mdee Mbunge wa Kawe kupitia CHADEMA, kulia kwake ni Waziri na naibu wake
Wananchi wakisikiliza mwafaka wa mgogoro wa ardhi katika makazi yao, hakika wameona ukombozi kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.
Mh Halima Mdee akiongea na makamanda wake, kushoto kwa Mh Halima Mdee ni mwanadada chipukizi katika siasa Eng. Pamela Maasay, Mwenyekiti BAVICHA jimbo la kawe, Vijana hawa kwa ujumla wameiva haswaaa kuutafuta ukombozi
Hatimaye leo Mh Halima Mdee ametangaza rasmi ushindi dhidi ya serikali dhalimu ya chama cha mapinduzi (CCM) juu ya mgogoro wa ardhi uliodumu kwa mda mrefu katika kata ya Bunju Chasimba, serikali imeamua kunyoosha mikono na kuwaachia wananchi hao kuendelea na maisha yao kama ilivyokuwa kabla ya mgogoro.
Hakika mwanadada huyu ambaye ni mbunge wa Kawe na mwenyekiti BAWACHA taifa kaonesha na kadhihirisha kuwa ana uwezo mkubwa na anafaa kuendelea kuwatumikia wana wa Kawe. Kashirikiana vyema na madiwani wake pamoja na wananchi wa Chasimba kwa ujumla hatua kwa hatua.
Mgogoro huu wa ardhi ulikuwa ukiwahusisha wananchi na muwekezaji wa kiwanda cha Cement cha wazo
Wananchi wapongeza sana juhudi binafsi zilizofanywa na mbunge matata Halima Mdee kwa kushirikiana na madiwani makini wa CHADEMA, Janeth Rithe,Deus Mtiro na Esther Samany ambao kwa mda mrefu wameonekana kupanda vilivyo na kuikomalia serikali kuhakikisha inamaliza mgogoro huo kwa maslahi ya ustawi wa jamii
Waliitupia serikali lawama bila kuchoka kwa kuendelea kumkumbatia mwekezaji wa kiwanda hicho huku ikiwatupa wananchi ambao ni wazawa na wamiliki halali wa ardhi hiyo.
Ilipofika saa 7:00 mchana wa leo, Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi pamoja (Mh Wilium Lukuvi) akiongozana na Naibu wake walifika pamoja na timu nzima ya wizara yake, hapakuwa na namna zaidi ya kukubali kuwa wananchi wa Chasimba,Chachui na Chatembo ni wamiliki halali wa ardhi hiyo na sio mwekezaji tena.
Mkutano mkubwa ulifanyika eneo hilo na wananchi wanaselebuka na kumpongeza Mbunge wao na wanajivunia kuwa na mbunge wa aina yake.
Hongera sana kwako Mh Mdee
Pitia kwa makini
ReplyDelete