MAALIMU SEIF AAHIDI KUNGANISHA UNGUJA NA PEMBA ENDAPO ATACHAGULIWA
Makamu wa kwanza warais wa Zanzibar na mgombea wanafasi ya urais kupitia chama cha wananchi CUF Maalimu Seif Sharifu Hamadi ameahidi kuwaunganisha wakaz wa visiwa vya unguja na pemba.
Ahadi iyo ameitoa mchana leo katika viwanja vya Timiliza, Chakechake Pemba wakati wakutambulishwa kama mgombea wakiti cha Urais kupitia tiketi ya chama cha CUF Zanzanibar.
Maalim Seif amesema endapo wanachi watampa ridhaa yakuwa Rais atahakikisha anaweka boti ambazo zitafanya safari zake kati ya Unguja na Pemba wakati wote ili wakulima waweze fanyabiashara zao kwa urahisi zaidi.
Amesema kuwa uwepo wa boti izo itasidia shughuli mbalimbali katika jamii ya watu wa zanzibari nakusema kuwa ndio njia pekee itakayoleta mwilingilino baina ya waunguja na wapemba.
Aidha Maalim Seif amesema kwasasa wazanzibari wanatakiwa kuwa wamoja ili waweze kukiondoa Chama Cha Mapinduzi(CCM) ambacho kimeonekana kushindwa kuleta umoja.
"Nduguzangu sasa nikipindi chakuwa pamoja na kuhakikisha tunaungana ili tuweze kuinyoa CCM ambayo imekuwa madarakani kwamuda mrefu lakini hawaja fanyalolote la msingi hadi sasa", alisema Maalimu Seif.
Mbali na boti izo Maalimu Seif amesema akichaguliwa kuwa Rais atahakikisha anatoa kodi katika bishara ya mchele ili chakula icho pendwa kwawakazi wa Zanzibari kipatika kwabei rahisi tofauti na ilivyosasa.
Comments
Post a Comment